08/05/2014
Wakati mwingine tunaangalia sana mapungufu ya wenzi wetu na yale ambayo wako tofauti nasi kiasi cha kushindwa kufurahia mazuri yao na tofauti zetu in a positive way. Muda wa kufurahiana na kujenga ndoa yenu mnajikuta mnautumia kukosoana na kulaumiana. Mume anaona mke hamheshimu anavyotaka maana analinganisha na ndoa fulani na mke anaona mume hampendi kikamilifu maana analinganisha na ndoa ya wazazi wake.
Hakuna jambo linaloboresha na kujenga ndoa k**a kuchukuliana. Jifunze kumchukulia mwenzio jinsi alivyo. Hapa sizungumzii kuchukuliana na dhambi, hapana. Dhambi haichukuliwi, inawekwa wazi, kutubiwa na kuachwa kabisa. Uasherati, uzinzi, kupiga, ukatili wa aina yoyote huo hauchukuliwi bali unatafuta msaada ili kuumaliza kabisa.!! Hapa nazungumzia kuchukuliana na uhalisia wa mtu alivyo. Yale ambayo unaona huwezi kuyachukulia yapeleke mbele za Mungu. Mungu pekee ndiye anayeweza kumbadili mwanadamu, mueleze yeye na uombe neema ya kuchukulina na mwenzi wako kwa furaha.
KOL. 3:12-14
"Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; k**a Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu."