Joo_Tz

Joo_Tz Joo Tz(Baba Jayden)
Proffessional;Movie director & video,Actor FROM MBEYA TZ.
+255745327319

19/10/2025

ILIPOISHIA JUMATATU ..

Kwa mara ya kwanza Suma alijishangaa kugundua kitu cha ajabu sana. Pamoja na mapenzi yake yote juu ya viumbe hao, siku hiyo Suma alimuogopa!

“Nimekuuliza wewe ni nani?”

“Mimi ni jini Suma.”

“Jini?”



“Ndiyo…tena naamini nimekuja muda mwafaka. Nina mazungumzo kidogo na wewe k**a kweli unapenda majini k**a ninavyokuona ukihangaika,” akasema yule msichana aliyejitambulisha kuwa ni jini ak**eti kitandani.

Suma akazidi kuogopa!

SASA ENDELEA…

HOFU iliutawala moyo wa Suma, alipata wakati mgumu kidogo wa kutafakari japo kwa sekunde tatu tu. Alitaka kujiridhisha kwamba aliyekuwa mbele yake alikuwa jini kweli au lah!

Lakini hata k**a alikuwa jini kweli, bado alikuwa na mambo mengine ya kujiuliza.
Kwa nini awe mwoga leo kwa majini? Si ni yeye ndiye aliyeweka manukato makali na udi kwa ajili ya kuwaita?

“Ni nini hiki?” akajiuliza.
“Ni jini Suma,” yule msichana akamjibu.
Akashangazwa na kitu kingine kipya; yule msichana aliyesema ni jini alimjibu swali ambalo alijiuliza mwenyewe kichwani mwake, tena bila kutoa sauti.

Amesikiaje?

“Sawa tufanye ni jini, sasa kwa nini namuogopa?” akawaza tena.
“Hata mimi nakushangaa kwa hilo!” yule jini akamjibu.
Suma akatetemeka!

Kwa asilimia mia moja sasa aliamini aliyekuwa chumbani mwake alikuwa ni jini. Hilo hakuwa na shaka nalo hata kidogo. Ni kweli Suma alikuwa chumbani kwake.

Woga wake ukamfanya atake kurudi nyuma zaidi lakini haikuwezekana maana tayari alikuwa ameshafika ukutani.
“Suma!” yule jini akaita.
“Mmmmh!” Suma akaitika kwa kuguna.

“Napenda kusikia sauti yako, ingawa nimeshaisikia mara nyingi kabla.”
“Wewe ni nani kwani?” Suma akauliza baada ya kujikaza kidogo.
“Mimi ni jini.”

“Najua ni jini…unaitwa nani na unataka nini?”
“Suma acha hizo bwana, mimi nimekuja hapa kwa ajili yako maana wewe ndiye unayehitaji msaada wangu na si mimi kutaka msaada kutoka kwako. Kwa maneno mengine, ni sahihi zaidi mimi kuuliza nikusaidie nini?”

Suma akahema kwa kasi.
“Pole sana Suma.”
“Mh! Kazi ipo leo!” akawaza.
“Tena kubwa sana,” yule jini akamjibu.
“Sawa, sasa naanza kukuelewa lakini napenda kujua jina lako k**a wewe unavyofahamu langu.”
“Naitwa Zukhaiya.”

“Zakhia?” akauliza kwa mshtuko kidogo.
Alimkumbuka Zakhia wake.
“Siyo Zakhia, nimesema Zukhaiya.”
“Sawa, kwanza umeingiaje humu ndani kwangu?”
“Achana na maswali ya kitoto. Twende kwenye hoja ya msingi, wewe si unataka kuoa jini?”

“Ndiyo.”
“Kwa nini jini na si binadamu?”
“Mambo mawili makubwa nahitaji; kwanza penzi la dhati lakini pia mali. Familia yangu ni duni sana.”
“Najua.”

“Nataka kuwasaidia wazazi wangu watoke kwenye umasikini, pia nami niishi maisha yasiyo na shida.”
“Umenena vyema.”
“Je, ni wewe?” Suma akauliza kwa shauku.
“Nani?”
“Nitakayekuoa?”

“Hapana.”
“Sasa kwa nini umekuja?”
“Nimesikia uhitaji wako. Nitakusaidia lakini kwa masharti.”
“Sawa, nipo tayari.”

Zukhaiya akasimama pale kitandani, akamwangalia Suma kwa macho yanayobadilikabadilika rangi kila baada ya muda mfupi. Akatabasamu kisha akainama kidogo na kuketi tena kitandani.
Ghafla akasogeza mdomo wake hadi ulipogusana na wa Suma.

Akamwangushia busu mwanana. Suma akashtuka. Zukhaiya akarudi nyuma kidogo kisha akambusu tena katika shavu la kushoto na baadaye la kulia.
Zukhaiya akamgeuzia mgongo Suma na kumtaka amfungue zipu ya gauni lake iliyokuwa mgongoni. Suma akashtuka!

“Lakini ulisema siyo wewe.”
“Nifungue zipu,” Zukhaiya akasema kwa sauti ya kuamrisha.
Suma akafanya hivyo.
“Nataka unifurahishe kimapenzi…” Zukhaiya akasema kwa sauti laini, harufu nzuri ikitawala katika chumba kile…
“Mh!”

