UNI_Updates.tz

UNI_Updates.tz Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from UNI_Updates.tz, Business Center, Dodoma.

To you all UNI_updates.tz members.... we love you and we serve with smile
13/02/2023

To you all UNI_updates.tz members.... we love you and we serve with smile

Wanafunzi  wa mwaka wa kwanza na wa pili wanaosoma taaluma ya uandishi wa habari na mahusiano ya jamii(BAJP) katika chuo...
12/02/2023

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili wanaosoma taaluma ya uandishi wa habari na mahusiano ya jamii(BAJP) katika chuo kikuu Cha Dodoma,wametembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo kilometa kadhaa kutoka chuoni kwao Kwa lengo la kufanya matendo ya huruma hospitalini hapo ikiwa ni SUPRA CHARITY SEASON 1.

Ikiwa ni siku hiyo ya tarehe 11 February 2023, mhadhiri msaidizi wa chuo hicho Ndg. Mary Kafyome aliyeambatana na vijana hao ameeleza kuwa tukio Hilo lililenga kuwaandaa vijana hao kuwa maafisa uhusiano Bora hapo baadae.

Mbali na kutoa vitu mbalimbali Kwa wagonjwa vya kuwasaidia,tukio lingine la msingi zaidi walilofanya hospitalini hapo ni kutoa damu ili kuokoa maisha ya watu wengine. Mkuu wa kitengo cha DAMU SALAMA Ndg. Kocy Kibaja amewashukuru Sana vijana hao na kuomba watu wengine pia waige mfano huo ili kuokoa maisha ya mamia ya watu wanaopoteza maisha Kwa kukosea damu.


_udom255

PR EXCELLENCE  AWARDS ni mashindano ya kumpata afisa uhusiano. Je umepiga Kura kumpendekeza Public relations officer (PR...
12/02/2023

PR EXCELLENCE AWARDS ni mashindano ya kumpata afisa uhusiano. Je umepiga Kura kumpendekeza Public relations officer (PRO) Bora atakaeye wania tuzo hii.

Usikose, tarehe 18 February,2023 pale JNICC Dar es salaam Ambapo tuzo hizo za umahili zitatolewa . Fatilia ujue k**a afisa uhusiano uliyemchagua atawania tuzo hii.





"Ni lengo letu kuwa UDOM iwe salama kwa wote ili kila unapokutana na mwenye uhitaji wa kujifunza, basi unamshauri kuja h...
11/02/2023

"Ni lengo letu kuwa UDOM iwe salama kwa wote ili kila unapokutana na mwenye uhitaji wa kujifunza, basi unamshauri kuja hapa kwetu kupata elimu bora. Na ile tufike ni muhimu kutambua kuwa kabla ya kuona chochote kwa mtu mwingine,ona kwanza kuwa yeye ni binadamu k**a yeye na mpe heshima anayostahili, si kwa namna alivyo bali kwa sababu tu yeye ni binadamu k**a wewe. Niwasihi sote tushiriki katika kupinga vitendo hivi kwa kuvunja ukimya bila kujali nani anafanya vitendo hivi vibaya" alisema Prof. Lokina.
Kwa kushirikiana na UNESCO,chuo kikuu Cha Dodoma Kimefanya kongamano mahususi lililofanyika hivi leo Kwa lengo la kupinga ukatili wa kijinsia hasa vyuoni. Akifungua Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu inayosema" MAZINGIRA SALAMA! TOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA VYUONI", prof. Razak Lokina- Naibu Makamu mkuu wa chuo,taaluma,utafiti na ushauri,ame alilishukuru Shirika la UNESCO Kwa kuungana na chuo kikuu Cha Dodoma kupinga ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha haki na usawa vinatawala.
Kadhalika,mratibu wa mradi wa UNESCO wa 03 PLUS Kwa upande wa Dodoma Bw. Faraja Msangi aliishukuru menejimenti ya chuo kwa kujidhatiti kuhakikisha ukatili wa kijinsia unapigwa Vita na kutoa elimu ili kudumisha haki na usawa.

