03/12/2022
Kuna muda unafika,unajiona kukata tamaa,unaona huwezi tena,unajivua thamani, mbele unaona giza,hujui nini ufanye,muda unakuendea kombo kiasi unaona ndo basi tena,unaowategemea ndo wameshakuangusha,unaowapenda hawapo tena unabaki kujilaani na kujiona wewe si mtu mwenye bahat bali mikosi,,,,,,
Nataka nikuambie kitu moja muhimu, katika nyakati hizi ndipo Mungu anakuhitaji sana,ndipo roho yako inataman sana kuwa karibu na Mungu na ndipo Mungu anatamani kujionyesha KATIKA maisha yako.
K**a ilivo kwa mtu anaekusaidia alivo na wivu anapoona juhudi zake zinaenda bure pale anapotoa msaada,na pengine huthamin kabsa mchango wake kwa sababu unazo options mbalimbali na huwezi kuona mchango wake,akaamua Kukaa pembeni na kuacha kujishughulisha na mambo yako ndivo ilivo kwa Mungu pia,, atasubir muda ambao umekata tamaa na umejaribu kila njia ukashindwa,ndipo atapochukua nafasi yake.
Uzuri wa Mungu wetu si k**a walivo binadamu akuwekei kinyongo,yeye ukimrudia na kuomba toba hupokea na kukumbatia, maana yeye ndiye baba wa huruma mwenye kugeuza ghadhabu na kuwa Rehema, mwenye kuyafanya yote yanayoshindikana kwetu wanadam.
Nakukumbusha tu bado hujachelewa mtafute Mungu ndio kimbilio,yupo na wala hajakusahau.