“Tafadhali.”
“Sawa.”
Kazi kubwa ikafanyika. Kwa Suma kulikuwa na ugumu kidogo mwanzoni lakini baada ya muda akashangaa ametulia na kumzoea Zukhaiya. Zoezi hilo likakamilika kwa ukamilifu wake.
“Hapo sawa, umefanya vizuri sana.”
“Ahsante Zukhaiya.”

“Umemaliza jambo la kwanza…sasa tunaweza kufanya makubaliano.”
“Makubaliano gani tena?”
“Lazima tuingie mkataba.”
“Mkataba?”
“Ndiyo…mkataba tena wa siri.”
“Kwa nini siri?”

“Hutakiwi kumwambia mtu yeyote juu ya mkataba wetu. Mimi nipo hapa k**a wakala.”
“Ni upi?”
“Nitakupa maelekezo, kwa sasa acha niondoke, kesho nitakuja tena,” akasema Zukhaiya akisimama na kuelekea mlangoni.

Suma akamwita lakini Zukhaiya hakugeuza shingo. Alitegemea kumuona Zukhaiya akifungua mlango na kuondoka lakini jambo hilo halikutokea…
Alitoweka!
Ilikuwa ghafla sana!
*

MBEZI BEACH, DAR
Uso wa Suma ulikuwa umechakazwa na machozi k**a maji usoni mwake. Ustaadh Alii alimwangalia kwa huruma Suma. Alijua ni kwa namna gani kumbukumbu zile zilimtesa, hasa katika kipindi kigumu k**a hiki ambacho anateseka kuliko kawaida.

“Suma jikaze, mimi na wenzangu tupo hapa kukusaidia. Sikia nikuambie, Allah hajawahi kushindwa hata siku moja. Kuwa huru, dua zetu zitajibu. Hebu niambie kilitokea nini baadaye?” Ustaadhi Alii akauliza.

“Acha tu Ustaadhi, sasa naanza kupata picha. Sijui k**a naweza kuishi kwa amani tena.”
“Utaweza mwanangu, Allah anajua zaidi. Atakusaidia, tafadhali endelea kutueleza.”

“Basi baada ya hayo ya usiku ule, asubuhi nilikutana na kitu cha ajabu sana…” akasema Suma akiangalia juu, machozi yakishindwa kuacha kuuchafua uso wake.
*
Bado harufu ya mchanganyiko wa manukato iliendelea kupenye katika pua za Suma. Kwa kiasi fulani sasa alihisi kupaliwa! Akakohoa kwa nguvu kiasi kwamba alihisi mbavu zake zikichezacheza!
Akashtuka!

Moshi ulikuwa umejaa chumbani mwake lakini giza totoro nalo likichukua nafasi kubwa chumbani mwake. Jasho jingi lilikuwa likimtoka mwilini mwake.
Hapohapo akapata kumbukumbu mpya! Alimkumbuka Zukhaiya ambaye alikuwa naye chumbani hapo muda mfupi uliopita. Alisimama ghafla na kusogea mpaka mlangoni.
Mlango ulikuwa umefungwa!

Ni kweli muda mfupi uliopita alikuwa na jini aliyejitambulisha kwa jina la Zukhaiya, mara akamwambia anaondoka na alipofika mlangoni akatoweka ghafla.
“Mh!” akaguna Suma
“Alikuja kweli humu chumbani?” akawaza tena.

Suma akagundua kitu kipya. Pamoja na kwamba alikuwa akihisi kwamba alikuwa kwenye ndoto, sasa alianza kuwa na uhakika kuwa kweli jini Zukhaiya alikwenda chumbani mwake.
Alikuwa na dalili zote kuwa alikutana kimwili muda mfupi uliopita. Mazingira yote yalithibitisha hivyo.
“Kwahiyo nimefanya mapenzi na jini?” akawaza tena.

Taratibu akarudi kitandani na kuketi. Akakumbuka kitu. Alisimama haraka na kusogea kwenye swichi ya ukutani kisha akawaza taa. Akasogea kwenye meza ndogo ya kujipambia na kujitazama kwenye kioo.
Ndiyo…mashavu yake yote mawili yalikuwa na alama ya mdomo wa mwanamke aliyepaka rangi maalumu ya mdomo, wenyewe wanaita lip stick. Ni alama hiyo ndiyo iliyomthibitishia pasipo shaka kuwa kweli alikuwa na Zukhaiya ndani ya chumba chake.
Wazo lingine likauvamia moyo wake alikumbuka neno moja tu, kubwa na muhimu zaidi kwa muda wote aliozungumza na Zukhaiya;

MKATABA!
“Siyo mimi nitakayekuwa na wewe Suma, nipo hapa kuwawakilisha wenzangu lakini ni lazima tuingie mkataba,” akakumbuka maneno ya jini Zukhaiya.
“Mkataba?” swali hili aliliuliza yeye na alilikumbuka barabara.
“Ndiyo tena mkataba wa siri.”

“MKATABA?!!!” Akawaza sasa Suma.
“Ni mkataba gani sasa na alimaanisha nini aliposema tunatakiwa kuingia mkataba?” anazidi kuwaza.
Akiwa katika mawazo hayo, macho yake yakatua kwenye saa iliyokuwa ukutani. Mshale wa saa uligota kwenye mbili na wa sekunde ulikuwa umesimama kwenye 16.

Yes ilikuwa saa 8:16 usiku!
“Ni usiku sana saa hizi,” akawaza tena.
Aliutamani sana utajiri, lakini kwa mara ya kwanza alianza kuhisi kuwa na wasiwasi na uamuzi wake.

