12/12/2014
Watu wengi wamekuwa wakifikiria kuhusu
namna ya kujikwamua kutoka kwenye
umasikini.Leo hii nitawaelezea kuhusu
biashara ya kufuga kuku wa kienyeji
ambavyo inaweza kukukwamua kutoka
kwenye umasikini. Lengo kuu ni
kuwawezesha watu kutengeneza ajira kwao
binafsi na watu wengine.
Takwimu za uzalishaji (kutaga, kuangua na
kukuza kuku)
Utafiti uliofanywa na Dr. John Bishop kwa
msaada wa shirika la kitaifa la utafiti wa
kilimo nchini Equador na Chuo kikuu cha
Florida nchini Marekani, umeonyesha
kuwa ; K**a kuku akitunzwa vizuri
kutokana na mbinu bora za ufugaji,
anaweza Kuongeza uwezo wa kutaga mayai
kutoka mayai 10 hadi mayai 12 kwa mwezi.
Kwa mfano ukiwa na kuku 12 na jogoo 1
waliolishwa kilo 1 ya nafaka kila siku
unaweza kuuza dazani 10 za mayai kila
mwezi ambayo ni sawa na mayai 4 kila
siku.
Jee unapenda kutajirika kwa kufuga na
kuuza kuku?
Angalia mchanganuo wa mahesabu mapato
yako yatakuwa k**a ifuatavyo, Kwa
kipindi cha miaka 2. K wa mtaji wa Sh.
500,000/= k**a una eneo la eka 1 na
mabanda ya kutosha kiasi cha kuku 10,000.
Ukianza kwa kufuga kuku 25 ( kuku 20 na
jogoo 5) ambao utawanunua kwa Sh.
250,000.00. Hao kuku 20 wakianza kutaga
vifaranga 10 kila mmoja wataangua
vifaranga 200 watunze vizuri katika
vifaranga hao tuchukulie majike yanaweza
kuwa 150 ambao ndani ya miezi 6 au zaidi
nao wataanza kutaga. Kipindi hicho
utakuwa na kuku (200+ 25 =225.) Baada ya
hiyo miezi 6 kuku watakaotaga ni 170 kila
mmoja akipata vifaranga 10 mpaka mwisho
wa mwaka utakuwa na kuku
(1700+20+55=1775) ukiuza kuku 1,000 kwa
bei ya Tshs. 10,000 utapata Tshs.
10,000,000/=. Mwaka wa 2 majike 775
yakiangua vifaranga 10 kila mmoja
utakuwa na kuku 7,550 mwisho wa mwaka
ukiuza kuku 3,000 kwa bei ya Tshs. 10,000
utapata Tshs. 30,000,000/= Hesabu hizi ni
kwa makadirio ya chini sana kwani k**a
nilivyoelezea hapo juu kuku mmoja k**a
atatunzwa vizuri anaweza kuataga mayai
kati ya 10 hadi 12 kwa mwezi.Kuku wa kienyeji wamekuwa wakifugwa
kwa wingi vijijini kwa malengo ya kupata
nyama na mayai kwa ajili ya familia
husika na kwa ajili ya kupata pesa za
kujikimu. Kuku na mayai ya kienyeji yana
faida kubwa kiafya kutofautisha na kuku
wakisasa ambao hukuzwa kwa kemikali.
Idadiya kuku Tanzania inakadiriwa kuwa
na jumla ya kuku Milioni 34 wanaofugwa
na takribani 60.5% ya kaya
zinazojishughulisha na kilimo. Hata hivyo
uzalishaji wake umebaki kuwa duni
kutokana na changamoto za wafugaji
zifuatazo; Utunzaji duni , Udhibiti mdogo
wa magonjwa, lishe duni, makazi duni,
Uzaliano wa karibu, Teknolojia duni,
Kukosekana kwa mtazamo/mwamko wa
kibiashara.
Faida ya kufuga kuku wa kienyeji.
Ufugaji wa kuku wa kienyeji una manufaa
mengi kwa mfano; Kuku hutumia eneo dogo
kuliko wanyama wengine wa kufugwa, pia
hutumia chakula kidogo hivyo ufugaji
unaweza kuendeshwa bila kutumia mtaji
mkubwa. Kuku wanaweza kupewa mabaki
ya chakula pamoja na vyakula vya
kujitafutia k**a vile wadudu,mbegu na
majani. Kazi za usimamizi wa kuku
zinaweza kufanywa na mama na watoto.
Kuku na mayai humpatia mfugaji chakula
bora na kumuongezea mapato. Pia mfugaji
ni k**a mtu aliyewekeza fedha zake benki
au kwenye kitegauchumi kingine ambapo
kuku huweza kuongezeka kutokana na kuku
kutaga na kuangua vifaranga k**a faida
inavoongezeka benki na kwenye
vitegauchumi vingine. Mfugaji ni sawa na
mtu aliyeweka akiba benki kwani akipata
shida anaweza kuuza kuku na kulipa ada,
mahari matibabu ya hospitali pamoja na
shida zingine. Kuku wa kienyeji anasaidia
kusafisha mazingira kwa kula wadudu na
kuongeza rutuba kwa mbolea inayotokana
na kinyesi cha kuku ambacho hakina
kemikali. Mbolea hii ni nzuri sana na k**a
inazalishwa kwa wingi inaweza kuwa
chanzo kingine cha mapato kwa mfugaji wa
kuku. Kuna mjasiriamali ninayemjua
anafuga kuku wengi anazo tani nyingi za
mbolea hii na anauza mbolea ya mavi ya
kuku kwa Sh. 600 kwa kiloba cha kilo 50.
