25/08/2026
Wakati mwingine tunadhani biashara inahitaji kukua haraka.
Orders zaidi.
Wateja zaidi.
Wafanyakazi zaidi.
Matawi zaidi.
Lakini kuna swali tunapaswa kujiuliza kwanza:
“Je, mfumo wetu uko tayari kubeba hiyo growth?”
K**a leo unashindwa kuhudumia wateja 20 vizuri, kupata wateja 100 hakutatatua tatizo.
Kutakuwa na malalamiko zaidi.
Makosa zaidi.
Madeni zaidi.
Pressure zaidi.
Kwa sababu growth haifanyi mfumo mbovu kuwa mzuri.
Inaufanya udhaifu wake uonekane zaidi.
Ndiyo maana wakati mwingine si lazima ukimbilie kukua.
Kwanza tengeneza uwezo wa kubeba kile unachotaka kukua nacho.
SOKONI #034
Kukua kabla ya kuwa tayari ni kuongeza tatizo.