“Lakini bado nina nia ya kupata utajiri, sitakiwi kurudi nyuma katika wazo langu hili,” akawaza mwenyewe.
Ni muda huo ndipo alipoamua kuvuta shuka na kulala. Haikuwa kulala hasa kwa maana ya kulala bali alijilaza! Alisaka usingizi kwa muda mrefu sana lakini wapi!
Ataupata wapi?
Anamuwaza Zukhaiya.

12/10/2025

ILIPOISHIA IJUMAA

“Vipi kwani?”

“Yule matawi ya juu sana, nimeshangaa kuona mnafahamiana tena mna ukaribu.”

“Kawaida tu, yupo lakini?”

“Kwani yeye amekuelekeza lini hapa?”

“Muda kidogo, ni k**a miezi minne hivi imepita.”

“Ni kweli alikuwa anaishi hapa…”

“Na sasa?”



“Amehama.”

“Amehamia wapi?”

“Soweto.”

“Dah….sijui itakuwaje sasa?” akasema kwa sauti Suma.

“Vipi ni muhimu sana kuonana naye?”

“Sana tena sana yaani.”

“Pole sana, unajua anapofanyia kazi?”

“Hapana.”

“Nitakusaidia, labda hapo unaweza kumpata.”

“Nitashukuru sana ndugu yangu.”

“Anafanya kazi Benki ya CRDB.”



“Wapi?”

“Ile iliyopo kwenye round about. Jengo la Kahawa.”

“Ahsante sana kaka, utakuwa umenisaidia sana. Ngoja nitajaribu kwenda kumwulizia pale.”

“Poa bwana.”

Suma akaondoka zake.

ENDELEA SASA…



HAKWENDA kazini. Alitaka kumpata kwanza Zakhia. Alichojua yeye ni kwamba Zakhia anafanya kazi Benki ya CRDB tu. Si zaidi ya hapo. Mawazo tele yalikuwa kichwani mwake wakati akifikiria namna ya kumpata huyo Zakhia.

Alijua wazi kwamba benki hiyo ni kubwa na kuna idara nyingi, hivyo isingekuwa rahisi kwake kufahamu moja kwa moja yupo idara gani, jambo ambalo kwa kiasi fulani lilimkatisha tamaa.



“Lakini nikiulizia watakuwa wanamjua tu…..tatizo ni k**a kuna Zakhia mwingine hapo…hata akiwepo ni rahisi kumwelezea huyu ninayejua jinsi alivyo. Watakuwa wanamfahamu tu.

“Nitajua la kufanya. Mimi si mgeni hapa mjini na sidhani k**a nitashindwa kujieleza kwa kiwango hicho. Nitampata tu Zakhia,” aliwaza kichwani mwake akiwa ndani ya daladala asubuhi hiyo wakati likishusha abiria katika kituo cha YMCA.



Alishukia KNCU, kisha akatembea kwa miguu taratibu jirani na Benki ya NBC, akapita katikati ya mzunguko wa mnara wa saa kisha akachepuka kidogo na kurudi kwenye Jengo la Kahawa. Alipita getini kulipokuwa na askari wawili wenye bunduki mikononi mwao.

Akaingia moja kwa moja ndani ya Benki ya CRDB. Pamoja na kwamba ilikuwa ndiyo kwanza saa 3 asubuhi, alikuta ndani ya benki hiyo kumefurika watu wengi. Wengine wakiwa wamekwenda kuhifadhi fedha huku wakiwemo waliokwenda kuchukua.



“Customer Care…” Suma alisoma maneno hayo kwenye bango dogo juu ya meza iliyokuwa na wahudumu watatu; mmoja kati yao mwanaume.

“Huyu mwanaume hawezi kunisaidia, huenda labda naye anamtaka akanikosesha bure,”akawaza Suma huku akimsogelea mhudumu mmoja wa k**e, akiwa amepamba uso wake kwa tabasamu mwanana kabisa.



“Habari yako sister?” Suma akasalimia.

“Njema kabisa kaka, karibu sana.”

“Ahsante.”

“Tafadhali naomba nikusaidie.”



“Ahsante sana…samahani sana, nina shida muhimu nje ya kazi.”

“Unaweza kunieleza tafadhali.”

“Mimi naitwa Suma, ni ndugu yake na Zakhia. Najua anafanya kazi hapa, lakini sifahamu ni kitengo gani. Tafadhali dada naomba unisaidie nionane naye k**a unamfahamu!”



“Zakhia?”

“Ndiyo.”

“Pole sana!”

Moyo wa Suma ukapiga kwa nguvu puuuu!



“Pole sana!” maneno hayo yakajirudia ubongoni mwake.

Alisahau kila kitu na kuanza kutafakari neno ‘pole sana’. Alishindwa kuelewa ni kwa nini alipewa pole.

Hofu ikauvaa moyo wake, picha aliyoiona mbele yake ni jeneza la Zakhia na watu wakiimwimbia huku wakimsindikiza. Uso wa dada aliyekuwa akizungumza naye ndiyo kishawishi cha fikra zote hizo. Maumivu makali yakautawala moyo wake.



“Iwe na maana yoyote ile lakini isiwe akawa amekufa…hilo tu ndiyo wasiwasi wangu na nisingependa kabisa litokee,” akawaza kichwani mwake.

Yule dada alitulia kwa muda, naye alikuwa katika kutafakari wakati akimwangalia Suma namna alivyoshangazwa na jibu lake. Alishajua alichokuwa akiwaza…



“Kwani kaka wewe unatokea wapi?”

