Rudisha Tabasamu Kwa Afya Bora

Rudisha Tabasamu Kwa Afya Bora Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Rudisha Tabasamu Kwa Afya Bora, Business service, Moshi, Dar es Salam.

Learn to enjoy every minute of your life. ...
13/05/2018

Learn to enjoy every minute of your life. ...

UMUHIMU WA MAJI KATIKA MWILIMaji huunda zaidi ya theluthi mbili ya miili yetu, lakini wengi wetu huacha kunywa maji na k...
28/02/2018

UMUHIMU WA MAJI KATIKA MWILI
Maji huunda zaidi ya theluthi mbili ya miili yetu, lakini wengi wetu huacha kunywa maji na kunywa vinywaji vingine wakisahau kunywa maji ya kutosha.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwili wa mwanadamu umejengwa kwa asilimia kati ya 55 na 75 za maji na watu wembamba wana kiasi kikubwa cha maji mwilini kuliko wanene. Kwa sehemu kubwa tumetokana na maji, hii ni sababu zaidi ya asilimia 94 ya damu yetu ni maji, zaidi ya asilimia 85 ya ubongo wetu ni maji.

Asilimia 60 ya uzito wako ni maji na mifumo ya mwili wako hutegemea maji ili kufanya kazi zake kwa ufanisi. Unapoanza kuhisi kiu, mwili unakuwa umepungukiwa na maji. Hata katika upungufu mdogo wa maji mwilini, asilimia moja hadi mbili ya uzito wa mwili hupungua, suala hilo humfanya mtu akose nguvu na ajisikie amechoka.

Upungufu sugu wa maji mwilini (chronic dehydration) ndio chanzo cha magonjwa mengi kwa mwili wa binadamu ambayo kisababishi chake kilikuwa hakijulikani.

Kwa asili, upungufu sugu wa maji mwilini unamaanisha upungufu wa kudumu wa maji ambao umedumu kwa muda fulani. K**a ilivyo kwa maradhi ya upungufu wa kiini lishe fulani, mfano upungufu wa vitamini C kwa ugonjwa wa kiseyeye (scurvy), upungufu wa vitamini B kwa ugonjwa wa beriberi ama upungufu wa madini ya chuma kwa ugonjwa wa anemia, upungufu wa vitamini D kwa ugonjwa wa matege/nyongea na mengine unayoyafahamu; namna mahususi ya kutibu magonjwa hayo ni kurudishia kiasi kilichopungua. Kwa mujibu huu, ikiwa tutaanza kutambua mkanganyiko wa kiafya uletwao na upungufu wa maji, uzuiwaji wake na hata udhibiti wake wa mwanzo utakuwa ni rahisi.

Mwili unahitaji kwa kiasi kikubwa maji ili kufanya kazi zake vema. Kwa mfano, mapafu yako yanahitaji vikombe viwili vya maji hadi vinne kila siku ili kufanikisha kazi yake ya upumuaji kwa ufanisi. Na kiasi hicho huhitajika zaidi wakati wa baridi. Kunywa glasi nane za maji au robo lita kila siku ndio kiwango ambacho kipo akilini mwa wengi, wote wakiwa na imani kwamba ndicho kiwango kinachokubalika kiafya, si kweli!

Mahitaji ya maji yanatofautiana kati ya mtu na mtu. Mambo k**a jinsia, hali ya hewa, kiwango cha joto la mwili, ushiriki wa mazoezi, aina ya kazi, umri na aina ya mlo unaokula kulingana na kundi lako la damu ni mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa.

Ukweli ni kwamba kiwango cha maji ambacho unachopaswa kunywa kinatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine.
Mwenye uzito wa kilogramu 45 mpaka 49 anahitaji kunywa lita 1.9 hadi 2.0, mwenye uzito wa kilogramu 50 hadi 54 anahitaji kunywa lita 2.1 hadi 2.2, hali kadhalika kilogramu 55- 59 kwa lita 2.3 hadi 2.4 na kuendelea.

Maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa mawili mpaka mawili na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri.

Ikiwa inakulazimu kukojoa chini ya muda wa masaa mawili tangu unywe maji, pamoja na hatua nyingine muhimu tofauti utalazimika:
• Kuacha kunywa maji matupu, jaribu kunywa juisi (uliyotengeneza mwenyewe) ya chungwa, juisi ya matunda mchanganyiko, ya zabibu au juisi nyingine yeyote kulingana na kundi lako la damu na hali ya mwili wako, isipokuwa kwa watu wanaosumbuliwa na pumu (asthma) ambao hawatakiwi kunywa juisi ya chungwa. Wakati huo huo muhimu kukumbuka kuongeza robo tatu gramu za chumvi katika kila nusu lita ya juisi yako.

