24/01/2020
Name: SAFARI
SEASON 2: episode 11
Nilihisi roho inatoka kwa jinsi sasha alivyozidi kunikaba......
"Hapana usimuue kaka yangu tafadhali nakuomba!!!!!.."
Sharifa alilia sana huku fred na bababyangu wakimzuia asisogee pale nilipo, na jeri akimzuia mama yangu kwani walijikuta wanalia sana kwa jinsi nilivyozidi kunyong'onyea pale mikononi mwa sasha.
Ghafla alinitupa chini kisha akarudi nyuma kisha akawaambia wale watu wake wanichukue na wanipeleke anapoelekea yeye.wale watu walinibeba nisijue naenda wapi kwani nilikuwa na maumivu shingoni, ndugu zangu walitamani kunifata lakini walizuiwa na wale mijitu.
Tuliingia kwenye chumba ambacho kulikuwa na vitu vingi vya ajabu, hasahasa kulikuwa na vyungu vingi vilivyoandikwa majina ya watu nilishangaa kuona vile vitu kwasababu sikuwahi kuviona kabla.
Nilitupiwa kwenye kiti kwa kishindo kisha sasha akawaamuru wale watu waondoke ili tubaki wawili, sikujua anataka kunifanya nini!!.ghafla nikahisi mikono yangu imenasa katika kiti bila hata ya kufungwa kamba, kumbe ulikuwa ni uchawi wa sasha .
"Wewe ni jasiri sana na una nguvu nyingi katika mwili wako ila bado hazitoshi kukufanya uwe shupavu kuliko wote hahaha!!" Sasha aliongea huku k**a ananinong'oneza skioni kisha akainuka,
"Una maana gani,? Na unataka kunifanya Nini hebu nifungue hapa!"
"Hahaha ndio maana nikakwambia Bado Nguvu zako hazitoshi!! ...ila nataka nikupe Nguvu zaidi na utakuwa na uwezo wake kutoka Hapo ulipo kwa urahisi!"
Niligundua kabisa kuwa huyu alitaka kunipandikiza Nguvu za kichawi katika mwili wangu ili aweze kunitumia katika kazi zake.
Sikuwa nabuwezo wa kupinga kwasababu alinifunga mdomo nisiongee chochote pale nilibaki kufurukuta bila mafanikio,
Sasha alienda mpaka kwenye p**a na kuchukua chungu kimoja kidha akachukua na kisu cha kishetani na kunisogelea tena, aliongea lugha zake zisizoeleweka kisha akanichana katoka mkono wangu na kishabakawa anakinga damu yangu kuingia kwenye kile chungu nilihis maumivu ila nilishindwa kutoa sauti
Kisha akaamua kata na yet na akaikinga damu yake mulemule Kisha akaanza kuikoroga ili zichanganyike, nilianza kuhisi mabadiliko ndani ya mwili wangu Kisha naye akakichukua kile chungu na kukiweka kwenye kabati K**a vile vyungu vingine vilivyoandikwa majina kishabkile chungu kikaanza kujiandika chenyewe kichawi likatokea jina langu katik kile chungu MASON
Hivyo bas nikagundua kabisabhata wale walinzi wenye minguvu wote walipitia hapa nilipo mimi basi nikapata wazo la kufanya lakini sikuweza kutoka pale nilipokuwa.
Ghafla nilihisi kabisa kunabroho ya kishetani imeingia ndani ya mwili wangu.
Baada yabhapo alinifungua nikiwa sijielewi yaani najitambua mimi ni binadamu lakini nilijihisi pia mimi ni shetani mtarajiwa.
Tulifika mpaka pale walipokuwa wenzangu ili aweze kunitambulisha k**a mfuasi mpya wa sasha nilisimama k**a sanamu nisiweze kutingishikabhata kidogo. Alianza kuzungumza lung'a za ajabu kisha wale walinzi woote wakapiga magoti ili kukaribishwa mfuasi mpya wa sasha. Lile ndilo lilikuwa zoezi la mwisho na k**a likisitishwablile zoezi basi hakua kitakachotekea basi aliendelea kuongea lugha zake na moshi ukiwa unatoka chini ya ardhi kuja juu..
Alikuja mlinzi mmoja nabkumpa sacha tunguli moja nyeusi ambayo huwa inatumika kwaajili ya kukaribisha watu wapya na bila kile kitunguli basi hawezi kubadilika kabisa.
Basi alikinyanyua juu na kuendrlea kuongea , ndipo yule binti jasiri alipoona kuwa hawezi kukaa kuendelea kuona ushetani unaendelea kwakuwa walinzi wamepiga magoti nabvichwa wameinamisha aliinuka na kwrnda kuchukua jiwe la wastani kisha akalirusha kwa hasira na kupasua kile kitubguli alichoshika sasha,,....sasha alikasirika lakini hakujua ni nani alirusha jiwe ghafla zikasikika sauti za mashetani yakilia nyumba nzima na mimi nilikosa nguvu kwani nilidondoka mpaka chini.. sasha aliwafata wale watu na kuwauliza ni nani karusha jiwe hakuna aliyejibu bas hakupoteza klmuda alimk**ata baba mmoja na kuanza kumkausha sasa wakati anafanya hivyo yule bint jasiri alinifata huku watu wakiwa wanakimbia kimbia wasijue wakimbilie wapi
"Mason mason....amka mason"
Nilisikia jinsi alivyokuwa ananiita nilijikuwa nanyoosha mkono upande wa kile chumba tulichokuwa mimi na sasha huku nikisema
"Kab..kabati...n..na vyu..vyungu..vun..vunj!"
Kisha nikapoteza fahamu
"Nivivunje!!!"
Yule binti alijiongeza na kuinuka kukimbia kuelekea kwenye kile chumba huku walinxi wakimkimbiwa kwa kasi
Alifika ndani akalionna lile kabati ni kubwa kuliio mwili wake lakini akalisogelea na kuanza kulisukuma. alilidondosha mpaka chini nabvyungu vyote kupasuka......
COMENT LIKE SHARE TUSONGE 12