“Nadhani hilo si la muhimu sana kwa sasa, kabla hujanieleza nini kimempata ndugu yangu.”

K**a ni kutunga uongo, Suma aliweza. Zakhia si ndugu yake bali ni mwanamke ambaye alionekana kumpenda na sasa ameamua kumfuatilia ili awe wake mke wake wa ndoa.



Akili yake haikutulia kabisa, kuna wakati alijaribu kubashiri kitu alichotaka kuelezwa na msichana aliyekuwa mbele yake. Alikuwa tayari kuambiwa chochote lakini si taarifa ya kifo.

“Tafadhali naomba uniambie, nini kimempata Zakhia?”

“Zakhia amehamishwa. Amehamia Dar es Salaam, Tawi la Vijana.”

Suma akajikuna kidevu.



Kwa hakika kidevu chake kilikuwa hakiwashi ila alilazimika kufanya hivyo. Kichwa kiliwaka moto. Ndoto zake ziliyeyuka kabisa. Alimwangalia yule dada aliyekuwa akimsikiliza kwa makini. Alitafakari jambo lingine la kumwuliza ili aweze kumsaidia.

“Dada utanisaidiaje ndugu yako?”

“Pole sana, maana ingekuwa rahisi kukupatia namba zake za simu ila sina. Wewe una simu?”



“Hapana.”

“Si unaona? Ni vigumu kukusaidia lakini k**a una shida ya muhimu nakushauri nenda Dar es Salaam. Ni rahisi kufika, hilo tawi lipo eneo la Mtaa wa Lumumba, Mnazi Mmoja. Ukimwulizia pale utampata.”

“Sawa yupo idara gani?”



“Nimesikia kwamba yupo Utawala sasa hivi lakini sijui ana nafasi gani.”

“Sawa.”

Suma alitoka nje ya benki akiwa na mawazo tele. Hakutaka kwenda kazini tena. Akarudi nyumbani kwake Majengo. Haikuwa tatizo sana kutokwenda kazini siku hiyo maana alilipwa kutokana na namna anavyofanya kazi na siyo mshahara!

***



Ni siku ya nne leo anaendelea na mateso ya fikra. Suma bado hajapata uamuzi wa nini afanye. Mawazo tele yalimwandama. Hakutaka kuwaudhi wazazi wake kuhusu suala la kuoa lakini wazo lake hasa lilikuwa kuoa jini!

Potelea mbali ameamua kuoa binadamu lakini si mwingine zaidi ya Zakhia. Kitu kilichomsumbua ni eneo ambalo angeweza kumpata Zakhia.

Dar es Salaam.

Tangu kuzaliwa kwake hakuwahi kukanyaga ardhi ya Dar es Salaam, vipi angefikaje? Nani angekuwa mwenyeji wake? Nani angemkutanisha na Zakhia?

Hilo ndilo lililomtesa. Kwa lengo la kupoteza mawazo akaamua kwenda kwenye kibanda cha video kwa lengo la kupoteza mawazo na kujipa amani ya moyo wake. Naam! Sasa ameketi kwenye benchi akiangalia Sinema ya Power of Love in Hidden World (Nguvu ya Mapenzi Katika Ulimwengu Usioonekana).



Filamu hii sasa inaharibu ubongo wake. Hatua aliyopiga angalau ya kumkubali binadamu Zakhia inaanza kurudi nyuma. Hadithi ya filamu hii inamteka. Anamwona mwanaume fukara ambaye anabadilika na kuishi maisha ya furaha akimiliki fedha nyingi.

Hakupata mahali pengine popote zaidi ya msaada wa jini. Kijana huyo ambaye umri wake ulikaribia kufikia miaka 30 alionekana kung’arishwa sana na fedha za mpenzi wake jini aliyeitwa Zulfa.

Suma akatamani kuwa yeye!



“Nipo tayari kuachiwa laana, lakini mimi lazima nioe jini. Simtaki tena hata huyo Zakhia. Kazi iliyobakia sasa ni kutafuta mambo ambayo majini wanavutiwa nayo halafu nawatega. Nitampata tu!” akajisemea wakati akiendelea kuangalia sinema hiyo.

K**a ni kutekwa, Suma alikuwa ametekwa kihisia hasa. Mawazo ya Zakhia yalifia hapo. Sasa akawa na lengo moja tu; kuoa jini.

Tayari alikuwa na mbinu mpya. Kwa kuwa ndiyo aliokuwa akiwahitaji katika maisha yake, alifanya juhudi za ziada ili kugundua majini wanapenda nini. Alijihakikishia kwamba lazima angemnasa mmojawapo.

Hilo tu!

***



Suma hakuwa na muda wa kupoteza. Mkakati ulianza kutekelezwa haraka iwezekanavyo. Alikwenda kwenye duka la vipodozi na kununua perfume aina tatu kisha akaenda kwenye duka la dawa za asili na kununua marashi mengine ya aina mbalimbali na udi.

Tayari alikuwa na vifaa vya kazi. Suma alidhamiria kabisa kuwatega majini. Kwa maelezo aliyopata na jinsi alivyojifunza kupitia sinema za majini, viumbe hao walivutiwa sana na marashi ya aina mbalimbali.

Kuna nini tena?



“Tayari nina zana za kazi, wasiwasi wa nini? Watanasa tu. Suma akasema akitabasamu akiwa chumbani mwake.

Ni saa 5:45 usiku!

Saa sita kasoro!