Kuku wa kienyeji ana uwezo mkubwa wa
kuhimili magonjwa, hutaga mayai na
kutunza vifaranga badala ya kutumia
mashine. Kuku wa kienyeji anaweza kuishi
nchi yoyote duniani bila kuathiriwa na hali
ya hewa.
Aina za magonjwa ya kuku na jinsi ya
kukinga magonjwa.
Wapatie chanjo kuku wako kwa afya bora.
Wapatie kinga mara kwamara kila baada ya
miezi 3. Magonjwa yafuatayo ndiyo huwa
yanawashambulia kuku.
New castle
Dalili za ugonjwa huu ni kuku kushindwa
kupumua, kukohoa na kutokwa na
mate,kuwa na kinyesi cha rangi ya kijani,
ugonjwa huu hauna dawa. Chanjo hutolewa
machoni kwa njia ya matone.
Minyoo.
Dalili za mionyoo ni kuku kukosa hamu ya
kula uzalishaji wa mayai kupungua. Ukiona
dalili hizo waone wataalamu wa mifugo
upate dawa.
Wadudu.
Utitiri husumbua kuku, kwa kuwasababisha
kukosa usingizi,ngozi kuharibika,huathiri
uzalishaji wa mayai. Ukiona dalili hizi
wasiliana na wataalamu wa mifugo upate
dawa.
Magonjwa ya mapafu.
Huathiri sehemu za kupitishia hewa na
kuwa na sauti ya kukoroma. Hali hii
hupunguza uzalishaji wa mayai na uzito
wa kuku kupungua. Ukiona dalili hizi
wasiliana na wataalamu wa mifugo upate
dawa.
Mambo mengine unayopaswa kuyajua k**a
mfugaji wa kuku
Inapokuja katika ufugaji wa kuku wa
kienyeji ,mbinu inayotumiwa kijijini ile
kuku huachwa azurure katika boma bila
uchungaji ama na uchungaji mdogo.Kuna
matatizo mengi ambayo kuku hukutana
nayo. Kuku halishwi vyema kwani hula
masalio ya.chakula na mabaki mengine
wanayoyapata. Vifaranga wadogo huachwa
washindanie chakula na kuku wakubwa na
huwa nyama rahisi kwa wanyama
wanaowinda na kula nyama na husambaza
magonjwa. Kuku hawapati maji ya kutosha
na hawana mahali pa kujisetiri dhidi ya
upepo na mvua ama kuwaweka salama
dhidi ya wanyama wanaowinda na kula
nyama bila kusahau wezi. kuku hutaga
mayai ardhini na yanaweza kuharibiwa
kwa urahisi na kuliwa na wanyama
wengine. Sio kawaida kuku kupewa chanjo
na matibabu dhidi ya magonjwa na
vimelea. Matokeo ni kuku wengi huwa
wagonjwa na hukua pole pole,hutaga mayai
machache na nyama kidogo.
Ili kuhakikisha mapato mazuri kutoka kwa
kuku wako,fanya yafuatayo:
Kuwapatia kuku mgao mzuri wa vyakula
tofauti na maji safi.Kutemeana na kipindi
cha mwaka,wataweza kujitafutia chakula
kwa kukwaruza ardhi katika boma.
Wapatie chakula cha ziada ili kuku
waongeze uzani na kuku watage mayai
mengi zaidi. Walishe vifaranga na chakula
kilicho na protini k**a mchwa ili wakue
kwa haraka na wawe na afya. Wajengee
kuku mahali penye giza na patulivu
ambapo wanaweza kutaga mayai yao.Kuku
huhitaji kujisikia wakiwa salama kutoka
kwa wanyama wanaowinda na kula nyama
na wapita njia. K**a kuku watasumbuliwa
mara kwa mara watakuwa wakiviacha
viota vyao na hii huathiri uanguaji wa
mayai. Ikiwa nia yako ni utoaji wa
mayai,ni vizuri kufuga kuku wa k**e
pekee.Jogoo mmoja anaweza kufugwa
aangalie wanyama wanaowinda na kula
nyama na kuwahudumia kuku.Wakati jogoo
wa ziada wanapofikia umri wa
kuuzwa,wanafaa kuuzwa,kuchinjwa ama
kutolewa k**a zawadi kuzuia jogoo kula
chakula ambacho ni adimu na kupigana na
kuwataabisha kuku. Ukubwa wa kundi
unafaa kuafikiana na ukubwa wa nyumba
au banda ,kiasi cha chakula unachoweza
kununua na raslimali za chakula katika
maeneo yanayokuzunguka. Usinunue kuku
kutoka katika vyanzo ambavyo
havijathibitiwa haswa vipindi milipuko ya
magonjwa ni kawaida kwa sababu
wanaweza kusambaza magonjwa kwa
wengine. Toa chanjo mara kwa mara
kulingana na ushauri wa watoaji chanjo na
madaktari wa wanyama wa nyumbani.
Vifaranga wachanga wanapaswa kuchanjwa
dhidi ya magonjwa ya kawaida ya
kuambukizana wakifika umri wa wiki 2-3.
Ikiwa kuku watataabika kutoka kwa
ugonjwa sugu unapaswa:
• Kuita daktari wa wanyama
• Kumwtenga kutoka kwa wengine
• kuku anafaa kuuliwa mara moja kwa
kutegemea jinsi ugonjwa ulivyo mzito na
• Anafaa kuchomwa ama kuzikwa katika
kina kirefu ili kuzuia mbwa na wanyama
wengine kuwachimba na kusambaza
ugonjwa.
Angalia ni kuku wagani wana dalili za
kutaka kuangua mara moja kwa mwezi na
uwapatie matunzo ya ziada
Toa maoni yako....