15/06/2026
*V-K9s Dog Training Tz*
Leo tunakuletea somo la aina za mbwa
*makundi makuu 7* kulingana na kazi wanayofanya au walizofundishwa kufanya.
1. *Kundi la Mifugo ya Kazi / Working Group*
Hawa ni mbwa wa nguvu, wenye akili, na ustahimilivu. Walifugwa kulinda, kuvuta mizigo, kuokoa watu.
*Mifano*: German Shepherd, Rottweiler, Doberman, Siberian Husky, Saint Bernard
*Uwezo*: Ulinzi, uokoaji, kuvuta sled, ulinzi wa nyumba. Wanahitaji mazoezi mengi.
2. *Kundi la Kuwinda kwa Harufu / Hound Group*
Wanafugwa ili kufuatilia mawindo kwa kutumia pua zao.
*Mifano*: Bloodhound, Beagle, Greyhound, Dachshund
*Uwezo*: Kunusa umbali mrefu, kukimbia kasi sana. Bloodhound anaweza kufuatilia harufu ya siku 2-3 zilizopita.
3. *Kundi la Kuwinda kwa Macho / Sporting Group*
Wanasaidia wawindaji kuchota ndege majini na nyikani.
*Mifano*: Labrador Retriever, Golden Retriever, Cocker Spaniel, Pointer
*Uwezo*: Kuogelea vizuri, kuchota/kubeba vitu bila kuviharibu, utii mkubwa. Ndio maana Labrador ni mbwa wa wanatumika kuongoza vipofu.
4. *Kundi la Kufuga Mifugo / Herding Group*
Wanafugwa ili kudhibiti na kuongoza ng'ombe, mbuzi, kondoo.
*Mifano*: Border Collie, Australian Shepherd, Belgian Malinois
*Uwezo*: Akili kali sana, wepesi, utii. Border Collie anachukuliwa kuwa mbwa mwenye akili zaidi duniani. Anaweza kujifunza amri 200+.
5. *Kundi la Mbwa Wadogo / Toy Group*
Hawa ni wa kuburudisha na kuwa marafiki wa nyumbani.
*Mifano*: Chihuahua, Pomeranian, Shih Tzu, Maltese
*Uwezo*: Hawana nguvu kubwa, lakini ni wabunifu wa kuhisi hisia za mwenyeji, rahisi kubeba, nzuri kwa watu wanaoishi ghorofani.
6. *Kundi la Terrier*
Wanafugwa ili kuwinda panya na wanyama wadogo ardhini.
*Mifano*: Jack Russell, Bull Terrier, Yorkshire Terrier
*Uwezo*: Ujasiri mkubwa kuliko ukubwa wao, mkaidi, mwenye nguvu kwenye nguvu ya kutafuna na kuchimba.
7. *Kundi la Mbwa Wasio wa Kazi Maalum / Non-Sporting Group*
Hawa ni mchanganyiko. Walifugwa kwa kazi mbalimbali.
*Mifano*: Bulldog,