08/06/2018
Usalama wa chakula kwa afya ya mtumiaji/mlaji.
Tunaendelea na somo letu LA kanuni bora za usindikaji/uzalishaji.
UNUNUZI WA MALIGHAFI.
Ateuliwe mtaalamu maalumu wa kutayarisha orodha ya malighafi na vifungashio kulingana na ubora unaohitajika.
Malighafi zinuniliwe kwa wafanyabiashara au wakulima wanaotambilika ikiwezekana kuwepo na mkataba kati ya mkulima na msindikaji.
Kuwepo na mfumo utakaohakiki ubora na viwango vya malighafi Mara tu malighafi inapofika kiwandani mfano Kipimia unyevu kwa wasindikaji wa nafaka ni mhimu, kifaa cha kupima maji kwa wasindikaji wa maziwa nk.
Malighafi zitakazokuwa zimeharibika zitolewe Mara moja ili kuepuka uharibifu wa malighafi zingine. Ni mhimu sana , wasindikaji wengi wamekuwa wakipata hasara kwa sababu ya kutofahamu kwamba malighafi mbovu zinaweza kuharibu malighafi zingine.
USAFIRISHAJI WA MALIGHAFI.
Unahitaji uangalifu mkubwa wakati wa usafirishaji kuepusha uharibifu wa chakula.
Wazalishaji/wasindikaji wapo wa aina nyingi, kuna wasindikaji/wazalishaji ambao hununua malighafi shambani au sokoni na kusindika kwa kutumia vitendea kazi vyao yaani mashine nk. Kuna wale ambao hununua bidhaa ambazo tayari zimeshasindikwa mfano Mchele, unga, maziwa ya unga nk na kufungasha(kupack) wenyewe, kuna wale wanunuzi na wasambazaji wa malighafi. Makundi haya yanapaswa kuzingatia kwa kina namna ya usafirishaji wa malighafi kwenda kwenye eneo la uzalishaji.
SIFA YA VIFAA VYA KUBEBEA MALIGHAFI.
Vifaa vya kubebea vyakula(magari) yakaguliwe kabla hayajapakia ili kuhakikisha usalama wa vyakula. Hii ni kwa wale wasindikaji wanaonunua mzigo mkubwa. Kwa wale wasindikaji wanaosafirisha mizigo kutumia maroli au mabus ya abiria(gari lisilo rasimi kwa usafirishaji wa chakula) mnatakiwa kuhakikisha vifungashio vya malighafi viko vizuri kwa ajili ya usalama wa chakula.
Pia vifaa vya kubebea vyakula(gari) vitumike kubeba vyakula tuu na si vinginevyo kwa ajili ya usalama wa vyakula . Mfano gari linalosafirisha nyama, samaki , maziwa nk haliruhusiwi kubeba mchanga, mbolea , kemikali nk hii ni kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji/ mtumiaji. Vifaa hivyo pia vinapaswa visafishwe pindi vinapomaliza kutumika kuzuia maambukizi ya vimelea na uchafu mwingine.
Malighafi nyingi kwa asilimia kubwa zinahitaji uthibiti joto kipindi cha usafirishaji. Uthibiti joto..ni joto ambalo linafanya malighafi isipoteze ubora wake kuanzia0°C-25°C hii hutegemea na aina ya malighafi. Kwenye kiwango hiki cha joto vimelea Vingi( micro.organisms) ambavyo hatuvioni kwa macho mfana bakteria, fungus, virusi haviwezi kukua kwenye joto dogo na hii inasaidia kusafirisha malighafi yako katika khali ya ubora.
Malighafi mfano nyama, Samaki, maziwa vinapaswa kusafirishwa vikiwa vimeganda katika vyombo vinavyozuia visiyeyuke.
HATUA ZA USINDIKAJI.
1. Kupokea na kukagua(receiving).
Kwa wasindikaji wanaonunua shambani au sokoni hakikisha malighafi imetunzwa vizuri, iliyovunwa kwa wakati baada ya kufikia kiwango cha kukomaa.
