Ushauri Juu Ya Maswala Ya Kiuchumi na Uwekezaji

Ushauri Juu Ya Maswala Ya Kiuchumi na Uwekezaji Jifunze jinsi ya kuwekeza

23/01/2022

� ʟɪғᴇ ɪs ɴᴏᴛ ᴘᴇʀғᴇᴄᴛ༄ 𝚋𝚞𝚝 𝚢𝚘𝚞𝚛 𝚘𝚞𝚝𝚏𝚒𝚝 𝚌𝚊𝚗 𝚋𝚎�
ᴘublic_Figure
☟︎︎︎
ғᴏʟʟᴏᴡ ᴍᴇ

08/11/2019

*Kanuni za kuikuza biashara ndogo ili iwe biashara kubwa*
Kila kitu kinachoanza kwa hatua ndogo kinatakiwa kukua katika ukubwa, hivyo unapoonzisha biashara ndogo basi fahamu namna ambavyo biashara hiyo itakuwa kubwa.
*Zifutazo ndizo kanuni za kuikuza biashara ndogo ili iwe biashara kubwa.*
Jitahidi pia kujua washindani wako wanafanya nini haswa wale ambao wako juu yako zaidi. Hii itakusaidia sana kuweza kujua ni mambo gani ambayo unaweza kuyatumia kwa nafasi yako kuweza kupanda juu zaidi ya hapo ulipo, usijifungie tuu ndani na wala usitake kujua wengine pia wanafanyaje kitu ambacho kinataka kufanana na chako. Fanya uchunguzi kwa kuingia google andika kitu ambacho unataka kujua kuhusu biashara yako na baada ya hapo andika pembeni mapungufu ambayo umeyaona katika biashara yako ambayo sasa unaweza anza kufanyia kazi pia.
Mitandao ya kijamii ni sehemu nzuri ya kuweza kutangaza biashara yako, hakikisha unaonekana kwamaana ya kufanya biashara sio unaonekana kwa manufaa ya watu kukuona na wewe upo kwenye mtandao. Kuna mitandao k**a facebook, instagram, twitter, linkeldn inanguvu sana kwa wafanyabiashara haswa kuweza kutambulisha biashara yako kwa watu ambao huwajui pia.
Nimekuwa nikitumia mitandao hii katika shughuli zangu na nimeona matokeo makubwa sana kwa kipindi kifupi nawe inawezekana hebu tenga muda kwenye kujifunza kutumia mitandao ikufanyie biashara.
Weka malengo katika biashara yako. Bila malengo katika biashara yako unaweza kubaki hapo hapo ulipo. Hakikisha unapoanza biashara yako uweze malengo kwa kuangalia unataka biashara yako iweje baada ya muda flani na ufanye nini kwa wakati huo ili uweze kusogea katika kutimiza malengo yako hayo mfano umeanza biashara ya 100,000/= na katika malengo yako unataka baada ya mwaka mmoja biashara yako iwe ya mtaji wa 1,000,000/= hapa ni lazima upange kila siku ufanye nini kuweze kufanya ndoto yako kutimia, lakini pia ni lazima ujue mambo gani unatakiwa kuacha.
Ijue biashara yako na jiendeleze katika kujua mambo mapya ambayo yatakusaidia kuweza kuongeza ubunifu katika biashara yako ambayo unaifanya. Usilale na kuamka tuu na kwenda kwenye biashara yako jiulize leo umejifunza nini kipya cha kuongeza katika biashara yako na umegundua nini unatakiwa kupunguza ili uzidi kusonga mbele na biashara yako izidi kuwa mpya katika macho ya wateja wako. Ukiwani mtu wa kubaki vile vile katika biashara yako utakimbiwa na wateja na mwisho wa siku utaanza kuisema biashara yako ni mbaya. Kuna mambo k**a kujua jinsia ya kuongoza mzunguko wa hela katika biashara yako, jinsi ya kumtawala mteja wako na kumfanya wa kudumu, kujua soko jipya kwaajili ya bidhaa yako n.k. KWA HUDUMA YA BUSINESS PLAN WASILIANA NAMI NIKUSAIDIE

08/11/2019

*ELIMU YA MATUMIZI YA FEDHA*
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kuitumia. Kanuni ifuatayo imetumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani.

*Kanuni*
•Fungu la kumi 10%
•Akiba 30%
•Matumizi 40%
•Dharura 10%
•Msaada 5%
•Sadaka 5%
*Jumla 100%*

Hii kanuni inafanya kazi katika kila fedha unayopata k**a pato lako la mwezi.

*Mfano* K**a unapata Sh. Laki 5 kwa mwezi (500,000/=) fungu la 10 ni Sh. 50,000/=, hii ni mali ya Mungu si yako. Unatakiwa utoe kanisani kila mwezi, pia hata k**a umepewa fedha k**a zawadi unapaswa uitolee fungu la 10.

*Faida za Fungu la kumi*
•Hulinda kazi au biashara unayoifanya dhidi ya adui.
•Magonjwa, ajali(vitu vitakavyokufanya utumie fedha bila mpangilio) n.k yanakuwa mbali nawe.

