01/10/2026
Katika kuendelea kuhamasisha upatikanaji na matumizi ya mbegu bora za mazao katika mikoa inayotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), inayotekelezwa na Wizara ya Kilimo, chini ya ufadhili wa IFAD, KIJANI imeendelea kutoa elimu ya mbegu kwa wakulima katika Kata ya Igalula, wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.
Elimu hiyo imeendelea kutolewa kwa wakulima walioshiriki katika Maonyesho Bunifu ya Mbegu yanayofanyika katika mikoa inayotekeleza programu ya AFDP, ikiwemo Shinyanga, Mwanza, Geita na Tabora kwanzia Septemba 29,2026 hadi oktoba mosi 2026.
Kupitia maonyesho hayo, KIJANI inaendelea kuwaelimisha wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu bora kutoka ASA, hususani mbegu zinazosaidia wakulima kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo ukame na magonjwa.