***



Harufu kali ya udi ilizisumbua pua zake, kwa namna fulani Suma alihisi k**a anapaliwa hivi. Udi nne zenye manukato tofauti zilikuwa zikifuka moshi kila upande wa chumba chake.

Muda kidogo aliona kivuli mlangoni mwake. Suma akapekecha macho ili kuangalia vizuri. Ghafla kile kivuli kilibadilika, akamuona msichana amesimama mbele yake. Kwa uzoefu wake alioupata kwa kuangalia filamu za majini, hakuchukua muda mrefu kugundua kwamba aliyekuwa amesimama mlangoni mwake alikuwa ni jini!



“Wewe ni nani na umeingiaje chumbani kwangu wakati mlango wangu niliufunga?” Suma akamwuliza msichana aliyekuwa amesimama mbele yake.

Alikuwa msichana mrembo sana, mweupe, mrefu na mwembamba kiasi lakini mwenye umbo linalofanana na tarakimu namba nane. Hakuwa na cha kumjibu zaidi ya kutembea taratibu akimfuata pale kitandani.



Kwa mara ya kwanza Suma alijishangaa kugundua kitu cha ajabu sana. Pamoja na mapenzi yake yote juu ya viumbe hao, siku hiyo Suma alimuogopa!

“Nimekuuliza wewe ni nani?”

“Mimi ni jini Suma.”

“Jini?”



“Ndiyo…tena naamini nimekuja muda mwafaka. Nina mazungumzo kidogo na wewe k**a kweli unapenda majini k**a ninavyokuona ukihangaika,” akasema yule msichana aliyejitambulisha kuwa ni jini ak**eti kitandani.

Suma akazidi kuogopa!

12/10/2025

ILIPOISHIA JUMATANO

“Sina uhakika na hili jambo.”

“Usinitaje, mimi nimekuambia tu k**a shoga yangu. Sisi wote ni wazazi.”

“Sawa.”

“Lakini jambo lingine linalowashtua zaidi watu ni tabia yake ya kujipenda kupita kiasi. Muda wote msafi, ananukia marashi, ananyoa vizuri, anavaa nguo nzuri…kwanini ajipende hivyo k**a mtoto wa k**e? Mchunguze mwanao shoga yangu!”

SASA ENDELEA….



MAMA Suma alikuwa kimya kabisa, hakuwa na la kujibu, tayari walikuwa wameshaingia mtaani kwao. Mama Mwaija akaagana na mama Suma ambaye nyumbani kwake ilikuwa mtaa wa pili.

***

Siku nzima mama Suma alishinda na mawazo. Maneno aliyoambiwa na mama Mwaija yalimuumiza sana. Hayakuwa mambo mapya kwake, ila alishtuka baada ya kugundua kwamba kumbe yanajulikana na watu walishaanza kuyajadili!



Hata yeye mwenyewe alikuwa na mawazo sana juu ya tabia ya mwanaye kujipenda kupita kiasi. Jambo lingine lililomtesa ni kutokana na tabia yake ya kutopenda kabisa kuwa karibu na wanawake.

“Mwanangu jamani, hivi inawezekana ni kweli anafanya huo mchezo?” akawaza mama Suma.

“Lakini ngoja nitazungumza na baba yake, lazima nitafute ukweli wa hili jambo, ni aibu sana kwa familia yangu,” akaendelea kuwaza.



Jioni mumewe alivyorejea kutoka kazini, jambo la kwanza kuzungumza naye lilikuwa ni juu ya Suma.

“Kuna nini tena mke wangu?”

“Zungumza na mtoto, Suma anapotea.”

“Kivipi? Bado una yale mambo tu?”

“Siyo ninayo? Hata mtaani sasa wameanza kuyazungumza.”

“Mtaani?”

“Ndiyo.”

“Kivipi?”



Mama Suma akamsimulia mumewe kila kitu jinsi alivyozungumza na mama Mwaija. Baba Suma alishtuka sana, hakutegemea k**a mwanaye angekuwa akisemwa hivyo mitaani.

“Ngoja nitakwenda kuzungumza naye.”

“Ndiyo maana alivyoamua kujitegemea amekwenda kupanga Majengo, hataki kukaa hapa mtaani kwa sababu wameshajua tabia yake.”

“Mke wangu acha kumhukumu mtoto kabla hujawa na uhakika, Jumapili nitakwenda kwake, nitajua huko huko.”



“Rajabu ameshaoa, Elibariki ana mchumba, Meshack ndoa yake ilikuwa Jumamosi iliyopita, wote hawa amemaliza nao shule, mbona yeye hana hata mtoto wa kusingiziwa mitaani? Lazima kuna kitu,” akasisitiza mama Suma.

“Nimesema nipe muda nikazungumze naye, ukweli utajulikana mke wangu,” akasema baba Suma.

“Sawa.”

***



Alichelewa sana kutoka kazini siku hiyo, tayari ilikuwa imeshatimu saa moja na dakika zake za jioni. Alikuwa amechoka sana lakini pia alikuwa na hamu ya kujua mengi zaidi kuhusu majini.

Alikuwa amesimama kwenye duka maarufu la viatu mjini Moshi liitwalo Bora, akakumbuka kwamba katika jengo lilelile kuna ukumbi wa sinema wa Plaza. Asingeweza kwenda hadi Majengo akawahi kuangalia kwenye vibanda vya mitaani wakati ukumbi ulikuwa pale pale.

“Tatizo watakuwa na hiyo filamu?” akawaza.

