11/05/2023
MAMBO KUMI MUHIMU KATIKA UFUGAJI WA KUKU WA KISASA :
1. BANDA BORA:
Banda liwe na sifa zifuatazo: Liweze kupitisha mwanga hewa ya kutosha na vilevile liwe na kinga ya upepo mkali, mvua ya upepo na jua. Banda hili pia lapaswa kujengwa mahali ambapo hapatuamishi maji, panapoweza kufikika kirahisi na mfugaji wakati wa uangalizi, liwe
mbali na mabanda mengine ya kuku na pia liwe mbali na barabara na shughuli zenye kelele nyingi ili kuepuka usumbufu kwa kuku.
2. KUCHAGUA VIFARANGA BORA:
Ni muhimu kwa mfugaji kufahamu mahali pa kupata vifaranga bora wa mayai au nyama. Ni vyema mfugaji akanunua vifaranga kutoka vyanzo vilivyothibitishwa k**a vile Farmers Centre Chicks, Amadori na wengineo. Epuka kununua vifaranga toka vyanzo visivyokuwa vya uhakika ili kuepuka athari mbalimbali wakati ukifuga kuku hawa. Vifaranga bora ni vile vyenye nguvu, visiwe na vilema au magonjwa ya kuambukizwa. Vilevile ni muhimu kuhakikisha kuwa vifaranga hawa wamepewa chanjo dhidi ya magonjwa k**a Mahepe (Marek’s) n.k
3. JOTO LA KUTOSHA:
Joto la wastani ni muhimu sana katika uhai wa kuku, katika juma la kwanza joto linalostahili ni nyuzijoto 35oC na hupimwa kwa kipima joto na kiasi hiki cha joto kipunguzwe kwa nyuzijoto mbili kila juma hadi kufikia nyuzijoto 27oC katika juma la nne. Pamoja na kupima joto unashauriwa uangalie tabia na mwenendo wa vifaranga. K**a vifaranga vikichangamka na kunywa maji vizuri na kutawanyika sehemu zote joto hilo linatosha. Ikiwa joto halitoshi hujikusanya karibu na taa au hujirundika sehemu moja, hivyo unashauriwa kuongeza joto kwa kuongeza idadi ya vifaa au nguvu ya joto kwa mfano taa za umeme. Joto likizidi utaona vifaranga vinakaa mbali na taa vikipanua mabawa yao na kuhema haraka haraka. Hali hii ikizidi husababisha ugonjwa wa joto jingi (heat stroke) na hupelekea vifaranga kuamguka chini.
HALI YA HEWA NA MATOKEO YAKE
4. ULEAJI MZURI WA VIFARANGA:
Mara baada ya vifaranga kuwasili bandani, vikaguliwe vihesabiwe, na kisha viwekwe kwenye sehemu maalum ya kulelea (Brooder). Kisha vipewe maji safi ya uvuguvugu yenye dawa za viubakteria (Antibiotics) k**a vile OTC Plus, Neoxyvital na glucose.
Baada ya wiki nane kuku wawekwe kwa mujibu wa idadi katika banda, kwa mfano:
• Kuku wa nyama wawekwe 9 hadi 10 kwa mita moja mraba.
• Kuku wa mayai wawekwe 5 kwa mita moja mraba.
• Kuku wa mbegu (Parent stock) kuku 3.5 hadi 4.5 kwa mita mraba.
Nafasi katika banda huwafanya kukua haraka, kutaga vizuri na kwa pamoja.
5. MAJI SAFI
Pamoja na chakula hakikisha kuku wako wanapata maji safi na ya kutosha kila siku. Maji safi ni muhimu kwa vile maji yasiyo salama ni njia kuu ya isababishayo magonjwa. Maji husaidia kuyeyusha na kusafi risha chakula mwilini, kutengeneza mayai na kupunguza joto mwilini.
