King's Brains

King's Brains We Serve All who need to Grow Big from Small...
Contact us : [email protected]

03/09/2013

Ukitaka kufika mahali ambapo hujawahi kufika..Lazima ufanye kitu ambacho hujawahi kukifanya..!!!

16/07/2013

Ukweli kuhusu Ujasiliamali...

1. Unajidanganya k**a utaingia ujasiliamali ili uwe bosi wa nafsi yako...Ukweli huku wateja ndio mabosi wako wakubwa. watakufanyisha kazi hadi Usiku.....

2. Utakosea k**a unataka ujasiliamli ili urelax na kukwepa stress za boss, ukweli ni kwamba huku hakuna kurelax wala kupumzika. Muda wote unakuwa muda wa kazi hata k**a ni usiku maana wanaorelax ni wale tuu waliozipata pesa tayari.

HATA HIVYO KARIBU SANA TENA JIPE MOYO MKUU MAANA NI UKWELI PIA HAKUNA MTU ALIYEWAHI KUTAJIRIKA KWA MSHAHARA....Mtafute ukimpata niambie nami nitakupa zawadi ya fedha Taslimu Milioni moja..MSHAHARA HUWA HAUKUI, NDUGU YANGU ZINDUKA...!!! !K**a unaamini niliyosema basi Karibu sana katika Uwanja wa kujiajili....
Halikuwa kosa lako kuzaliwa Masikini, lakini Ole wako utakayekufa ukiwa maskini..!!! Usiogope kuanguka..maana Kabla hujaanza kutembea ulianguka mara nyingi mno, tena hata aliyegundua taa za umeme alijaribu takribani mara 500 ndipo alifanikiwa alichokikusudia...

12/07/2013

Vijana wa Kitanzania , Sasa ndio wakati wa kuamka na kutafuta maisha kwa nguvu. Ni wakati wa kila mmoja kutafuta kutimiza ndoto zake yeye mwenyewe.. Hatuna sababu ya kusinzia....Ni wakati wa kufikiria kujiajili zaidi...Usiwaze kila siku kuwa mteja.....Hebu tujaribu kufikiria kuwa na sisi tuanze kuhudumia wateja..Haina maana kuendelea kukaa tukiwaza kuajiriwa huku wachina wakija na kujiajili katika chi yetu wenyewe tena katika huduma na sekta tunazoweza kujiajili wenyewe.......Hatuna haja ya kuona haya. Hata k**a fursa iliyopo ni kuzoa taka, ukiona unaweza kuifanya kwa njia tofauti anza SASA.. Nawakaribisha wooote katika Kuanza kujitegemea kifikra na kiuchumi..KUMBUKA..Uhuru na furaha ya kweli hutimia pale unapokuwa huru kiuchumi.. NAKARIBISHA MAWAZO MAPYA YENYE KUJENGA

Address

Plot Number 642
Dar Es Salaam
54337,DSM

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when King's Brains posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share