“Ngoja nijaribu,” akajisemea.



Akapandisha juu haraka, ambapo alipita mbele ya duka la vifaa vya ujenzi la Njiwa Hardware, akapanda hadi kwenye ubao wa matangazo ya filamu katika Ukumbi wa Plaza Cinema.

Saa 12:00 jioni – Game in Forest (Billy Blanks)

Saa 2:00 usiku – Vampire’s With True Love (Sarafina Hollins)

Saa 4:00 – Shamba Kubwa – Kiswahili (Mzimuni Theatre Group)



Wengi walikuwa wakifurahia sana kuona kwamba kuna Filamu ya Shamba Kubwa ambayo ni ya Kiswahili. Ilikuwa filamu ya kwanza ya Kiswahili kuoneshwa katika ukumbi huo. Ingawa ratiba ilionesha kwamba ingeoneshwa saa 4:00 usiku, walikuwa tayari kusubiri!

Kwa Suma ilikuwa tofauti kabisa, alirukaruka juu kwa furaha alipoona Filamu ya Saa 2:00 usiku – Vampire’s With True Love, pamoja na elimu yake ya kawaida ya kidato cha nne, aliweza kupata tafsiri rahisi kuwa, sinema ile ilikuwa juu ya majini wenye upendo wa kweli.

“Haya ndiyo mambo ninayoyataka sasa,” akasema moyoni mwake kisha akatoka na kuvuka barabara.

Moja kwa moja aliingia kwenye Mgahawa wa Shaonaro kwa lengo la kupata chakula ili kuvuta muda wa kuingia kwenye sinema. Alikula kijeshi, robo saa kabla ya sinema kuanza tayari alikuwa dirishani akikata tiketi – alichosubiri ilikuwa ni muda tu!



Dakika zilikwenda taratibu sana, lakini hatimaye akaona watu walioingia saa 12 wakitoka, haraka akatupa macho yake kwenye saa yake ya mkononi, zilibaki dakika tano tu. Watu walipoisha, akaingia zake ukumbini na kukaa siti za mbele kabisa akisubiri muda ufike.

Saa 2:00!

Sinema ikaanza!

***



“Majengo Polisi….” sauti ya konda ilisikika akiuliza abiria wake.

“Shusha!” Suma akasema kwa sauti kubwa kwa kuwa alikuwa amekaa siti ya nyuma.

“Polisi?!!!”akauliza tena.

“Amesema shusha….tatizo nyie makonda huwa mnauliza abiria halafu mnatoa vichwa nje, mtasikiaje?” abiria mmoja akadakia.

“Tuliza mzuka, nimesikia.”



Daladala ile iliyotokea Mbuyuni kuelekea Kiboriloni ilisimama kwenye makutano ya barabara ya kuelekea Kituo cha Polisi Majengo. Suma akalipa nauli na kushuka zake, akavuka barabara na kuanza kutembea taratibu.

Akiwa anakaribia kufika Posta, akakutana na msichana mrembo sana. Alikuwa mweupe, mrefu, mwenye tabasamu pana, aliyevalia gauni aina ya dira. Suma alivutiwa naye sana, akamwangalia kwa muda mrefu sana bila kupepesa macho. Alivyokutana naye kabisa, akajifanya kuangalia pembeni.

Walivyopishana, Suma akageuza shingo; akakutana uso kwa uso na yule msichana. Alikuwa na tabasamu pana sana. Wote wakasimama.

“Si vibaya tukisalimiana,” yule msichana akasema akitabasamu.



Suma hakuwahi kupata mshtuko wa moyo k**a wakati huo. Alihisi moyo wake k**a umepigwa shoti ya umeme baada ya kusikia sauti tamu ya yule dada. Hakukumbuka k**a hakumjibu ila naye aliendelea kutabasamu.

“Mambo vipi?” yule dada akasalimia.

“Poa, mzima?” akaitikia Suma.

“Wa afya.”

Wakapeana mikono.

“Mimi naitwa Zakhia, sijui mwenzangu?”

“Suma.”

“Unaishi mitaa gani?”



“Hapo chini, jirani na Makando Bar.”

“Sawa.”

“Wewe je?”

“Nakaa nyuma ya nyumba ya Kishamba Dispensary.”

“Ahsante, nimefurahi kukutana na wewe.”

“Hata mimi pia, ingawa nataka kukuambia jambo litakalokushangaza kidogo,” akasema Zakhia.

“Jambo gani hilo la kushangaza?”

“Samahani lakini, usinielewe vibaya.”

“Niambie.”



“Suma mimi ni mwanamke, najua sina haki ya kueleza hisia zangu kwa mwanaume kwa sababu wengi wanachukulia k**a ni tabia mbaya, lakini naogopa kuacha kufanya hivi kwa muda huu maana sina uhakika wa kukutana tena na wewe…” akasema Zakhia kisha akatulia kwa muda.

Pumzi ndefu zilivutwa puani mwa Zakhia, kisha akaanza kuzishusha taratibu kabisa. Suma alikuwa kimya akimsikiliza. Alishahisi jambo lililokuwa njiani kumfikia…

“Hisia? Hisia gani hizo Zakhia?”

“Nakupenda sana!”

Suma akakunja uso.

“Samahani Suma, usinielewe vibaya tafadhali, ni hisia za moyo wangu. Nilijua ungenifikiria vibaya, lakini sina namna ya kuficha hisia hizi wakati ni kweli ninakupenda kutoka ndani ya moyo wangu.”

“Samahani sana Zakhia.”