MANYWESHEO
6. CHAKULA:
Chakula hiki hutengenezwa kwa kuzingati a utaalamu wa lishe ya kuku, kwa mfano chakula cha vifaranga huwa laini na proti ni nyingi, chakula cha kuku wakubwa huwa cha chenga na nguvu ya joto zaidi, vilevile, itabidi izingati we kwamba kuku wa mayai asilishwe chakula cha kuku wa nyama kwani atanenepa na kushindwa kutaga. Aidha umri wa utagaji hasa kwa kuku wa mayai na upatikanaji wa aina za nafaka na mashudu yatokanayo na mbegu za mafuta ni muhimu kuzingati wa wakati wa ulishaji au utayarishaji wa chakula cha kuku.
MALISHIO
Wakati ukiwalisha kuku wako, unaweza kutumia malishio (Feeder) za kisasa au vihori ambazo hutengenezwa kwa mbao na vijazwe chakula kufi kia theluthi mbili kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa kuku wanakuwa vizuri na kwa pamoja (uniform growth) ni muhimu kuhakikisha kwamba vifaranga wote wanapata nafasi ya kula chakula cha kutosha kila mara.Chakula hiki kiwe kimechanganywa na dawa ya kuzuia magonjwa k**a vile coccidiosis, (Ridocox/Salcox) salmonellosis(Colirid) kati ka kiwango kinachotakiwa.
VICHANGANYIO KATIKA CHAKULA
7. USAFI WA BANDA:
Hakikisha banda lako linasafi shwa na dawa za kuulia vimelea kwa mfano V-RID kila kabla na baada ya kuweka kuku, hii inasaidia kukinga kuku wako na magonjwa yanayoambukiza k**a Marek’s, Gumboro, Koksidiosis (Kikoti ) na kuharisha (Salmonellosis). Vyombo vya chakula, maji pia vioshwe kwa V-RID. Madirisha, milango, waya, kuta na kila kitu kioshwe kwa dawa ya V-RID. Pia Vyombo visafi she na maji na kubadilishwa mara mbili kwa siku.
8. KINGA ZA MAGONJWA:
Ni vema kuhakikisha kwamba kuku wanapati wa chanjo za kuzuia magonjwa mbalimbali k**a Newcastle, Gumboro, Marek’s. wakiwa na umri kuanzia wanapozaliwa hadi wiki ya tatu. Kinga hizi lazima zihifadhiwe na zitumiwe k**a inavyoshauriwa na wataalamu. Mfano wa dawa za kinga zinazoshauriwa kitaalamu ni k**a Thermostable 1, Newcasle lasota, Gumboro, Ndui na nyinginezo.
9. KUKINGA MAGONJWA SUGU
Magonjwa sugu ambayo huuwa au kudumaza kuku katika umri wote ni k**a
(a) Coccidiosis – Inakingwa kwa kuweka dawa mfano RIDOCOX au SALCOX kwenye chakula na inatibiwa na Amprolium na dawa za jamii ya SALFA.
(b) SALMONELLOSIS na E. coli Infections: Hukingwa kwa kutumia kiua bakteria k**a FARMACID Premix au COLIRID katika chakula. Tiba ni kutumia FLUBAN au DOXYCOL
(c) Mafua – Chronic Respiratory diseases, Infectious coryza na mengineyo.
Jitahidi kuzua vumbi katika mabanda,
Tumia TYLOFARM Premix au ANFLOX Feed Premix katika chakula.
(d) Sumu ya fangasi katika chakula:
Sumu hii ina athari kubwa k**a vile kuharisha, inadumaza na kuua. Inaweza kukingwa kwa kutumia MYCOBIND Katika Chakula.
10. FUATA KANUNI ZA UFUGAJI BORA:
Ni muhimu kwa mfugaji kuwa na uelewa wa kutosha wa kanuni za ufugaji bora ili aweze kupata matokeo mazuri. Baadhi ya kanuni hizi ni k**a vile,
• Kuwalea vifaranga vizuri
• Uelewa wa kuyatambua na namna ya kuyadhibiti magonjwa mbalimbali,
• Namna ya kutumia kinga na madawa kwa kiwango na wakati sahihi,
• Vyakula vinavyofaa kwa aina na umri wa kuku na
• Usafi wa banda lake.
Iwapo mfugaji atazingatia kanuni hizi k**a inavyoshauriwa kitaalamu basi hakuna shaka ya kutopata matokeo anayotarajia.
KWA MSAADA ZAIDI
TEMBELEA KURASA HIZI ZA KUKUSHOP. COM