24/09/2022
KUNGURU WA ZANZIBAR.
Muhenga ulishawahi kusikia kuhusu kunguru wa Zanzibar na ukawa unajiuliza wapoje au wana nini cha ajabu?
Kunguru wa Zanzibar ni hao unaowaona mtaani kwako wakirukaruka na kupozi kwenye nyaya za umeme na kusababisha shoti muda mwingine kwa kupigana kwenye nyanya baada ya kushikana ugoni 😂😂😂 (joking).
Kunguru hawa waliletwa na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wakisafirishwa kutokea Bombay nchini India mwaka 1891. Lengo ikiwa ni kudhibiti uchafu na takataka zinazoweza kuliwa na ndege hao kwenye viunga vya mji wa stone town na kwingineko kwenye manispaa za mji wa Zanzibar lakini baadae wakasambaa kwenye miji mbalimbali Tanzania bara k**a Dar es salaam, Morogoro, Pwani, Lindi na sasa ni almost Tanzania nzima.
Ukiacha kunguru wa Zanzibar kuna kunguru ambao walikuwepo jijini Dar, hawa walikuwa na rangi nyeusi na nyeupe ila ujio wa kunguru wa Zanzibar ukawafukuza kunguru hawa.
Kunguru weusi au kunguru wa Zanzibar hakika ni wasafishaji wazuri wa uchafu na mizoga kuliko hawa wenye rangi mbili ambao kwa lugha ya sasa unaweza kuwaita "wakishua" wenyewe hawataki kero wala stress. Ila ubaya wao kunguru weusi hawakuishia kusafisha mazingira tu mitaani bali walipita mpaka majumbani na madukani wakipita na vitu k**a mikufu, kofia, pochi, kupora vifaranga vya kuku, kuharibu viota vya ndege hata kudokoa mboga jikoni. Nk. Tabia ambazo kunguru wenye rangi mbili hawakuwa nazo kabisa.