“Niambie tu!”



“Wewe ni mwanamke mrembo sana, lakini hatuwezi kuwa wapenzi.”

“Kwanini?”

“Basi tu!”

“Au una mtu wako?”

“Sina.”

“Hujanipenda?”

“Hapana.”

“Bali tatizo ni nini sasa?”

“Tatizo ni msimamo wa maisha.”

“Unamaanisha nini?”

“Katika maisha yangu sijapanga kumuoa mwanamke na kumuoa.”

“Kwanini?”

“Ni utaratibu tu.”



“Kwahiyo hutaoa?”

“Hapana…natarajia kuoa lakini siyo bi….” Suma akakatiza sentesi yake baada ya kujisahau na kutoka kumponyoka neno ambalo hakutaka lisik**e.

Zakhia akashtuka sana. Hakuelewa alichokuwa akimaanisha Suma. Haraka neno likamponyoka: “Sijakuelewa.”

“Samahani, kwaheri,” akasema Suma kwa sauti ya ukali kidogo kisha akaondoka zake.

“Watu wengine kwa kuingilia maisha ya wenzao bwana…sijui balaa gani hili?” akawaza kichwani mwake Suma.

Zakhia alibaki amesimama kwa mshangao akimsindikiza Suma kwa macho hadi alivyoishilia. Hakuwa na jibu sahihi juu ya yale yaliyotokea.

***



Mtu aliyekuwa akigonga mlangoni asubuhi hiyo ndiye aliyemshtua Suma usingizi. Ilikuwa Jumapili, saa 2:30 za asubuhi. Muda ambao kwa siku ya mapumziko k**a hiyo huwa yupo kitandani hadi saa 4. Akatoka kitandani na kusogea hadi mlangoni, akafungua.

Alikuwa ni baba yake mzazi.

“Kumbe baba, karibu sana baba…” akasema Suma kwa furaha.

“Ahsante.”

“Shikamoo mzee.”

“Marhaba,” akaitikia akionekana hana furaha kabisa usoni mwake.



“Vipi baba, mbona k**a haupo sawa? Kuna tatizo gani?”

“Tatizo lipo Suma mwanangu, tena tatizo kubwa sana lakini leo nahitaji hili tatizo liishe.”

“Ni nini baba?”

“Matusi tunayotukanwa sasa yanatosha. Njoro nzima inatutusi kwa sababu yako. Umetuvua nguo mwanetu.”

“Ni juu ya nini baba?”

“Wewe una tatizo gani?”

“Kuhusu nini baba?”

“Kwanini hutaki kuoa?”

“Ni hilo tu baba?”

“Kwani dogo?”



“Hapana mzazi wangu, nipe muda nijipange baba. Tatizo ni maisha hakuna kingine.”

“Unataka maisha gani zaidi ya haya?”

“Baba sina fedha, nitamtunza vipi mwanamke?”

“Mwanangu kila mtu huja na riziki yake. Kuoa ni faradhi, utajiwekea riziki mwenyewe mpaka utashangaa. Tafadhali nisikilize baba yako, mambo yanayozungumzwa kuhusu wewe ni makubwa sana, kikubwa ninachokuomba oa mwanangu. K**a huna mwanamke sema nikutafutie mimi mwenyewe, nimechoka na haya matusi ya mtaani.”



Suma alitulia kwa muda, akatafakari sana kisha akamwangalia baba yake…

“Nimekuelewa baba, nipe muda nitakuwa nimekamilisha hili suala.”

“Muda gani?”

“Miezi sita inatosha.”

“Mingi sana.”

“Baba ulichoniambia siyo chepesi kiasi hicho, ndiyo maana nimekuomba unipe miezi sita nitakuwa nimeshapata mtu sahihi.”

Baba yake akatingisha kichwa kukubaliana na jibu la mwanaye.



“Tafadhali na iwe hivyo.”

“Nakuahidi baba.”

“Sawa, ngoja mimi nikuache sasa.”

Suma akafungua droo la kabati la nguo, akatoa fedha kidogo na kumpatia baba yake. Hawakuwa na mazungumzo zaidi, mzee huyo akaondoka.



Kichwani mwa Suma kulikuwa na mwanamke mmoja tu; Zakhia! Ingawa hakutaka kuharibu mipango ya maisha yake, lakini aliona si vyema kuwaudhi wazazi wake, Zakhia ndiye mwanamke pekee ambaye angekidhi kuwa mke wake!



“Alisema anakaa kwa Kishamba….nitamfuatilia, tena leo hiihii!” akajisemea kwa sauti ya chini.

“Lakini pia sitakiwi kuacha wazo langu lipotee. Nitamfuatilia lakini wakati huo huo nitandelea kufikiria namna ya kupata jini wangu wa kuoa. Nimeshasikia maneno eti natakiwa kupuliza manukato makali chumbani, ngoja nitajaribu kufanya hivyo.

“Hapa inabidi nitumie mbinu mbili kwa wakati mmoja. Najua nitafanikiwa tu. Hawa wazee nao wananiingilia sana kwenye mambo yangu. Ngoja nitaona mwisho wake,” Suma akawaza.

Akajirudisha kitandani.

