Mambo Yote

Mambo Yote A business directory which shows photographic location of buildings and their contact details, streets and many more.

Post job opportunities here for others who might be looking for opportunities to and qualify to work.
06/01/2026

Post job opportunities here for others who might be looking for opportunities to and qualify to work.

Banana benefits
14/02/2024

Banana benefits

14/02/2024
Sasa nitaeleza namna ya kujitafuta na kujipata kwa kutumia concept ya IkigaiIkigai ni nini?Neno hili la kijapani lina ma...
16/11/2023

Sasa nitaeleza namna ya kujitafuta na kujipata kwa kutumia concept ya Ikigai

Ikigai ni nini?
Neno hili la kijapani lina maana sababu ya kuishi kiswahili reason of being, kingereza raison d'etre kifaransa.
Ikigai ni vile vitu vinakupa mwelekeo wa maisha na kukupa hamasa ya kusonga mbele.

Tafiti zilifanyika huko Japan baada ya kuona watu kule wanaishi miaka miingi sana (zaidi ya 100) wakiwa na afya amani na furaha. Pamoja na mambo mengine ilionekana sababu kuuubwa sana ni "ikigai"
Hebu angalia maisha ya watu wa zamani hapa kwetu Tanzania halafu angalia maisha ya watu wanaoishi sasa tena zaidi wale wa.tabaka la kati walioajiriwa na waliojiajiri.
Umri wa kustaafu kwa Tanzania ni miaka 60 je, unaona nini kinatokea kwa wastaafu wengi? Kwa haraka haraka kuna mambo makubwa matatu hutokea.
1. Kupata maradhi ya kudumu yasiyoambukiza
2. Kufilisika hata baada ya kulipwa fedha nyingi
3. Kutokuwa na furaha
Kustaafu kumekuwa kwa kuogopesha mno kiasi wengine hawataki hata kustaafu wengine wanadanganya hata umri.

Lakini ni kweli tunatakiwa kustaafu? Je, ukistaafu kazi umestaafu maisha? Neno kustaafu ama retirement halipo kwa vocabulary za wenzetu wajapan kwa sababu hawastaafu yaani wanaendelea kutimiza wajibu wao hapa duniani. Wamejipanga. Wako active mpaka umri mrefu.

Tunawezaje kujitafuta na kujipata sasa.

Kwa kutumia mchoro hapo juu tutaweza kupata kujua kwanini tunaishi kwanini tumekuja duniani na nini sababu au wajibu wetu. Kitu kinachokufanya uamke asubuhi. Hapa naukumbuka sana msemo wa *_"mbeba maono hafi"_* tunauchukulia poa k**a vile kuna watu specific ndo wana kazi maalumu hapa duniani kumbe hata mimi na wewe ni watumwa, watumishi hapa duniani kila mmoja kwa nafasi yake.

Angalia mchoro kwa makini kisha anza kujaza majibu kwa kutumia huo muongozo hapo.

Tenga walau saa moja, tafuta mahali pa utulivu chukua peni na karatasi/notebook tafakari kwa kina upate majibu sahihi kwani wewe ndo unayeweza kumtafuta wewe na kumpata. Majibu yako waweza kushare na watu wako wa karibu wanaokufahamu na kukujua na walio tayari kusema ukweli wanaweza kukuongezea ila usije beba maoni ili uwaridhishe chukua kile kinacholeta maana kwako.

1.
Hapa ni kile kitu ukifanya unapata burdaani ndani yani amani kabisa na kuwa na nguvu, kukufanya uwe hai na mwenye furaha na raha. Mifano ni mingi yaweza kuwa kuogelea kukimbia kusoma kupiga stories na washkaji, kuabudu, kuandika nk. Usiangalie unachoweza bali unachopenda

2. /AMBACHO WEWE NI MKALINWAO
Hapa inajumuisha mambonyote ambayo wewe ni mzuri katika kuyafanya. Uwe umejifunza au ni hobbies tu au vipaji ulivyonavyo. Mfano kuchora, kupiga chombo fulani cha mziki, kuimba, public speaking upasuaji(madaktari) kupika kushauri nk.
Hapa angalia vile unavyoweza bila kuangalia passion wala malipo. Yani kitu unakiweza haswaaa

3.
Hapa dunia inajumuisha kujitoa kwako kwa jamii inayokuzunguka na ulimwengu wote. Hii yaweza kuwa kile unachokiona wewe au wengine wanakiona inawezekana dunia inahitaji madaktari wanawake, wataalamu wa IT yanahitajika maji safi na salama, chakula bora, mbegu bora mafunzo ya vijana nk.
Angalia sana kile kinachohitajika bila kuweka mahitaji yako mbele kwenye hili eneo

4. KWA KUKIFANYA
Nini unaweza kufanya ukapata maokoto. Angalia nyuma sasa k**a passion yako vipaji vyako ujuzi wako.je, nini unaweza kufanya na ukalipwa? Je, ni kuandika, kuongea, nini ulichonacho ni hot sokoni?