• Kuhakikisha unakunywa maji kwa mujibu wa kipimo chako kulingana na uzito wako. kunywa maji mengi zaidi ya kiwango chako husababisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla hayajatumiwa na mwili.

• Achana kwanza na matumizi ya kinywaji chochote cha kutengenezwa kiwandani, acha chai ya rangi na kahawa. vinywaji hivi ni mawakala vikojoshi (diuretics), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla mwili haujayatumia. utarudi kunywa chochote ikiwa utavihitaji tena vinywaji hivyo mara utakapokuwa sawa kwa mara nyingine tena kiafya. Acha pia uvutaji wa sigara na au pombe.

Maji yana faida nyingi katika mwili ikiwa ni pamoja na kusaidia umeng’enyaji wa chakula, huboresha hali ya viungo na misuli, maji yanaweka ubongo katika hali nzuri zaidi ya ufanisi zaidi hivyo kunywa maji ya kutosha kunamuwezesha mtu kufikiria vyema zaidi, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa k**a mafua na kusaidia kupona haraka ugonjwa huo, mawe ya figo, matatizo ya ini, baadhi ya saratani na magonjwa mengine.

Ikiwa unataka kupunguza unene na uzito, pamoja na taratibu maalum, sahihi na salama, maji pia huchochea kukusaidia kwa kiasi kikubwa kwa kuwa huongeza kasi ya shughuli za kimetaboliki na kufanya mwili kutumia nishati nyingi zaidi, hivyo kupunguza kiasi cha nishati kitakachohifadhiwa mwilini katika hali ya mafuta hivyo kuchangia kupunguza unene na uzito kiujumla.

Nguvu zetu hazitokani na vyakula tunavyokula, bali zinatoka katika maji ambayo yanaiweka atomu ya haidrojeni katika chakula.

Vyakula tulavyo hutupatia vitamini na madini tunayoyahitaji ili kubaki katika afya. Ikiwa mwili haupati maji halisi (glasi 1 au 2) kabla ya kula chakula na kusubiri (robo saa au nusu saa), basi mwili lazima ujikope maji wenyewe.

K**a mwili utakopa maji toka katika damu, basi ateri lazima zipunguze vipenyo vyake na moyo lazima utumie nguvu nyingi ili kusukuma damu ambayo ni nene (nyingi), kitendo hiki tunakiita 'shinikizo la damu' (BP).

Ikiwa mwili utajikopa maji toka katika ubongo, utapatwa na 'kichwa kizito' au kichwa kuuma ambacho kinaweza pelekea maumivu ya kichwa.

Ikiwa unakunywa pombe na inavuta maji toka kwenye ubongo, utapatwa na kutokujisikia vizuri au uchovu (hangover).

Kokote katika ogani au tishu mwili utakakokopa maji, lazima ogani au tishu hiyo iachiwe madhara na hivyo kusababisha maumivu ama ufanyaji kazi wa ogani au tishu hiyo usio wa kawaida .

Kila tunapopumua hewa nje (exhale) tunapoteza maji. Ikiwa utahema juu ya kioo, utauona ukungu (maji). Tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumua tu kila baada ya masaa 24!
K**a mwili utakopa maji toka mapafuni, utapatwa na pumzi fupi itakayopelekea upatwe na pumu (asthma) na matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa upumuaji.

Mapafu na moyo vinauhusiano wa karibu, kwa hiyo k**a mwili utakopa baadhi ya maji toka katika mishipa ya moyo, utapatwa na maumivu ya moyo ambayo yanaweza kurahisisha kutokea kwa shambulio la moyo (heart-attack).

Mishipa inahitaji damu na maji wakati unafanya mazoezi, kwa hiyo k**a unatakiwa kula chakula na kisha kutembea au kupandisha ngazi (za ghorofa) na una upungufu wa maji (dehydrated), unaweza ukapatwa na pumzi fupi, shambulio la pumu, utapatwa na maumivu ya moyo (angina) au kukak**aa kwa mishipa (cramps).

Ndiyo maana tumekuwa tukisikia, kamwe usiende kuogelea mara tu baada ya kumaliza kula kwa sababu mishipa itakak**aa. Mwili unapokuwa katika kazi yake ya umeng'enyaji chakula, huielekeza (diverts) damu toka katika mikono na miguu kwenda katika utumbo mdogo ili kusaidia umeng'enyaji wa chakula. Baadhi ya vyakula ni rahisi kumeng'enywa na huwezeshwa na maji pekee, k**a vile matunda na mboga za majani.

Vinywaji vingine (liquid beverages) k**a vile kahawa, chai, soda , pombe na juisi, si maji kwa mwili. Hivi ni vyakula pia kwa sababu ulimi unaipata ladha ya viongezi (additives) na sio ladha ya maji halisi, na hivyo mwili utakishughulikia kinywaji hicho k**a chakula.

