Marko Mlonganile

Marko Mlonganile Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Marko Mlonganile, Business service, Dodoma.

Business Consultant/Coach // Mtalaam/Mshauri wa Biashara/Uwekezaji

Embedodo // www.embedodo.com

Like na follow kwenye mitandao yote ya kijamii jina ni Embedodo

Hayati JP Magufuli aliwahi kusema kuwa Tanzania inapaswa kuwa Donor County (Nchi inayotoa msaada) na sio omba omba. Unab...
25/03/2026

Hayati JP Magufuli aliwahi kusema kuwa Tanzania inapaswa kuwa Donor County (Nchi inayotoa msaada) na sio omba omba. Unabii umeanza kutimia.

Viva & viva

18/01/2026

Hii inaumiza saana. Prof anaongea kiswahili, mswahili wa Rombo, kiingereza ni Lugha yake ya tatu ya kuungaunga. Anasema 'Watanzania " Waombe ruhusa ya kufundisha watoto wao kwa lugha yao. Viongozi wa Masaki mnaishi dunia yenu. Asilimia 99 ya watanzania ni sisi waswahili. Hizi kauli ni dharau kubwa na ubaguzi wa wazi kwa Watanzania.

Tuacheni watanzania tusome kwa lugha yetu kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu. Hizo lugha zingine watasomea wenye lugha zao. Why mnanyanyasa wananchi mnaowaongoza? Kisa watoto wenu wanasoma Cambridge au????

HERI YA MWAKA MPYA 2026 WATANZANIA WENZANGU. KWA MWAKA 2026 NITAJIKITA KWENYE AGENDA ZIFUATAZO:1. KUANZISHA HALMASHAURI ...
01/01/2026

HERI YA MWAKA MPYA 2026 WATANZANIA WENZANGU.

KWA MWAKA 2026 NITAJIKITA KWENYE AGENDA ZIFUATAZO:

1. KUANZISHA HALMASHAURI ZA MIKOA
Utaratibu utakuwa kila halmashauri watachagua mjumbe mmoja katika uchaguzi mkuu ambaye ataungana na Mwenyeviti/Mameya wa halmashauri, Makamu wao pamoja na wabunge wa mkoa husika kuunda Baraza la Wawakilishi la Mkoa. Kiongozi wao atachaguliwa miongozi mwa wajumbe wanaotoka chama chenye wajumbe wengi na ataitwa Gavana wa Mkoa na atasaidiwa na naibu gavana wa mkoa. Mtendaji Mkuu ataitwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mkoa (Regional Exercutive Director). Wawakilishi wa kila halmashauri watalipwa na halmashauri zao, huku mkoani ni posho tu za vikao. Wabunge wataendelea kulipwa na Bunge na Mameya/Wenyeviti/ Makamu/Naibu watalipwa na halmashauri zao na hawataruhusiwa kuwa magavana, naibu gavana wala mwenyeviti wa k**ati bali watabaki kuwa wajumbe tu. Nafasi ya Mkuu wa Mkoa na RAS wake itabaki k**a ilivyo kwa Mkuu wa Wilaya na DAS kwa sasa kushugulikia masuala mahsusi. Hatua hii ni muhimu kusogeza serikali na wananchi. Kwa mfumo wa sasa serikali ipo mbali sana kutoka kwa wananchi na wanakutana kwenye ziara badala ya kuishi nao, kuwa nao, kushinda nao. Changamoto nyingi zinapaswa kumalizwa na mamlaka za mkoa badala ya kusubiri viongozi wa kitaifa pekee.