UKIMALIZA HILO ZOEZI UTAANGALIA KILE KILICHOTOKEA SEHEMU ZOTE NNE NDO IKIGAI YAKO

Yaani utaona ni kitu
Unapenda kufanya hata bure
Unaweza kufanya
Dunia/jamii inakihitaji
Ukifanya kinaweza kukulipa.

Ni zoezi rahisi halafu gumu ila lina maana kuubwa sana kwa maisha yetu. Tusizurulezurule tu tukaenda zetu muda ukiisha. Tufanye vitu vya kutufurahisha na kuwanufaisha wengine lakini vinatuingizia maokoto.

[Mambo muhimu5 ya kuzingatia

1. Anza taratibu, focus kwenye mambo muhimu
2. Jitambue wewe mwenyewe na kujikubali
3. Tafuta amani na mwendelezo. Shiriki/shirikisha na watu wengine
4. Furahia mambo madogomadogo uliyonayo uyakuzeIshi sasa sio kesho

    AND  Leo naomba tujifunze mambo matatu yanayoendana ila ni muhimu mnooo tena sana kwa maisha ya mwanadamu maana bila...
16/11/2023

AND

Leo naomba tujifunze mambo matatu yanayoendana ila ni muhimu mnooo tena sana kwa maisha ya mwanadamu maana bila kuyajua utaishia tuu kuzurula hapa duniani kisha uende zako.

Purpose ni kusudi
Calling ni wito
Assignment ni kazi maalum

Kila mwanadamu hapa duniani ana kusudi lake la kuishi. Usipojua kusudi lako utashangaa biashara ndoa mahusiano yani maisha yanavurugu kwelikweli na utasindikiza tu wengine kwenye makusudio yao. Wale wanaojua kusudi inakuwa rahisi sana hata k**a biashara anahama viwango kwa viwango. K**a ni kazini matunda yanaonekana k**a ni mahusiano mengine yanashamiri lakini kuubwa kuliko yote huishi maisha ya furaha na amani na mafanikio makubwa (tafsiri ya mafanikio hapa sio pesa).
Je, kuna tofauti kati ya hivyo vitatu?
Kusudi la mtu huwa halibadiliki kwenye maisha.
Calling inaweza kubadilika
Assignment ndo hubadilika kila uchwao.

Twende kwa mfano huu....
Mfano kusudi lako wewe hapa duniani ni kuwa muuguzi/nurse Wito wako unaweza kuwa kuhudumia wazee, wazazi watoto au walemavu nk. Lakini assignments zaweza kubadilika. Unaweza kutumwa/kuitwa sehemu fulani labda hospitali ama mkoa fulani kwa wakati fulani then Mungu akaona uhitaji wa vile vipaji alivyoweka ndani yako vinahitajika shuleni au mtaani ama akakupa mtu/watu specific udeal naye. Na unaweza kuwa na assignments zaidi ya moja kwa wakati mmoja.
Sasa wawezaje kujua kusudi lako wito ama kazi maalumu?

_Tutaendelea....._

WATU NA VIATU..... Kwenye maisha lazima kuna watu watu wako na watu viatu. Unapopata watu ambao wanakukimbilia ukiwa na ...
26/10/2023

WATU NA VIATU.....
Kwenye maisha lazima kuna watu watu wako na watu viatu. Unapopata watu ambao wanakukimbilia ukiwa na shida. Wanakukumbatia ukiwa na jambo lako. Wanakwambia ukweli ukikosea wanajua kuficha aibu yako. Hao ni watu wako. Wakumbatie waheshimu lakini kamwe usisahau wema wao kwa makosa au kosa walowahi kukufanyia. Usifute mema 800 kwa kosa moja. Waombee wasamehe wapende sana. Hata k**a umepata funzo la kukaa nao mbali kwa makosa yao *usisahau wema wao wa dhati*

Tafadhali follow .international kwa nondo za mahusiano malezi na mengine mengi.
26/08/2023

Tafadhali follow .international kwa nondo za mahusiano malezi na mengine mengi.






We design it all
25/08/2023

We design it all

Address

Dar Es Salaam
BOX71831

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mambo Yote posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share