Utafaidika na baadhi ya maji k**a vile katika matunda na mboga za majani kwa masharti ya kinywaji hicho kutokuwa na kafeina (caffeine). Kafeina ni kikojoshi (diuretic), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili.

Kunywa maji masaa 2 hadi 2 na nusu baada ya chakula kunasaidia kumalizia umeng'enyaji wa chakula na kuunywesha mwili maji baada ya kukaukiwa kulikosababishwa na kazi ya umeng'enyaji wa chakula.

Njia bora ya kuupa mwili maji ya kutosha ni kutii kiu chako kila unaposikia kiu inabidi unywe maji ya kutosha. Njia nyingine ni kuchunguza mkojo wako kwa makini kuanzia rangi na harufu yake, ikiwa una rangi nzito na harufu kali hii ina maana mwili hauna maji ya kutosha.

Kwa wale wanaofanya mazoezi, watu wengi hupoteza kati ya lita moja na mbili za jasho kila saa moja la mazoezi ya kawaida. Hivyo mtu anapaswa kurudishia maji yaliyopotea kupitia jasho ingawa kuhisi kiu bado ndio mwongozo wa moja kwa moja wa kunywa maji.

Ripoti ya makubaliano iliyochapishwa na British Journal of Sports Medicine, ilidai wanamichezo wengi wako katika hatari ya kupatwa na ‘Hiponatremia’ (upungufu wa chumvi ya natri katika damu) inayotokana na michezo tatizo linaloweza sababisha mtu kunywa maji mengi hivyo anaweza kusababisha kichefuchefu, kutapika, kuumwa kichwa, uchovu na wakati mwingine huweza kusababisha matatizo makubwa k**a kupoteza fahamu na hata kifo.

Ili kujilinda na kupungukiwa au kutozidisha kiwango cha maji, ni vyema kuusikiliza mwili wako unachotaka. Kunywa maji safi na salama kwa kiasi kinachostahili kiafya kunaweza kuboresha maisha na kuimarisha afya.
Tunaweza kufupisha hapa kuwa, kutokana na mazoea yetu ya kusubiri kiu au mdomo ukauke ndipo tunywe maji, huwa tunaulazimisha mwili kuishi katika mfumo wa mgawo wa maji na hatimaye usambazwaji wake, mfumo huo ndio huleta hatari mwilini kwa kuzalisha ishara mbalimbali za magonjwa ambayo dawa yake pekee ni kubadilika kwetu na kuanza kunywa maji kabla ya kusikia kiu na kujifunza umuhimu wa maji kwa maisha marefu bila magonjwa.

Kuna maajabu zaidi ya milioni katika glasi moja ya maji kuliko dawa yoyote utakayotumia.

ANGALIZO:
• Ili kuhakikisha figo zako zinafanya kazi vizuri, ni lazima kiasi cha maji unachokunywa kiwe karibu sawa na kile unachotoa.
• Wakati huo huo, kwenda chooni mara nyingi kwa siku kunaweza kukusababishia kupoteza vitamini muhimu, madini na elektrolaiti na kukufanya vibaya zaidi ya vizuri.
• Unatakiwa kuwa makini sana unapoanza kuongeza uchukuaji wa maji mwilini, anza pole pole kwa kuongeza glasi 1 kila siku mpaka utakapofikia kiwango cha maji unayohitajika kunywa. Lazima uupe mwili muda wa kujirekebisha badala ya kuzoea vinywaji k**a kahawa, chai na soda, kwa kuwa vinywaji hivi huufanya mwili kujiendesha kwa namna nyingine tofauti na inavyopaswa.
• Unaweza kuumwa na kichwa au unaweza usijisikie vizuri tu siku tatu mpaka wiki moja za kuanza kujizoeza kunywa maji kiwango unachotakiwa, usiache kunywa maji kwa kuwa hayo si madhara bali ni dalili kuwa taka na baadhi ya sumu ambazo zimelundikana ndani ya mwili wako katika mifumo tofauti zimeanza kuvunjwavunjwa mwilini. Zoezi ambalo huhitaji msaada zaidi sambamba na matumizi ya maji katika kufanikisha zoezi hili.

VIDONDA VYA TUMBO, MARADHI HATARI KWA AFYA YA MFUMO WA CHAKULA.Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula katika mwili unaohusika na...
25/02/2018

VIDONDA VYA TUMBO, MARADHI HATARI KWA AFYA YA MFUMO WA CHAKULA.

Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula katika mwili unaohusika na umeng’enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili ili kuuwezesha kufanya kazi mbalimbali.

Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng’enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika k**a ‘Peptic Ulcers’.

Vidonda vya mfumo wa umeng’enyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo ‘Gastric Ulcer’, vikiwa katika duodenamu tunaita ‘Duodenal Ulcer’ na vikiwa katika esofagasi tunaita ‘Esophageal Ulcer’.

