12/08/2021
Story:AFRROAMERICA
Mtunzi:Fahamuelson Tz
Episode:1
Simulizi yetu inaanza ikituonesha kijana mmoja aitwaye Martin akiwa na wazazi wake wakimsindikiza kuelekea air port ili aweze kusafiri kuelekea marekani kwa ajili ya masomo yake, kiuhalisia alipata scholarship ya kwenda kusoma nchini humo,wakiwa bado kwenye safari kuelekea uwanja wa ndege mama yake Martin alimwambia mwanaye “mwanangu kuna jambo la muhimu nnalotaka kukuambia, naelewa ya kwamba kwa sasa umepiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako na hadi kupata nafasi hii hadimu sina budi kufurahia mafanikio yako mwanangu hivyo basi nakusihi ukifika huko usije ukasahau ulipotoka kwakuwa vijana wengi sana hubadilika na kusahau nyuma yao mara baada ya kufika matawi ya juu, nina mengi sana ila hili ni la msingi sana zingatia" mama alimsisitizia mwanaye jambo hilo na Martin alimuahidi mana yake kutekeleza swala hilo, baba naye hakuwa nyuma alimwaambia"Martin mana yako yupo sahihi kabisa ila mimi k**a kila siku ninavyokuambia heshima ni kitu chenye thamani katika maisha heshimu kila mtu bila kujali rika, jinsia wala hadhi please mwanangu do as i say alafu utaona matunda yake" Martin alimsikiliza pia baba yake na kuwaahidi wazazi waje kwamba hatawaangusha stori ziliendea mpaka walipofika uwanjani waliagana kwa mara ya mwisho kwa furaha huku mama yake akilengwalengwa na machozi kabla hajapanda ndege mama yake alimwambia , "Martin usisahau tuliyokuambia" Martin alisema sawa mama usijali kuhusu hilo, mfanyakazi wa kina martin alimkumbatia na kumnong'oneza, "Mdogo wangu kumbuka heshima ikizidi huleta dharau", Martin kwa mda huo hakujua lile neno liba uzito gani aliwapungia mkono na kupanda ndege na mda mchache kijana Martin alikwea p**a kuelekea pande za marekani, , , .....
Je Martin atafanikiwa kufika marekani?
Vipi kuhusu maisha yake akiwa katila nchi ya kigeni asipojulikana, , , usikose kufuatilia sehem inayofuata, na pia usisahau ku like, comment na kushare pia waalike marafiki zako wa like page yetu wa hadithi na simulizi