Droo ya mtanange mkali wa vuta nikuvute huku Chriss Marcelle,Robert na  Bille bingwa wa yanga fans wakibahatika kuona ny...
11/02/2023

Droo ya mtanange mkali wa vuta nikuvute huku Chriss Marcelle,Robert na Bille bingwa wa yanga fans wakibahatika kuona nyavu ya wapinzani wenzao wa simba fans na Sam Magesa, Edwin Mbiza na Shaibu Matipa hawakuwa mbali kujibu mapigo ya derby hiyo wote wakiibuka na mabao manne kwa manne katika mechi ya kufunga semista leo tarehe 11/2/2023 iliyoandaliwa na wizara ya michezo na burudani chini ya Waziri wa michezo, Twalibu Zungo na Naibu Waziri,Godfrey Assenga wa serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar-es-Salaam (Daruso mlimani)

Akiwa ikulu ya DODOMA (Chamwino), Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezungumza na vion...
11/02/2023

Akiwa ikulu ya DODOMA (Chamwino), Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezungumza na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya juu(TAHLISO) na Shirika la vyuo vikuu na taasisi ya Elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE) hivi Leo tarehe 11/02/2023,Kwa lengo la kuinua ubora wa Elimu nchini Tanzania.
Katika kutimiza lengo hilo,Mama Samia Suluhu Hassan ametambua pia changamoto zinazowakumba wanazuoni, ikiwa ni pamoja na pesa ya kujikimu kutokidhi mahitaji yao ya msingi hali inayopelekea wanazuoni hao kujinyima kwenye swala la Kula Kwa kujiwekea bajeti ya aftatu Kwa siku na wengine Kula mlo mmoja Kwa siku.kwa kulitambua hilo Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo kuwa waongezewe pesa ya kujikimu."...unajipanga ule mara moja Kwa siku...sasa, waziri wa Elimu nenda kaangalie. Tutaanza na elfu kumi." Hayo ni maneno ya Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha kuwajali vijana Kwani ndio nguvu ya Taifa.
Kadhalika Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kujituma ili wawe msaada Kwa jamii katika kuinua maendeleo nchini ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira.



official



Katika msimu huu wa  valentine's Day, UDOM wameona ndio muda wao kuisimamisha semista, watu walambe glucose ndani ya sik...
10/02/2023

Katika msimu huu wa valentine's Day, UDOM wameona ndio muda wao kuisimamisha semista, watu walambe glucose ndani ya siku moja ili wapate nguvu mpya kukabiliana na UE kwa kuja na kitu cha kujipoza na semista hii .Kitu chenyewe ni SCARLET FASHION SHOW itakayofanyika Pestana Siku ya kesho tarehe 11/02/2023.
Kwenye show hii kubwa sana na wakali wa comedy watakuwepo.
Subiri uone na kuthibitishaa kuwa "Burudani ni sehemu ya maisha"...Kwanini upitwe?



Mchuano huu mkali wa kufunga semista umetarajiwa kufanyika siku ya Kesho terehe 11/02/2023 ukihusisha mechi nne Ambapo m...
10/02/2023

Mchuano huu mkali wa kufunga semista umetarajiwa kufanyika siku ya Kesho terehe 11/02/2023 ukihusisha mechi nne Ambapo mechi zote hizo zitachezwa katika viwanja vya Chuo kikuu cha Dar-es-Salaam (UDSM)kumaanisha kuwa UDSM watakuwa kwenye viwanja vya nyumbani. TMDA VS UDSM itachezwa Ground No.1 kuanzia saa 7:30 AM,CBE na DIT watachuana katika kiwanja cha ground No.2 kuanzia saa 7:30AM ,TRA VS ARU watamenyana ground No.1 kuanzia saa 9:00AM, na bila kuwasahau TRA VS TPA watatoana jasho ground No.2 kuanzia saa 9:00 AM.Hakika kesho ni patashika nguo kuchanika katika viwanja vya UDSM katika mtanange huu mkali. Je Nani ataibuka mshindi kwenye kandanda hili?...kesho itafahamikaaaaaaaa......