Kisababishi kikuu cha vidonda vya tumbo ni bakteria aina ya ‘helicobacter pylori’ kupitia vyakula na maji. Pia, hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo k**a wapenzi wanaonyonyana ndimi.

Bakteria hao huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng’enya viitwayo ‘urease’ inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.

Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
Sababu nyingine ni chembe za urithi (genetics). Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu na wenye vidonda pia. Hii hupelekea kudhania kuwa chembe za urithi zinahusika pia.

Uvutaji sigara na tumbaku. Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta. Matumizi ya pombe/vilevi. Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo.
Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Ieleweke ni mara chache mtu kuugua vidonda vya tumbo na kutoonyesha dalili. Zifuatazo ni dalili zinazotokea kwa wagojwa wengi; maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda. Maumivu yanaweza kuanzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua. Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia, yanaweza kuwa makali wakati wa usiku yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.

Dalili nyingine ni kushindwa kumeza vizuri chakula au kukwama k**a kinataka kurudi mdomoni, kujisikia vibaya baada ya kula, kupungua uzito, kukosa hamu ya kula.

Dalili hatari ni pamoja na kutapika damu, kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito na kupata kichefuchefu na kutapika.

NAMNA YA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO.
Mambo yafuatayo yatakusaidia kuishi vizuri ukiwa na vidonda vya tumbo; Kwa kuzingatia kundi lako la damu vizuri kufahamu vyakula vipi ni sahihi kwako pamoja na vidonda vya tumbo ulivyonavyo. Mfano halisi ni kunywa maziwa na vitu vitokanavyo na maziwa k**a maziwa mgando na jibini kwa mtu wa kundi la damu ‘O’.

Kwa mtu wa kundi hili la damu ‘O’ maziwa hufunika utumbo na kupunguza athari za asidi ya tumboni.

Jitahidi kupunguza uzito hasa ikiwa uzito umezidi na hauendani na kimo chako.

Kula chakula sahihi kulingana na kundi lako la damu angalau kidogo mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza athari za asidi inayotengenezwa na tumbo.

Epuka matumizi ya vileo vya aina yoyote, kwa maana unywaji wa pombe mara kwa mara hutonesha kwenye vidonda vya tumbo vinavyotaka kupona.

Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.

Acha kuvuta sigara, tumbaku, na bangi. Uvutaji wa sigara utakuweka kwenye hatari zaidi ya kuanza vidonda vipya na kuzuia vidonda vingine visipone.

“Nakumbuka ugonjwa huu ulinianza Oktoba mwaka juzi, ulianza kwa tumbo kuunguruma pia nilipoteza hamu ya kula hali iliyonifanya niende katika zahanati ya kijijini kwetu, wao walinieleza kwamba nina vidonda vya tumbo walinipa dawa nikapata nafuu kidogo lakini baada ya muda hali ilibadilika na kuwa mbaya.
“Ikatokea kwa siku kumi na saba sikwenda haja kubwa, tumbo lilivimba kiasi cha kutaka kupasuka, nikaenda Hospitali ya Mount Meru, Arusha, nilifanyiwa vipimo kikiwemo cha x-ray, wakagundua kuwa sehemu ya haja kubwa kumeziba ikabidi wanifanyie upasuaji, pia walitoboa tumbo nikawa najisaidia kwa kutumia mpira.
“Baada ya siku mbili tangu nifanyiwe upasuaji huo, kibofu cha mkojo kikawa kinauma baada ya mrija kuziba, nilifanyiwa upasuaji nikawa najisaidia kwa kutumia mpira baada ya tumbo kutobolewa tena, huu mfuko wa kulia ni wa haja ndogo na wa kushoto ni wa haja kubwa.

“Nikiwa bado nipo Mount Meru madaktari walikata kipande cha nyama pajani na kukipeleka hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa vipimo na majibu yalipokuja iligundulika kuwa nina saratani ya utumbo mpana”. Hayo yakiwa ni maelezo ya mmoja wa wahanga walioathirika na vidonda vya tumbo na kupelekea madhara zaidi kwa afya yake.

Ni muhimu zaidi kudhibiti maradhi haya ya vidonda vya tumbo kwa kuepuka madhara mabaya na hatari zaidi kadiri tatizo linavyoendelea kuathiri mifumo mingine husika hasa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Madhara haya hatari ni k**a saratani ya tumbo na utumbo na kadhalika k**a tulivyoona.

Wasiliana nasi kupitia namba

0755273087

kwa maelezo na msaada zaidi au comment namba yako

Address

Moshi
Dar Es Salam

Telephone

0755273087

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Rudisha Tabasamu Kwa Afya Bora posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Rudisha Tabasamu Kwa Afya Bora:

Share