24/04/2026
Kuku wanamaliza chakula mapema Nitafanyaje chakula kilo 5.5 kitoshee mpaka siku 60?
๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ๐๐ฝ
Habari yako, leo nilipata ugeni wa mama cheupe [sio jina halisi] huyu ni mteja wangu mzuri wa CFP za kuku wanaokua hapa Dodoma
Leo alikuja dukani na alikuwa ana changamoto yake ambayo ni hii "afanyaje chakula kitoshee mpaka siku 60" nilimpa ushauri wa nini Cha kufanya ili chakula kilo 5.5 kitoshee mpaka siku 60
Inawezekana huelewi hii dhana ya chakula kilo 5.5 imetokea wapi, usiwaze... Iko hivi mfumo wetu wa ulishaji wa kuku chotara umegawanyika sehemu mbili
Sehemu ya kwanza ni kuanzia siku 1 mpaka siku 25 ambapo kuku mmoja anakula chakula kilo 1 sehemu ya pili ni kuanzia siku 25 mpaka siku 60 ambalo kuku mmoja anakula chakula kilo 4.5
Kwahiyo kuanzia siku 1 mpaka siku 60 jumla kuku chotara mmoja anakula chakula kilo 5.5 si tumeelewana?
Sasa Ikiwa na wewe unapata changamoto hiyo ya chakula kilo 5.5 kutofika siku ya 60 Fanya mambo yafuatayo
1.Kwanza pakua hii chati ya kuku wa sasso ambayo utaitumia kujua kiwango cha chakula wanachokula kila siku kuanzia siku 1 mpaka siku 60
Kupakua hiyo chati bofya hii link hapa๐๐ฝ
https://drive.google.com/file/d/1JyGNxKDUKYsQyaQAkHvE0KB-702M1Mhr/view?usp=drivesdk
๐๐ฝK**a huwezi kupakua hii chati tafuta mtu akusaidie kuipakua na unaweza kwenda nayo stationery wakakuchapishia ukawa na nakala ngumu [hard copy]
๐๐ฝChati hii ni ya sasso na tunaitumia kwa kuku chotara aina zote, hatuna chati za chotara wengine k**a unayo unaweza kuitumia.
2.Jambo la pili Jifunze kutumia hiyo chati kwa kuangalia hii video hapa kwa kubofya hii link ๐๐ฝ
https://youtu.be/ssrq3vHNL0o
๐๐ฝK**a unapata changamoto kuangalia hii video tafuta mtu akusaidie namna ya kufungua hii video ya YouTube najua tunatofautiana!
3.Jambo la tatu hakikisha unawalisha kuku kwa kipimo kila siku k**a ambavyo hiyo chati inaonesha kiwango husika kwa kila siku
Hapa unahitaji mzani, k**a Bado huna mzani tupigie 0752 912132 kuagiza mzani wa kidijitali bei yake ni 20,000 na unapima kuanzia gram 100 mpaka kilo 50. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Moshi Agrovet tunapatikana Dodoma Majengo Sokoni
Zingatia kwamba kiwango cha chakula wanachokula kitakuwa kinabadilika kadri wanavyokua siku kwa siku
4.Ulishaji wa chakula ni asubuhi na mchana utagawa chakula nusu kwa nusu yaani k**a kuku wako chotara wanakula chakula kilo 20 kwa siku utawapa kilo 10 asubuhi na jioni utawapa kilo 10
๐๐๐๐๐๐๐๐
Jifunze jinsi ya kuwalisha kuku wako kwa kufuata viwango vinavyoelekezwa kupitia hiyo chati
Tafadhali sisi hatutakufanyia hayo mahesabu ndio maana tumeandaa chati na hiyo video ili uweze kujifunza na kufanya wewe mwenyewe kila siku hapo bandani kwako.
Ni rahisi Wala sio ngumu
Asante sana kwa usikivu wako kwenye hili suala ๐๐ฟ
CFP
Ulishaji wa uhakika