07/01/2017
Habari ya Leo:
BAADHI YA WATU WANASHINDWA KUFANIKIWA KWA SABABU HIZI MBILI YAMKINI ZIPO NYINGI MIMI NIMEONA HIZI MBILI:
• Jambo la kwanza:
Kutokujuwa kile unachotakiwa kufanya hasa kwa utulivu na uzuri
Maana hii upelekea wengi kushindwa kufanikisha ndoto zao kabisa iwapo, ujuwi kile unachokitaka vizuri, suala la kufanikisha ndoto zako litakuwa gumu kidogo.
Mambo ya kuzingatia katika swala hili la Kwanza:
Ili uweze kufanikisha ndoto zako lazima kile kitu unachokitaka uweze kukijua vizuri.
Hakikisha unajuwa njia utakazotumia hadi kukipata kitu hicho.
Usifanye kosa la kubebesha mambo mengi katika ubongo wako.
• Jambo la Pili:
Kukosa hamasa kwa kitu unachokitaka. Maana kubwa kuhamasika/Uzingativu Fulani katika jambo husika ni kitu cha muhimu sana ili kufikia ndoto zako kubwa.
Mambo ya kuzingatia katika swala hili la pili:
Fanya kila ufanyalo katika kufanikiwa hakikisha una hamasa ya kufanya hicho unachotaka kukifanya katika maisha yako na kiweendelevu.
Endelea kusonga mbele usisubiri hamasa yako kupoa au kupozwa tafuta hamasa ya kufanikiwa kwako, kila siku na ukifanya hivyo mafanikio yako jirani sana kukufuata.