Kwa wasindikaji ambao wanalima wenyewe hakikisha uvunaji, ukaushaji, usafirishaji na uhifadhi vifanyike kwa uangalifu kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu.
Kwa hiyo malighafi inapopokelewa kwa ajili ya usindikaji zingatia mambo yafuatayo
1.Hakikisha malighafi imekauka kwa kiwango kinachofaa kwa upande wa nafaka ikiwezekana tumia kifaa maalumu cha kupimia unyevu.
2. Isiwe ya kuharibiwa na wadudu kwa malighafi zote mfano Matunda nk
3.Iwe imekomaa katika kiwango kinachotakiwa.
4.Isiwe na uchafu au mchanganyiko wa mbegu zingine( kwa upande wa nafaka).
5.Isiwe na ukungu mfano mahindi, mihogo, viazi nk
2.UHIFADHI WA MALIGHAFI.(Storage)
Ni mhimu malighafi ihifadhiwe vizuri kwenye ghala au stoo kabla ya kutumika. Kwa upande wa nafaka magunia yenye malighafi yapangwe juu ya chaga(Pallet) au Trubai ili kuzuia unyevu.
Hakikisha ghala/stoo ya kuhifadhia malighafi ni safi, isiwe inavuja na kuruhusu wadudu mfano panya kuingia ndani. Kwa wasindikaji wa nafaka ni mhimu kutenga malighafi kiasi itakayotumika kwa mda usiozidi miezi mitatu kwani mashambulizi ya wadudu huwa ni ya kiwango chini sana na hivyo hushauriwi kutumia viuatilifu(pesticides).
3.Maandalizi(preparation).
Katika hatua hii malighafi zote hutengenezwa kwa kuongezewa thamani ya chakula mfano mbegu za alizeti husagwa na kutoa mafuta, Matunda k**a vile maembe huoshwa, hukatwakatwa na kusagwa kuwa juisi nk.
Hivyo unashauriwa kuanza kutengeneza/kusindik**alighafi uliotangulia kuhifadhi stoo.
4. Ufungashaji na kuweka lebo(Packaging and labeling).
Katika hatua hii bidhaa iliyozalishwa kwenye malighafi husika hufungashwa kwenye vifungashio safi na vilivyokidhi viwango kwa ajili ya bidhaa husika na kubandikwa lebo inayoitambulisha bidhaa hiyo.
Nitoe angalizo katika swala vifungashio...kabla haujaanza kusindika/ kununua bidhaa yako kwa ajili ya kufungasha hakikisha umefanya tafiti juu ya vifungashio vya bidhaa yako ni mhimu sana..k**a unapata shida jitahidi hata kuonana na wataalamu wanaofahamu vifungashio bora. Kila bidhaa ina vifungashio vyake kutokana na sheria ya chakula ili kuepuka hasara ya kukataliwa kwa vifungashio vyako na mamlaka husika(TFDA/TBS) zingatia hilo. Lakini pia vifungashio vizuri huvutia wateja na pia hutunza ubora wa bidhaa yako. Kwa upande wa lebo kuna vitu vya kuzingatia ambavyo kabla haujatengeneza unatakiwa kuwaona TFDA kwa ajili ya maelezo kutokana na viwango(standards) inavyosema.
5.UHIFADHI WA BIDHAA(storage)
Bidhaa iliyotengenezwa inatakiwa ihifadhiwe kwenye sehemu safi . pia bidhaa inatakiwa ikaguliwe Mara kwa Mara na kugeuzwa ili kuzuia kuharibika kutokana na joto nk
6.USAMBAZAJI(distribution).
Hatua hii ni ya usambazaji wa bidhaa yako kwenda kwa mlaji, vifaa vinavyotumika kusafirishia bidhaa vinatakiwa viwe visafi k**a nilivyoeleza kwa upande wa malighafi. Hizi ndio hatua za usindikaji.(processing steps).
Karibuni kwa maswali, mapendekezo, ushauri napatikana 0685295391 Juliana Kitinde mtaalamu wa maswala ya usindikaji wa vyakula na vinywaji....itaendelea