2. KUANZISHA MAMLAKA HURU (K**A BOT) YA KUSIMAMIA MASHIRIKA NA TAASISI ZA UMMA
Mamlaka hii itakuwa huru kuanzisha, kuuza, kufuta na kuunganisha mashirika yote na Taasisi ambazo zinafanya biashara. Zitabaki zile tu mamlaka, wakala, tume, bodi, na zingine k**a hizo ambazo lengo mama ni kusimamia sekta. Mfano sekta ya maliasili, TFS, Tawa na Bodi ya Utalii ni wasimamizi. Ila Tanapa na Ngorongoro ni wafanyabiashara hivyo watahamishiwa kwenye mamlaka ya usimamizi wa mashirika. Pale uchukuzi, TPA, TRC, ATCL, TRC, TAA, wote ni wafanyabiashara; Latra, Tasac na TCAA ndio wasimamizi. Wasimamizi/mamlaka/ wakala watabaki chini ya Msajili wa Hazina. Watumishi wa mashirika wote hawatakuwa watumishi wa umma tena na watafanya kazi kwa ajira za mkataba. Watumishi wa Umma wanaofanyakazi kwenye mashirika mkataba ukiisha/ukivunjwa wanarudishwa Utumishi ila ambao sio watumishi itakuwa ndio mwisho wa ajira zao.

3.KUANZISHA MFUKO WA UWEKEZAJI WA TAIFA
Nchi zote zenye rasilimali zina mifuko hii ambayo inakusanya faida toka BOT, mashirika mbalimbali, mirabaha ya madini, gesi, misitu na rasilimali zingine na kuziwekeza duniani. Pia hutoa mitaji kwa makampuni binafsi na yale yanayomilikiwa na serikali. Huwa sehemu nzuri kwa serikali kukopa lakini huwezesha miradi mikubwa k**a bandari ya kimataifa ya Bagamoyo, Tanga na Mtwara au miradi k**a LNG Plant nk. Kumbuka rasilimali huisha au hupoteza thamani (k**a ilivyo kwa mafuta/makaa ya mawe) lakini vizazi vinaendelea kuja. Lazima tuendelee kuwekeza ili rasilimali hizo zifaidishe vizazi vijazo pia kuwezesha Tanzania kushiriki uchumi wa Dunia.

4. KUUNGANISHA MIKOA YOTE KWA RELI YA SGR, HALMASHAURI ZOTE PANDE ZOTE KWA LAMI NA KATA ZOTE KWA LAMI/ZEGE AU CHANGARAWE.
Binafsi sio muumini saana wa ujenzi wa reli ya mkoloni. Reli inayowaza zaidi kuhudumia wengine kuliko sisi. Mpango wa reli uboreshwe. Reli ya kati ya SGR inaendelea kujengwa vipi kuhusu reli ya Tanga-Arusha-Musoma- Mwanza? Vipi kuhusu Reli ya Mtwara-Songea- Makambako/ Mbambabay? Vipi kuhusu Reli ya Tanga-Dar-Mtwara? Vipi kuhusu reli ya Arusha-Dodoma-Iringa- Mbeya? na vipi kuhusu reli ya Tabora-Mpanda-Sumbawanga-Mbeya? Mfumo huu wa reli unawezesha Mikoa yote kuunganishwa kwa reli.

Pia katika kila halmashauri ya Wilaya/Mji/ Jiji lazima iunganishwe kwa lami kwa Pande zote kutoka halmashauri nyingine au mkoa mwingine. Na mwisho tuunganishe kata zote kwa changarawe kwa kila upande. Afadhali zile trioni 6 zilizopangwa kupeleka umeme kila Kitongoji zijenge kwanza barabara hizi muhimu. Hakuna haja ya kuwa na umeme kwenye kitongozi wakati barabara ya kwenda wilayani/katani tu haipitiki kwa nusu mwkaka. Kupanga ni kuchagua.

5.FURSA KWA VIJANA
Mwaka huu nitatumia muda wangu kueleza fursa kwa vijana zilizopo Tanzania, nchi jirani na duniani. Fursa katika sekta za kilimo, Madini, Tekinolojia, ajira, masomo, uwekezaji, usafirishaji na zinginezo. Lengo ni kuwafungulia dunia vijana wenzangu na wapambanaji wenzangu.

