06/03/2022
KITENGO: FEYOSTAR GLORY OF THE LORDE ARISED ON WORLD (GLA WORLD)
MAADA: PALE ULIPOWEKA USO WAKO NDIPO KUNA NGUVU YA MUNGU
Unaposogelea uso wa Bwana Maana yake ni hali ya kupokea ulinzi na baraka zake KWA Maana MUNGU anafanya kukushika mkono KWA macho yako ya nyama hauto ona lakini KATIKA macho ya rohoni ni kuinuliwa kwako KWA sababu mkono wake JUU y'ako ni ushuhuda tosha AYUBU 16:8-10"Umenishika Sana ni ushahidi JUU yangu, Na kukonda kwangu kwaniinukia,kwanishuhudia usoni pangu, Amenirarua KATIKA ghadhabu zake na kunionea Amesaga saga meno JUU yangu mtesi wangu hunikazia macho makali
Kunawakati watesi wako wanakuwinda usiku na mchana kutaka kuku angamiza Jambo la kufanya ni kuhutazama tu Uso wa Mungu ndani ya moyo wako usishindane na wanadamu KWA sababu ya wanadamu ni batiri lakini ya MUNGU ni hai na Yana Mwanga KATIKA maisha yako AYUBU 22:21"Mjue Sana MUNGU Ili uwe na amani ndivyo mema y'ako yatakavyokuijia" MUNGU unapomjua na yeye atakujua na atakuonyesha kazi inayokupasa kuifanya KATIKA maisha ya kumtegemea MUNGU na maisha ya kimwili pia"
MUNGU anapokuwa upande wako hutotikisika kamwe MATENDO 2:25-27 "Maana Daudi ataja habari zake nalimwona Bwana mbele yangu Siku zote KWA KUWA Yuko upande wa mkono wangu wa kuume nisitikisike KWA hiyo moyo wangu ukapendezwa ulimi wangu ukafurahi,Tena mwili wangu nao utakaa KATIKA matumaini"
Maana yake tumaini lako linabebwa na imani y'ako ndiyo itakayo kufanya ucheke na ufurahi KWA sababu mkono wa MUNGU uko JUU yako ZEKARIA 9:14-15 "Naye Bwana ataonekana JUU yao, Na mshale wake utatoka k**a umeme, Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta, Naye atakwenda KWA pepo za kisulisuli za kusini , Bwana wa majeshi atawalinda,Nao watakula na kuyakanyaga mawe ya teo, Nao watakunywa na kufanya kelele k**a KWA divai, Nao watajazwa k**a mabakuli, k**a pembe za madhabau
Hii ni faida ya kukaa jirani ya uso wa Mungu "Fuata Nyota YAKO ya kukalibia uso wa Mungu timiza ndoto zako zenye tumaini jema "
FEYOSTAR