*Akiba 30*
•Fedha hii unaiweka kwa matumizi yako ya baadae k**a kujenga, kusomesha, kulima, vitega uchumi n.k.
*mfano* k**a pato lako kwa mwezi ni sh. 500,00/= asilimia 30 ni sh. 150,000/=

*Matumizi 40*
•Fedha hii itatumika kwa matumizi ya kila siku, chakula, maji, umeme n.k
•Hutumika pia kwa matumizi mengine ya starehe, mavazi n.k
•K**a pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/=, asilimia 40 ni sh. 200,000/=
• *angalizo* matumizi yasizidi fedha hiyo.

*Dharura 10*
•Hii ni fedha unayotunza kwa ajili ya mambo usiyoyatalajia k**a msiba, magonjwa au kukwama jambo lolote n.k.
•K**a pato lako ni sh. 500,000/= unatunza sh. 50,000/= kwa ajili ya dharura kwa mwezi.

*Msaada 5%*
•Hii ni fedha ya msaada kwa watu wenye shida; watoto yatima, wajane, walemavu n.k
• k**a pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= unatunza sh. 25,000/= kwa ajili ya msaada.

*Sadaka 5%*
•K**a pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= tenga sh. 25,000/= kwa ajili ya sadaka kwa mwezi.
•Igawe fedha hii Mara 4 kwa sababu mwezi una jumapili 4 ambapo utapata ni sh. 6,250/=. Hivyo kila jumapili utaenda kutoa sh. 6,250/=.

*Kumbuka*;
Kitu chochote kinachoitwa sadaka kiombee kabla hujakitoa k**a siku mbili 2 au 3 ndipo uitoe sadaka.
•Jaribu na anza hata na kidogo kidogo, kuwa na nidhamu ya fedha uone nayo itakavyokuheshimu.
MUNGU IBARIKI KAZI YA MIKONO YANGU NA KWA IMANI TUTASHINDA

12/10/2018

Hii ni hatua ya Kwanza katika kuhakikisha unapta ujuzi dhabiti ktk nyaja ya uchumi na uwekezaji endelea kulike na kushare page

20/06/2018

*SOMO LA KUKUFUNGUA AKILI :
Kuna watu wanatamani kuwekeza ila hawana pakuwekeza hivyo wanatafuta njia yakuwasaidia kuzalisha Pesa zao

Sasa biashara kubwa ambayo watu wameikimbilia sana imekuwa Bodaboda

Je, wajua kuhusu Boda? Hakuna biashara isiyo na namahesabu. Kwasasa bei ya pikipiki mpya ni 1.5m. mpaka--2.2 m. Ili kukamilisha usajili wake mpaka iwe arali kutumika kwa usafiri Mahesabu sasa watu wengi akisha chukua mkopo wa 2.2 m anachukua Boda nakumpatia Kijana wakuendesha makubaliano ni 7000/= *kwa siku inaonekana Pesa nyingi kweli ebu njoo pamoja namimi kwa mahesabu
*7000×7 (week 1)= *49,000* .
**49,000×4 (month 1)= *196,000* .
*×12(Year 1)=2,352,000* Hayo ndio mapato ya mwaka mzima faida kwenye mtaji wa 2.2 m faida itakuwa *152,000* bila* kuhesabu week and gharama za uharibifu na ufundi hapo hazipo alafu mtu anasema amewekeza kabisa akifikisha 1.5 m ananunua boda nyingine ili mapato yaongezeke bila kujua k**a anaongeza Mtaji na kuongeza Asara na Msongo wa mawazo kupata habari za pikipiki imek**atwa kila mwezi niuhakika sasa wengine utengeneza kibubu na kila malejesho ya siku uwekwa kwenye kibubu je ni biashara gani yakuishi kwenye kibubu mwaka mzima ?? watanzania tunahitaji kupata elimu sana juu ya biashara na uwekezaji *

Sasa zipo njia nyingi za uwekezaji na zakuzalisha Pesa nzuri ambayo inaweza kukupa Furaha maishani amka ewe mstaafu na mfanya kazi upate elimu juu ya biashara

Bila umepata sababu kwanini baba zetu wanajikuta magonjwa k**a Plesha na stroke miaka michache baada ya Ku Staafu wanawekeza sehem isiyo sahihi
Kesho titaangalia kwa watu wanao wekeza kwenye magari. Uchotakiwa ni like, comment and share.

19/06/2018

Welcome ktk page yangu ambayo inajihusisha na maswala mbalimbali ya kiuchumi na uwekezaji, lengo kubwa la kuanzisha page hii nikupeana ushauri, maoni, mawazo pamoja na mambo mbalimbali ya kiuchumi na uwekezaji kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na maendeleo kwa ujumla. Unachotakiwa ni kushare, kucomment pamoja na kulike page ili kupata taarifa kwa urahisi kila itakapotumwa mpya.. KARIBUNI karibuni sana wadau wote wenye ndoto ya kufanikiwa kimaisha.....💵💵💵💵💵

Address

Makulu
Dodoma

Telephone

+255745400799

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ushauri Juu Ya Maswala Ya Kiuchumi na Uwekezaji posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ushauri Juu Ya Maswala Ya Kiuchumi na Uwekezaji:

Share