Timo M

Timo M Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Timo M, Business service, Kariakoo, Narung'ombe Street, Dar es Salaam.

05/02/2024

*Anaandika Baba Askofu Benson Bagonza kuhusu kifo cha Kada wa CCM Thadei Ole Mushi*

1. Nimeumizwa sana na kifo chake.

2. ⁠Aliwahi kutetea hadharani haki yangu ya kuishi.

3. sikuwa nakubaliana naye mambo karibu yote isipokuwa moja: haki yake ya kusema na kutoa mawazo yake.

4. Hakuwa mvumilivu wa hoja zilizoonekana kuwa nguvu dhidi ya chama chake. Alikuwa tayari kupotosha hoja kinzani bila kunoa ya kwake ikubalike.

5. Niliumia mno alipotokea hadharani kukanusha na kuwazodoa waliokuwa wakituhumu mchezo mchafu juu ya kuugua kwake.

6. k**a kulikuwa na robo ukweli ktk tuhuma zile, basi watesi wake walimtumia kuwasafisha. Hakuna wa kuwachafua sasa.

7. Kwa msimamo wake wa kutetea uhuru wa maoni, alitengeneza maadui ndani ya chama alichokuwa anakitetea.

8. chama chake kinawaheshimu na hata kuwalinda wanaokikosoa wakiwa nje kuliko kinavyoweza kuwavumilia wanaokikosoa wakiwa ndani.

9. Wanaosema hakuwa chawa, hakupenda uteuzi na alijisimamia, wafikiri upy na kupitia maandiko yake.

9. k**a hakuwa chawa basi hatuna chawa.

10. Katika ombwe la fikra pevu miongoni mwa vijana wanaojihusisha na masuala ya siasa, alikuwa pekee kutumia muda wake kuandika na kujadili bila kutukana. Hatunao wengi.

Familia imempoteza mtu muhimu mapema.
Chama chake kimempoteza Mwenezi mwenye hoja kuliko yule.
Wizara ya elimu imempoteza mwalimu hodari aliyeitetea kazi yake.

Kwa heri Ole Mushi. Umeacha nchi gizani, unaenda kaburini penye giza. Yawezekana hakuna ulichopoteza hata k**a sisi twaweza kuwa tumepoteza.

RIP Ole Mushi

04/02/2024

Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza anena

KATIBA na SHERIA: Nani Zaidi?

Nimesikia Bunge limeridhia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) sasa iitwe Tume HURU ya Taifa ya Uchaguzi (NFEC?!)

Yaani kuongeza neno HURU kumeleta uhuru wa Tume. Kazi Iendelee. Lakini?

1. Ikiwa katiba inatamka ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi na hii ikaitwa ni Tume HURU ya Taifa ya Uchaguzi, si vyombo viwili tofauti hivi?

2. Je tutakuwa na chaguzi mbili - moja ikisimamiwa na Tume Huru na mwingine ukisimamiwa na Tume isiyo Huru?

3. Au kuna mpango wa ama kuingiza tume Huru kwenye katiba na kuondoa isiyo huru?

Vyovyote iwavyo, namlaani aliyependekeza Bunge letu libinafsishwe kwa DP World! Anahitaji kupimwa akili kwa sababu alikosea kwa kuleta hili pendekezo.

Bunge letu tukufu lina akili nyingi na lina viwango vya juu sana. Neno HURU lina upako wa kuondoa shida za tume ile iliyozoea kuchakachua chaguzi zetu.

Address

Kariakoo, Narung'ombe Street
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Timo M posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share