JuHas food product service

JuHas food product service pata huduma ya vyakula lakini pia ushauri mbalimbali juu ya vyakula na mche ya matunda na elimu juu ya chakula unachokula na tiba yake katika mwili hapa juhas

15/10/2022

Kula vizuri

27/07/2022

Ishi ukweli wako. Onyesha upendo wako. Shiriki shauku yako. Chukua hatua kuelekea ndoto zako. Tembea mazungumzo yako. Ngoma na imba kwa muziki wako. Pokea baraka zako. Ifanye siku ya leo ikumbukwe.-

20/01/2022
DAWA MBADALA 9 ZINAZOTIBU VIDONDA VYA TUMBO:Chagua dawa 3 kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri ...
31/07/2021

DAWA MBADALA 9 ZINAZOTIBU VIDONDA VYA TUMBO:

Chagua dawa 3 kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri haraka zaidi. Sasa usinywe zote wakati mmoja, moja tumia asubuhi, nyingine mchana na nyingine jioni. Kumbuka usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari.

1. UNGA WA MAJANI YA MLONGE

Mlonge ni mti mhimu sana katika utabibu k**a tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali. Mlonge una kiasi kingi cha vitamin C, Madini ya chuma, protini, Vitamini A na potasiamu.

Ongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni. Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi au unaweza kuuchanganya kwenye chakula k**a vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo.

2. KABEJI

Kabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.

Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U mhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.

*Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.

*Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.

*Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.

3. NDIZI

Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo ‘H. Pylori’.

Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo.

Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula walau ndizi zilizoiva 3 kwa siku.

Au menya ndizi 2 au 3 na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa. Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa wiki 2 hivi.

4. N**I

N**i ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. N**i huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la n**i na maji ya n**i (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.

Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la n**i au maji ya n**i kila siku. Pia unaweza kuitafuana n**i yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki 2 ili kupata matokeo chanya.

Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya n**i asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki 2 hivi.

5. UWATU

Uwatu unajulikana sana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi mengi mwilini. Unaweza pia kuutumia katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwakuwa uwatu inayo gundi maalumu au ulimbo ambayo huulinda ukuta wa tumbo kwa kuufunga au kuufunika k**a utando na hivyo kurahisisha hatua za kutibu vidonda vya tumbo.

Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji, chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 kwa wiki 2 au zaidi.

Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu ukichanganya kwenye kikombe cha maziwa ya moto.

Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2 kwa siku kwa wiki 2 au zaidi.

Ingawa maziwa hayashauriwi sana kutumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, hivyo unaweza kutumia maji ya uvuguvugu badala ya maziwa k**a vidonda vyako vimeshakuwa sugu sana au ikiwa unahitaji upate nafuu ya haraka na hatimaye kupona.

6. ASALI MBICHI

Asali mbichi, ile nzuri kabisa ambayo haijachakachuliwa inao uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. K**a ujuavyo asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho k**a ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.

Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4. Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.

7. KITUNGUU SWAUMU

Kitunguu swaumu pia husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Watafiti katika kituo cha utafiti wa kansa cha Fred Hutchinson Cancer Research Center in Seattle waligundua kuwa uwezo ambao kitunguu swaumu unacho katika kudhibiti na kuua bakteria mbalimbali mwilini unaweza kudhiti pia bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo ajulikanaye k**a Helicobacter Pylori (H. pylori).

Chukuwa punje 6 za kitunguu swaumu, menya na ukate vipande vidogo vidogo kisha umeze pamoja na maji vikombe viwili kutwa mara 1 kwa wiki 2 au 3

8. MKAA WA KIFUU CHA N**I

Mkaa pia hutibu vidonda vya tumbo hasa mkaa utokanao na vifuu vya n**i. Chukua vifuu vya n**i vitano au kumi vilivyokauka, viweke juu ya jiko la mkaa au popote na uvichome moto, mwishoni chukua mkaa wake usage kupata unga, kisha chota kijiko kikubwa kimoja na uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji changanya vizuri na unywe kutwa mara 3 kwa wiki 2 au 3.

9. MAFUTA YA HABBAT SODA

Ni moja ya dawa za asili chache zinazoweza kutibu vidonda vya tumbo moja kwa moja. Tafiti nyingi zinathibitisha mafuta ya habbat soda yanatibu aina zote za vidonda vya tumbo!

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hadi siku 60 hasa habbat soda grade 1. Vidonda vya tumbo pia upate unga wa asili wa majani ya mlonge na mbegu za maboga kwa matokeo mazuri na ya uhakika, kumbuka pia kunywa maji mengi ya kutosha kila siku, epuka pia vinywaji na vyakula vyenye asidi nyingi.

Share page yetu kwa kupata taarifa zaidi za afya.

najua kukaa nyumbani inachosha lakini rafiki karibu juhaspapaya tukupe miche bora ya papai ili upokuwa nyumbani unaendel...
05/05/2020

najua kukaa nyumbani inachosha lakini rafiki karibu juhaspapaya tukupe miche bora ya papai ili upokuwa nyumbani unaendelea kujifunza kuingiza pesa
karibu kwa oda ya miche bora kwa namba
0717290674
pata ushauri juu ya kilimo cha matunda na jinsi ya kuingiza faida

Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica ...
19/04/2020

Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica papaya

Papai ni moja ya matunda ambayo huchukua muda mfupi hadi kufikia mavuno. Huchukua muda wa miezi 8-9 kufikia mavuno.
Matunda katika mpapai utokeza katika kila jani na mpapai kwa wiki moja unauwezo wa kutengeneza majani mawili na kwa makadilio mpapai huanza kutengeneza maua katika jani la 32 hii ikimaanisha ni baada ya wiki nne.

