04/06/2023
MAOMBI YA KUOMBEA NDOA NA FAMILIA.
Katika familia baba ndie kichwa cha nyumba K**a neno linavyosema katika efeso 5:33.
Katika andiko hilo la efeso neno limeoredhesha vipaumbele muhimu ambavyo ndoa inapaswa kuwa au baba au mama, navyo ni I): upendo ( ii) heshima ( iii ) umoja (iv) utawala (v) kumstahi ( kuwa na adabu.
👉🏻NAMNA YA KUOMBA.
Baba katika jina la Yesu Asante kwa uzima ulionipatia katika maisha yangu siku hii ya leo,baraka zako na wema wako katika maisha yangu, ninaomba ukanisamehe kwa makosa niliyokukosea na dhambi zangu ukanisamehe,ninaomba damu yako ya thamani ikanitakase na kunisafisha nafsi yangu na roho yangu, ninatubu kwa niaba ya mume/mke wangu ninaomba rehema juu yake ninaomba rehema juu ya ndoa yangu baba ukatusamehe familia yangu na watoto zangu tumekutenda dhambi.
1:Baba ninaomba roho ya upendo ikawale ndoa yangu, upendo ukawe ndani ya mume/mke na watoto, tukapande kwa jina la Yesu.
2:Baba ninaomba roho ya umoja Kati yangu na mume wangu/mke wangu na familia yangu
3:Baba ninaomba mamlaka ya utawala K**a kichwa cha familia kikatawale kwa mume wangu, na watoto, ndugu wakamuheshimu mume wangu.
4:Baba nipe Moto wa kumuheshimu mume wangu, niondolee madharau,kiburi,kujiinua na hasira za kijinga katika ndoa yangu.
5:Baba naomba roho ya adabu na hekima katika ndoa yangu ikatawale katika maisha yangu.
Sasa hapo ushaomba kuhusu tabia au mambo yanayochangia anguko katika maisha yako ya ndoa.
👉Sasa Kuna tabia au mambo yanayosababishwa na nguvu za Giza, husuda na vijicho katika maisha ya mtu, uchawi na uganga.
Mfano: mwanzo 11:6-11.
Kisa hichi kinaeleza kuwepo kwa watu wenye malengo sawa na nguvu sawa na umoja wa kufanya Jambo lao na kufanikiwa na walikaa pamoja, Kilichofanyika Mungu alishuka na kuwatawanya wote.
😭 Kwahiyo katika ndoa au mahusiano kumbe anaweza adui akaingia na kusambaratisha umoja na uhusiano wenu badala ya kuelewana mkawa hamuelewani wala kusikilizana.
👉🏻NAMNA YA KUOMBA.
1: Wewe adui ulieingia katika ndoa yangu ili kusambaratisha Ninakuharibu kwa jina la Yesu.
2:Ninaharibu Kila kazi za wachawi katika ndoa yangu, maana imeandikwa hakuna uchawi wala uganga juu yangu Mimi
3:Ninaharibu na kusambaratisha kila roho mlizihachilia kwangu zikishindwe kwa jina la Yesu, iwe mafarakano, kutoelewana, kusikilizana au uzinzi au uesherati.
4:Ninavunja na kusambaratisha kila vikao vyenu vya kichawi mlivyokaa kinyume nami vikashindwe kwa jina la Yesu
5:Ninahachilia amani,upendo,furaha, maelewano, kibari katika ndoa yangu.
6:Ninamleta pamoja mume wangu, mke wangu,mtoto wangu, watoto wangu katika ndoa yangu katika jina la Yesu.
7:Baba naomba neema yako ikatawale juu ya familia yangu, ukamlinde mume wangu,mtoto wangu,mke wangu kwa jina la Yesu.
8:Bariki watoto zangu, fungua fahamu zao mashuleni wanaposoma,wakawe vichwa na si mkia.
9:Bariki nyumba yangu, ondoa magonjwa, umaskini, fungua madirisha ya mbinguni na malango yetu yakawe wazi juu yetu kwa jina la Yesu.
Festo wilfred
5-06-2023