28/04/2026
SALAM ZA POLE kutoka kwa wananchi,π
Uongozi wa Young Africans SC umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu yetu na mwigizaji mkongwe wa filamu nchini, Hashim Kambi.
Tunatoa pole za dhati kwa familia ya marehemu, Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), wadau wa mpira wa miguu, Shirikisho la Filamu Tanzania, wasanii wa filamu, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu.
Inna lillahi wa inna ilayhi rajiβun.
R I P