11/04/2023
👉Ukishindwa kunielewa hapa basi wakati utakuelewesha
👉Zama zimebadilika sana ,, tupo kwenye hatua ya kupambania maendeleo binafsi tofauti na zamani tulikuwa tunapambania maendeleo ya kikundi,,,
👉mfano zamani kwenye uko wenu kukiwa na mtu mmoja mwenyewe pesa basi ukoo mzima unaheshimika na kuonekana wote mnapesa
👉Narudia tupo kwenye zama za kupambania mafanikio binafsi sio mafanikio ya kikundi k**a zamani ,,,
👉leo hii mtu anakupa fursa ni kwel unatamani kujiunga ila huna mtaji na alie kupa fursa yeye huenda anatengeneza dollar 100$ kwa siku ila hawezi kukupa hata dollar 26 za kuanzia biashara.
👉Tunazijenga tabia kisha tabia zinatujenga ,,, usipo tuliza kichwa kwa sasa na kutazama upo kwenye nyakati kagi basi utaendelea kuumia zaid na zaidi,, utaona watu wanaringa na pesa zao ,, utaona marafiki wabaya nk ,, hapana wapo sahihi kabisa no money no frends ,,, no opportunity no campan...
👉Ndio maana unaona k**a unafanya mchongo flan na mtu flani ,, siku mchongo ukifika tamati kila mtu anaendelea na time zake ....
👉Ndege wanao fanana huruka pamoja ,, dunia ya sasa kuliko mtu akupe pesa bora akupe fursa hakuna mtu anataka kubeba matatizo ya mwingine ,,, kila mtu apambane na hali yake ,, tunaweza kuona ni ubaguzi ila ili tupige hatua ya kimaendeleo mtu mmoja mmoja ni lazima hatua hii itumike , hata kwa wenzetu wametumia sana hii slogan ndio maana wako mbali kimaendeleo
👉Dunia ya sasa ni dunia ya kupeana fursa ,,, Dunia ilipo fikia sasa ni nyakati za kupewa ndoano ukavue mwenyewe samaki.
👉Unapewa fursa tu mengine utajiongeza mwenyewe ,, mtu yeyote anaetaka kupiga hatua binafsi huwezi pata pesa yake kizembe
👉Ukiona mtu anakupa pesa free jiulize maswali kuna mtego mahali ,, kila mtu anaekuwezesha anatazamia return ya alicho kitoa ,, hakuna mjinga kwa sasa ,, ukiona huzaminiki kwa sasa basi jua huna msaada wowote kwa mtu.
By Mr Revolution🎯