25/04/2024
MKE AU MUME WAKO MTARAJIWA ANA NAFASI KUBWA SANA YA WEWE KUFANIKIWA AU KUTOFANIKIWA KWENYE HATIMA YAKO YA MAISHA ULIYOPANGIWA NA MUNGU.
Mwanzo 2:18
“BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
Kwa mujibu wa neno la Mungu mke/ mume wako mtarajiwa ni msaidizi wa hatima yako ya maisha uliyopangiwa na Mungu(your destiny helper). So unapotazamia suala la ndoa ( kuoa/ kuolewa) litazame kwa jicho la hatima uliyopangiwa na Mungu maana Mungu hukuandalia mke/ mume anayetakiwa kusapoti kusudi la kuumbwa kwako (hatima yako ya maisha aliyokupangia).
Mtu ambaye unafunga naye ndoa ni kielelezo cha hekima yako. Mwenzi wako ni picha ya hatima yako uliyopangiwa na Mungu. Mke/ mume sahihi huja katika maisha yako ili kukufanya kuzingatia kazi yako uliyoitiwa na Mungu hapa duniani ( kusudi la kuumbwa kwako).
Ndoa sahihi inaongeza kiwango chako cha kufanikiwa kwenye hatima yako ya maisha uliyopangiwa na Mungu wakati mke/ mume asiye sahihi ataongeza kiwango chako cha kushindwa kuifikia hatima yako ya maisha.
Unapokuwa na mwenzi ( mke/ mume) sahihi, anakuwa tishio kwa wapinzani wako na kukupa nguvu ya kutekeleza kusudi lako/ hatima yako ya maisha kwa ubora. Moyo wa mfalme Sulemani uligeuzwa kutoka kwa Mungu kwenda kwa miungu mingine kwa sababu ya uhusiano mbaya/ wenzi wasio sahihi ( wake ambao walikuwa wakiabudu miungu ya kigeni).
N.B Relax, don't panic linapokuja suala la kuoa/ kuolewa Mungu ndiye anayemjua msaidizi wako wa kufanana na wewe/ anayeendana na kusudi la kuumbwa kwako ( hatima yako ya maisha uliyopangiwa na Mungu). Pia Mungu ndiye anayejua majira yako sahihi ya wewe kuoa/ kuolewa so kwa mujibu wa Mhubiri 3:1,11 GOD’S TIME IS THE BEST. Usilazimishe majira uliyoyapanga wewe nakuhakikishia utachanganyikiwa sana tu na kupoteza focus ya maisha yako.
Weka pembeni tamaa ya macho, mihemko ya mwili, tamaa ya pesa na mali, pressure ya umri, maneno ya watu n.k linapokuja suala la kutaka kuoa/ kuolewa.
Ukiona majira yako ya kuolewa/ kuoa yamefika unachotakiwa ni kusimamia Yeremia 29:11 kwa kumwambia Mungu, wewe ndiye unayemjua mume/ mke wangu sahihi uliyenipangia maishani mwangu anayeendana na hatima yangu ya maisha uliyonipangia. Hivyo Baba yangu kwa huruma zako nakusihi nijulishe aliye wangu sawasawa na Isaya 45:11 inavyosema.
N.B Ikiwa bado hujaoa/ hujaolewa yakupasa kulikabidhi lango lako la ndoa kwa Mungu/ kuliweka wakfu madhabahuni pa Mungu kwa sadaka ili shetani asipate mpenyo/ nafasi ya kukuletea mke/ mume asiye sahihi maishani mwako maana shetani anapotaka kuharibu hatima yako ya maisha uliyopangiwa na Mungu anakuletea mke/ mume asiye sahihi kwako ambaye atakuwa ni kikwazo kwako cha wewe kushindwa kuitimiza hatima yako ya maisha aliyokupangia Mungu.
Msisitizo wa ujumbe huu uende zaidi kwa wadada ambao ndio huonekana kuchanganyikiwa sana linapokuja suala la kuolewa. Relax my sister you are valuable than gold, Boaz wako yupo anakusubiri so usijichukulie poa na kujirahisisha.
By Mwl. Upendo Staford ( Teacher of Divine Destiny).
Facebook: Hon. Upendo Staford
Instagram:hon.upendostafors