Ni Mimi MTZ7 (Mpwa wa Tz)

Sisi baado tunahangaika na English Medium badala ya kutafta maarifa. Ni utumwa wa fikra. Kiswahili kinapaswa kuwa lugha ...
15/08/2025

Sisi baado tunahangaika na English Medium badala ya kutafta maarifa. Ni utumwa wa fikra. Kiswahili kinapaswa kuwa lugha ya kufundishia kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Tuache fikra za kitumwa; tupende vyetu

Hongereni MAMLAKA kwa kubeba kombe lenu Wenyewe. Sisi k**a Simba SC Tanzania  tumewaachia hadi 2030 k**a mlivyosema; Sis...
25/06/2025

Hongereni MAMLAKA kwa kubeba kombe lenu Wenyewe. Sisi k**a Simba SC Tanzania tumewaachia hadi 2030 k**a mlivyosema; Sisi tunaheshimu MAMLAKA. Ila siku mkiamua tucheze mpira halisi na nyie mtaenjoy zaidi kuliko haya maigizo na maagizo yanayoendelea. Hongereni sana MAMLAKA. cc Young Africans Sports Club Ligi Kuu Tanzania AzamSports Tanzania Football Federation

14/06/2025

YANGA BINGWA HADI 2030; WATOTO WA MAMA WANADEEKA TU!

let's focus na mashindano ya kimataifa hizi takataka tuwaachie wahuni.
1. Unazuia Simba SC Tanzania kwa makomandoo; mabaunsa, wasimamizi wa uwanja na simu za viongozi toka juu.
2. Mamlaka za soka zinaahirisha mechi kutokana na vurugu hizo kwenye soka
3. WATOTO WA mama wanaenda CAS; upuuzi, wao; kesi inatupwa.
4. Mamlaka zinapanga tarehe ya mechi
5. WATOTO wa mama wanagoma Kwa jeuri na dhihaka
6. WATOTO wa Mama wanapanga tarehe wanayotaka wao kwa matakwa yao
7. Mamlaka zinatii na baadhi ya viongozi kujiuzulu
8. Mara wanasingizia wanadai TFF wakati barua zao zinaonesha wanaridhia kukatwa kufidia madeni yao
9. WATOTO wa mama wana hodhi team 8 na kuwa na ushawishi wa pekee wa timu 2; yaani walau timu 6 hazina ndoa nao
10. WATOTO wa mama wanapanga matokeo waziwazi pamoja na kujipangia kikosi cha timu pinzani cha kucheza nao
11. WATOTO wa mama wanatisha mamlaka za soka na zinatii kutekeleza matakwa yao batili.
12. Mpira wetu unaendeshwa kwa matakwa ya WATOTO wa mama na sio kwa kanuni, sheria na taratibu.
13. Kwa sasa WATOTO wa mama ndio mamlaka za mpira
14. Simba amepambana kujenga hadhi ya soka la Tanzania kwa jasho na damu; WATOTO wa mama wanapambana kubomoa na kulisambaratisha kabisa.
15. Kilichotokea Jana kimeondoa kabisa maana halisi ya soka ya kiushindani Tanzania; KILICHOBAKI sasa ni maigizo tu ya soka.

RIP Tanzania Football Tanzania Football Federation Ligi Kuu Tanzania Wallace Karia Simba Sports Club Young Africans Sports Club

In Tanzania there is something looks like beef🐂🥩, but it is not real meat 🥩, it is a stiff real skin of drudgery animal ...
04/05/2025

In Tanzania there is something looks like beef🐂🥩, but it is not real meat 🥩, it is a stiff real skin of drudgery animal even hyena can't afford it, only a man with durable steel teeth can chew and enjoy. By PLO Lumumba, Speaker, Arusha Economic Forum, AICC, 3rd May 2025.

Mtambo wa kuchuja samadi na kutumia shambani
16/03/2025

Mtambo wa kuchuja samadi na kutumia shambani

16/03/2025

Boonge la hospital; ukimlaza ndugu yako au hapa atakufilisi. Kila siku ataajifanya anaumwa Sana ili aendelee kubaki.

Ndio maana halisi ya kukua na kuendelea.. Sio miaka 30; tuko vile vile, tunalima vile vile, zana zile zile, na mavuno ya...
16/03/2025

Ndio maana halisi ya kukua na kuendelea.. Sio miaka 30; tuko vile vile, tunalima vile vile, zana zile zile, na mavuno yale yale

Baada ya mhitimu wa chuo kikuu kumaliza VETA
16/03/2025

Baada ya mhitimu wa chuo kikuu kumaliza VETA

Address

Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Marko Mlonganile posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Marko Mlonganile:

Share