"Wakipata ujuzi huu unawawezesha kupata machapisho kirahisi na kuweza kuyatumia kirahisi katika majukumu yao ya utafiti,...
10/02/2023

"Wakipata ujuzi huu unawawezesha kupata machapisho kirahisi na kuweza kuyatumia kirahisi katika majukumu yao ya utafiti, kufundisha na kufanya utafiti elekezi", Hayo ni maneno ya Dkt. Grace Msoffe Mkurugenzi wa huduma za maktaba katika chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) ambapo siku ya leo tarehe 10/2/2023,kurugenzi ya huduma za maktaba kwa kushirikiana na jumuiya ya wanataaluma Chuo kikuu cha Dodoma (UDOMASA), wameandaa mafunzo ya siku mbili yanayolenga kuongeza ujuzi kwa wanataaluma katika kutafiti taarifa mbalimbali za machapisho ambazo watatumia katika kufundishia,kufanya utafiti na kutoa ushauri elekezi.
_udom255

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kukutana na Kufanya mazungumzo na Jumuiya ya...
10/02/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kukutana na Kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Wanafunzi, Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania TAHLISO February 11 Mwaka huu.

Mazungumzo hayo kati ya Rais na Vijana hao wasomi yanatarajiwa kufanyika Ikulu Jijini Dodoma.

TAHLISO ni jumuiya ya Vijana wasomi wa Vyuo vikuu na Vyuo vya kati Nchini.







Afisa uhusiano wa umma wa Hospitali ya Benjamini Mkapa(BMH) jijini Dodoma Mheshimiwa Jeremiah Mbwambo alikutana na wanaf...
09/02/2023

Afisa uhusiano wa umma wa Hospitali ya Benjamini Mkapa(BMH) jijini Dodoma Mheshimiwa Jeremiah Mbwambo alikutana na wanafunzi wa Bachelor of arts in journalism and Public relations(BAJP) wa mwaka wa kwanza na wa pili, wa Chuo kikuu cha Dodoma, februari 8,2023 chini ya usimamizi wa mkufunzi wa somo la uhusiano kwa umma yaani Public relations Mrs. Mary Hospicia Kafyome kwa lengo la kuwanoa vijana hao na kuwaandaa kuwa maafisa uhusiano wa umma bora hapo badae.
Aidha katika semina yake Mheshimiwa Jeremiah Mbwambo amebainisha kuwa Benjamin Mkapa hospital(BMH) ndiyo hospitali pekee inayopandikiza figo kwa kutumia madaktari wake wazawa. Lakini pia aliwaambia wanafunzi wawe wanaojituma katika kazi na kuwashauri kabla ya kuanza kufanya kazi katika ofisi watakazo chaguliwa ni heri wakajua ofisi vizuri kwani itawasaidia kulinda picha ya taasisi na hivyo taasisi itawategema.
Pia mkufunzi wa somo la uhusiano wa umma, Mrs. Kafyome alitoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Mbwambo kwa ushirikiano wake.
Pia Mrs. Kafyome kwa kushirikiana na wanafunzi wake wameandaa charity chini ya Students of UDOM Public Relations Association(SUPRA) katika hospitali ya Benjamin Mkapa siku ya jumamosi tarehe 11/02/2023 wakiwa na ujumbe unaosema UHUSIANO BORA, JAMII BORA.mia22

_udom255

Leo, februari 9,2023 katika ukumbi wa idara ya habari (maelezo) jengo la PSSSF makole Ghorofs ya 8, Dodoma, Kaimu mkuu w...
09/02/2023

Leo, februari 9,2023 katika ukumbi wa idara ya habari (maelezo) jengo la PSSSF makole Ghorofs ya 8, Dodoma, Kaimu mkuu wa Chuo cha Bahari Dar-es-Salaam(DMI), Dkt. Tumaini Gurumo amefanya mkutano na vyombo vya habari akizungumzia utekelezaji wa majukumu ya Chuo kwa kipindi cha awamu ya sita.
Dkt. Gurumo amebainisha kuwa chuo kinatoa elimu na mafunzo ya ubaharia kuanzia madaraja ya usaidizi(Ratings) hadi madaraja ya juu ya maofisa wa melini kwa upande wa uongozaji meli au unahodha na uhandisi wa mitambo ya meli(master marine and chief marine engineer). Awali mafunzo haya yalikuwa yakikomea daraja la tatu na la nne la maofisa wa vyombo vya usafiri majini.
Habari kamili na picha kutoka ukurasa wa .

Address

Dodoma

Telephone

+255620188264

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UNI_Updates.tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share