27/01/2024
KWA NINI HUPATI MAOKOTO ?
Kupanga ni kuchagua - wahenga waliandika. nawakubali sana WAHENGA. Zamani sikujua maana ya hizi methali za wahenga. Na nilipozifuatilia nikashindwa kujua hawa wahenga ni watu gani.. ndipo kijana mdogo wa miaka 20 akaniambia⦠WAHENGA NI WAZEE WALIOISHI NA KUONA YAKITOKEA NA KUANDIKA. nami nimeamua kuwa MHENGA kwa Kuandika niliyoyaona Yakitokea
Kuna sababu KUU moja tu kwa nini mpaka sasa HUJAFANIKIWA
Ni kwa sababu hujapanga / ama hujatekeleza ulichopanga kufanya.
ANGALIA
-Mungu alikupangia Baraka kabla hajamuumba Adam
Mwanzo : 1 : 26 - Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
-hapo utaona MUNGU anawaza na kutamka Baraka kabla hajamuumba Adam.kwamba Adam na Uzao wake wawe WATAWALA. Wamiliki Uchumi. Na kumbuka ww umetokana na Adam na hivyo baraka za Mungu kwa Adam ni zako pia
-Serikali hupanga bajeti ya maendeleo ya taifa lake kabla mwaka wa matumizi haujaanza
-serikali hupanga mipango na Dira ya miaka 25
-makampuni na mashirika hupanga mipango ya muda mfupi na mrefu na kuifuata
β JE WEWE UMEPANGA NINI KWA MWAKA HUU ?
β JE UMEWEKA MITEGO IPI YA KUNASA FEDHA ambazo serikali imepanga kutumia katika bajeti yake ?
β Serikali imepanga kutoa tenda mbali mbali ktk miradi mbali mbali.. je ww umepanga biashara gani ya kunasa hizo fedha?
β Mashirika na kampuni mbali mbali zinapanga kufanya manunuzi mbali mbali je unacho kitu cha kuwauzia ?
β Je unayo huduma ya kutoa ?
β Watu wanapanga kufanya matumizi na manunuzi mbali mbali ..je una nini cha kuwauzia ?
β Adui zako nao wanapanga kukuangusha chini ili uendelee kuwa chini
β Je ww umepanga kufanya nini cha kukuinua juu?
β Yawezekana ni ww pekee ambaye hujapanga chochote
β Yawezekana ni we ndio hupangi chochote katika maisha yako na hivyo hupati chochote kwa kuwa hupangi chochote
β Kawaida ili upate kitu unatakiwa kupanga kabla hakijatokea
β Mkulima anayepanga kuvuna kilo 10,000 ili ajipatie 40 milioni hupanga miezi 12 kabla mavuno hayajatokea na huanza utejelezaji miezi 6 kabla ya kuvuna
β Huandaa mbegu, huandaa shamba, huandaa mbolea, huandaa dawa za wadudu, kisha muda wa kulima ukifika huingia shambani miezi kadhaa kabla kwa kufyeka,kulima, baadaye kupanda, kupalilia,kuweka mbolea, kupiga dawa, hatimaye KUVUNA na Kuuza na kujipatia fedha
β Mfanyabiashara wa NGUO anayetaka kupata fedha kwa kuuza nguo katika msimu wa sikukuu hupanga miezi 6 kabla. Huweka oda miezi 4 kabla ya msimu china. Anajua mzigo unasafiri kwa miezi 2. Anajua ili auze vzuri mzigo unatakiwa kufika mwezi mmoja kabla ya sikukuu ili wateja wa mikoani wanunue mapema na kupeleka mikoani.
β Yaani baraka Za Mungu unatakiwa uzipangilie kabla hazijatokea
β Hiyo inaonyesha huwezi kupata bila kupanga akilini
β Amka akilini .. jipangie unachotaka kupata mwaka huu, ingia kutekeleza ulichopanga na hatimaye utapata fedha
β Bila kupanga Akilini na kuingia kutekeleza hutapata matokeo
β Amini usiamini.. hupati kwa kuwa hujapanga na kuingia kutekeleza
β Ama unapanga lakini huingii katika kutekeleza
β Mungu hubariki UTEKELEZAJI wa mipango ya Kazi za mikono Yako
β Kuna wengine hupanga ila hawaingii katika kutekeleza
β Baraka za Mungu zipo zinazunguka zunguka kutafuta mtu aliyepanga kuzinyakua
β Kuna Mabilioni ya fedha yanazunguka zunguka kutafuta mtu aliyeweka mtego wa kuzinasa
β Waliojipangia mipango na kuitekeleza ndio wanaozipata
β K**a hujapanga chochote na kutekeleza hutazipata
β Kuna Mabilioni na Mabilioni ya Fedha yatatoka nje ya nchi na kuja tanzania miezi 4 ijayo ili kutafuta UFUTA..
β watakaopata hizo fedha za Ufuta na mbaazi na choroko na dengu ni waliopangilia na kuandaa kulima
β Hata mie nimepanga kuzipata na hivyo tayari nimenunua mbegu, ninaandaa shamba la kupanda ili mwezi wa 2 nianze kupanda
β Hakuna kupata k**a hujajiandaa na kutekeleza
β Hakuna kupata k**a hujapanga KUPATA
β Kuna mabilioni na mabilioni ya Fedha yatafurika ili kutafuta mahitaji wakati wa Mfungo wa Ramadhani na sikukuu ya IDDI na PASAKA miezi miwili ijayo
β Watakaozipata hizo fedha walijiandaa mwaka mmoja uliopita kuzipata
β Watu walipanda mihogo mwezi wa tatu mwaka jana ili wavune mwaka huu mwezi wa tatu wakati wa mfungo
β Watu wameagiza tende na mguo zinazoambatana na mfungo
β Mayai yatapanda bei na maziwa .. kuna watu walijiandaa kufuga kwa ajili ya kulenga hii sikukuu kubwa
β Je ww ulipanga Nini na Umetekeleza nini ili kujiandaa KUNASA FEDHA zinazotafuta huduma mwezi wa 3?
β K**a hukupanga na kuandaa hutapata kitu
β K**a hukupanga na kuandaa nguo za kuuza, Viatu, Vyakula, vyombo nk mabilioni hayo ya sikukukuu za IDDI NA PASAKA zitakupita
β Kisha utamlaumu MUNGU kwamba hajakubariki. Kumbe MUNGU alikubariki Afya na uzima na akili njema ila HUJAPANGA KUCHUKUA HUO MBARAKA
β Tambua Afya njema ya kimwili na kiakili ndio Baraka kuu kuliko zote ambazo MUNGU amekupa
β Kumbe Tatizo ni ww mwenyewe hujatumia Baraka KUU ya MUNGU ya uzima kujipatia maokoto
β Je lini utaanza kupanga kabla hujapata?
β Tambua bila kupanga mapema hakuna kupata mbeleni
Dr. PHARES JOHN
27/01/2024