FAIDA KIUCHUMI
Hekari moja inauwezo wa kuwa na mipapai 1000-2500. Mavuno ya mapapai kwa miezi 8 - 9 kwa mavuno ya kwanza ni tani 40 - 60 ikiwa kila mpapai unaweka matunda 40 hadi 50 kwa miezi 8 - 9. Baada ya mavuno ya kwanza, mavuno ya mapapai hayana msimu hivyo yataendelea ndani ya miaka mitano katika uangalizi mzuri wa mipapai yako hadi kufikia kipindi ambacho mpapai wako utapokufa..

JINSI YA KUJUA FAIDA
Kwa matunda 40 - miti 1000 jumla ya matunda 40,000 yatavunwa
Bei ya papai Tsh. 500 kwa papai
500 x 40,000 = 20,000,000/=
Hivyo kwa kila mwezi ni tsh. 2,500,000/= kwa mipapai ya miezi 8 kufikia mavuno.

Mahitaji
Mahitaji ya mipapai kwa mwezi hayazidi 500,000/-= hivyo unauhakika wa kupata faida ya 2,000,000/= kwa mwezi kutokana na zao la mapapai.

Muhimu: Maelezo hayo ni kwa ufupi na kwa bei ya kawaida sana na bei ya papai lenye kilo nzuri huzidi hapo. Pia mavuno huweza zidi hapo kwa maana hiyo faida huenda mbali zaidi ya hapo.
KWA MAHITAJI YA MCHE BORA YA MIPAPAI KARIBU JUHASPAPAYA KWA PIGA 0717290674

Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai we...
11/04/2020

Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya k**e ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.

Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya k**e tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.
UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI
Miche ya mpapai
Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika: -
1. Mbegu za Kawaida (Local seeds)
Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote. Hivyo itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya k**e.
2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya k**e na ya kiume pamaoja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1, MALAIKA F1 n.k.
Upandaji
kwa mahitaji ya miche bora ya juhaspapaya inakuletea pamoja na ushauri piga +255717290674

Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica ...
09/04/2020

Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica papaya

Papai ni moja ya matunda ambayo huchukua muda mfupi hadi kufikia mavuno. Huchukua muda wa miezi 8-9 kufikia mavuno.
Matunda katika mpapai utokeza katika kila jani na mpapai kwa wiki moja unauwezo wa kutengeneza majani mawili na kwa makadilio mpapai huanza kutengeneza maua katika jani la 32 hii ikimaanisha ni baada ya wiki nne.

FAIDA KIUCHUMI
Hekari moja inauwezo wa kuwa na mipapai 1000-2500. Mavuno ya mapapai kwa miezi 8 - 9 kwa mavuno ya kwanza ni tani 40 - 60 ikiwa kila mpapai unaweka matunda 40 hadi 50 kwa miezi 8 - 9. Baada ya mavuno ya kwanza, mavuno ya mapapai hayana msimu hivyo yataendelea ndani ya miaka mitano katika uangalizi mzuri wa mipapai yako hadi kufikia kipindi ambacho mpapai wako utapokufa..

JINSI YA KUJUA FAIDA
Kwa matunda 40 - miti 1000 jumla ya matunda 40,000 yatavunwa
Bei ya papai Tsh. 500 kwa papai
500 x 40,000 = 20,000,000/=
Hivyo kwa kila mwezi ni tsh. 2,500,000/= kwa mipapai ya miezi 8 kufikia mavuno.

Mahitaji
Mahitaji ya mipapai kwa mwezi hayazidi 500,000/-= hivyo unauhakika wa kupata faida ya 2,000,000/= kwa mwezi kutokana na zao la mapapai.

Muhimu: Maelezo hayo ni kwa ufupi na kwa bei ya kawaida sana na bei ya papai lenye kilo nzuri huzidi hapo. Pia mavuno huweza zidi hapo kwa maana hiyo faida huenda mbali zaidi ya hapo.
KWA MAHITAJI YA MCHE BORA YA MIPAPAI KARIBU JUHASPAPAYA KWA PIGA 0717290674

Karibu kwa huduma ya juhaspapaya ohhh miche bora kabisa😀😃😃🥰🥰
03/04/2020

Karibu kwa huduma ya juhaspapaya ohhh miche bora kabisa😀😃😃🥰🥰

Address

Ubungo
Dar Es Salaam
-KIBAMBA

Opening Hours

Monday 09:00 - 23:00
Tuesday 09:00 - 23:00
Wednesday 08:00 - 23:00
Thursday 08:00 - 23:00
Friday 08:00 - 18:00
Sunday 08:00 - 23:00

Telephone

+255717290674

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JuHas food product service posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to JuHas food product service:

Share