29/05/2024
MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA
Desemba 9 mwaka 1961 mambo makubwa mawili yalifanyika katika sehemu ya maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika,mosi ilikuwa ni kushusha bendera ya mkoloni na kupandisha bendera ya taifa huru na wakati huohuo na kupandisha mwenge wa uhuru katika kilele cha mlima Kilimanjaro tukio hili la kupandisha mwenge haikujulikana sana kwa maana yake hadi pale Baba wa taifa Mwalimu Julius kambarage nyerere alipozungumza mambo yafuatayo kuhusu tukio hilo "tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro umulike hata nje ya mipaka yetu ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini ,upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau" miaka 60 baada ya uhuru wa Tanganyika sasa ikifahamika zaidi kwa jina la Tanzania kutokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964.
Huko nyuma miaka michache kabla ya uhuru matukio ya namna hivi yalikuwa yakihusishwa na serikali ya kikoloni na wananchi walipigana kutaka uhuru wao. Watanzania wakati ule walipigana ili wapate haki ya kuchagua viongozi wao waliowataka kwa kuzungumzia matatizo yao kwa uwazi kutofungwa bila makosa au utu wao kutokutetwa kwa namna yoyote ile.
Katika mwaka wa kwanza wa uhuru wa Tanzania ilianza kujipambanua k**a taifa linaloamini katika umajumui wa Afrika Nyerere akielezwa muwa tayari kwa kusubiri Tanzania isiwe huru ili Jomo Kenyatta aachiwe huru kutoka jela Kenya na kuja kuwa raia wa shirikisho la Afrika mashariki na kushiriki katika harakati za kumkomboa mtu mweusi barani Afrika na kwingine duniani
Pia katika elimu Tanzania ilianza kufanya jitihada za makusudi za kusomesha watu wake kwa kuanzisha chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na vyuo vingine vya kistadi kiasi kwamba kufikia mwishoni kwa mwaka 1970 Tanzania ilikuwa ikitajwa kuwa mojawapo ya nchi zilizofuta ujinga kwa kiasi kikubwa duniani huku UDSM ikitajwa k**a mojawapo ya vitovu vya fikra za kimapinduzi barani Afrika
Pia Tanzania ilianzisha viwanda vingi vilivyotumia malighafi kutoka kwa wakulima na wazalishaji wengine watanzania na ingawa vipato vyao havikuwa vikubwa.
Kwahiyo katika kizazi cha kwanza cha watawala wa Tanzania kilifanikiwa kufanya jambo moja kubwa kuunganisha watu kutoka makabila,dini, mila na tamaduni tofauti na kutengeneza nchi ya watu wanaojiita watanzania lakini pia kwa kuangalia kuhusu vigezo k**a ujenzi wa barabara, ukuaji wa uchumi, upatikanaji wa huduma na bidhaa muhimu kwa maisha ya watu,tofauti ukilinganisha hali iliyokuwa miaka 60 iliyopita