***



Aprili 14, 1996
Majengo, Moshi – Kilimanjaro

MOSHI nzima ilikuwa kimya kabisa, ni siku ambayo ilitawaliwa na mvua za rasharasha karibu siku nzima. Usiku wa kuamkia siku hiyo, mvua kubwa ilikesha, ilikatika alfajiri kabisa na kusababisha hali ya hewa kuwa tulivu sana.
Kwa namna udongo wa mji huo ulivyo, kila mahali kulikuwa na tope jingi kwenye barabara za mitaani. Ni k**a vile mvua hiyo iliamua kuacha kunyesha ili kuwapisha waumini wa dini ya Kikristo waende kanisani.
Ilikuwa Jumapili ya Matawi, katikati ya Kipindi cha Kwaresma ikiwa ni wiki moja kabla ya Sikukuu ya Pasaka. Kuanzia saa nane mchana, mvua ikaanza tena kunyesha. Ilinyesha kwa saa moja kwa kasi ya ajabu, halafu ikakatika kisha ikafuata rasharasha.

Suma alikuwa ametulia kimya chumbani mwake. Alikuwa na mawazo mengi sana; kwanza alimfikiria baba yake na uamuzi wake wa kumtaka aoe haraka, halafu pili alikuwa akimfikiria msichana ambaye angalau anaonekana kufaa kuwa mkewe – Zakhia. Juu ya yote hayo, aliwaza zaidi namna ambavyo anakwenda kubadilisha nadhiri aliyojiwekea kwa muda mrefu sasa.

Alitamani sana kuoa jini na si binadamu. Kichwani mwake aliamini ni jini pekee ndiye ambaye angeweza kumfanya akaishi maisha ya raha mustarehe. Katika ubongo wake kulijengeka taswira ya kwamba majini ni viumbe wenye mapenzi, wasiotesa na wanaojali kuliko binadamu ambao wamekuwa wasaliti mara kwa mara kwa wenzi wao.
“Tatizo ni hilo…” akawaza.
“Lakini nitawezaje kujipinga mwenyewe?”

Alipata tabu sana ya kuwaza na kuwazua kichwani mwake. Akiwa mwenye kujiuliza maswali lukuki na kujijibu mwenyewe: “Mimi sina pesa, sasa msichana mzuri k**a Zakhia, nitawezaje kumtunza na akaishi vizuri k**a wanawake wengine? Jamani si nitadhalilika mimi? Au nikubali tu? Baba alisema kwamba kuoa ni jambo jema na mwanamke huja na riziki yake…
“Sasa k**a aliniongopea nitajuaje? Nitawezaje kufanya majaribio katika jambo makini na linalohusu maisha yangu k**a hili? Nitaweza kweli? Lazima nipate jibu la swali hili kwanza. Sitakiwi kukurupuka tu….sitakiwi kabisa…mimi ni mwanaume mwenye akili timamu na kichwa changu kinafanya kazi vizuri.

“Mwanamke anahitaji matunzo. Nitayatoa wapi? Baba ananidanganya na maneno yake ya uongo mtupu…k**a mwanamke huja na riziki yake, mbona yeye amemuoa mama na wametuzaa sisi hadi tunakuwa wakubwa, bado wanaishi maisha duni? Wanaishi nyumba ya kupanga? Au mama hana riziki? Sisi watoto wao je? Uongo mtupu!” aliwaza Suma.
Kwa kiasi kikubwa alipingana na mawazo ya baba yake, alijua ni ya kumshawishi tu! Hata hivyo, kuna jambo liliingia kichwani mwake kwa kasi ya ajabu sana. Alitakiwa kuheshimu na kusikiliza mawazo ya baba yake, lakini akiendelea kufanyia kazi ndoto zake.

“Acha nikazungumze na Zakhia, muda ambao nipo naye nitaendelea kufikiria namna ya kumpata jini wangu,” akawaza Suma.
Wazo hilo lilipita, tena aliamua kwenda kumfuatilia siku hiyohiyo. Tatizo likawa ni mvua. Aliendelea kusubiri sana mvua ipungue lakini haikukatika. Rasharasha ziliendelea. Hadi saa kumi mvua ilikuwa haijakatika. Alichoamua ilikuwa ni kutoka kwa kutumia mwavuli wake. Alipita njia za mkato.

Muda mfupi baadaye alikuwa anapita kwenye makutano ya barabara inayoelekea Faya na ile inayopandisha kwenda sokoni kupitia kwenye Baa ya Kipanga. Alikazana hadi alipokutana na Barabara ya Tunisia inayoelekea Mbuyuni kupitia Kiwanda cha Kahawa cha Coffee Quring na ile inayopandisha kwenda Kwa Kishamba.

Akashika ya kulia kwake. Hakuuachia mwavuli wake ambao ulimsaidia sana kuzuia mvua iliyoendelea kunyesha. Dakika tatu baadaye alikuwa ameshafika Kwa Kishamba. K**a alivyoelekezwa na Zakhia, alizunguka nyuma ya Zahanati hiyo na kwenda kusimama kwenye duka moja mbele ya nyumba hiyo.



“Habari yako ndugu yangu?” Suma akamsalimia mhudumu aliyekuwa pale dukani.

“Salama, karibu.”

“Ahsante…sihitaji bidhaa yoyote dukani kwako ila naomba kuuliza.”

“Uliza tu ndugu yangu.”

“Kuna msichana namwulizia, alinielekeza anaishi humu ndani.”

“Anaitwa?”

“Zakhia.”

“Zakhia?” akamwuliza kwa mshangao kidogo.

“Vipi mbona umeshtuka ndugu yangu?”



“Ni ndugu yako?”

“Hapana ni rafiki yangu.”

“Dah!”

“Vipi kwani?”

“Yule matawi ya juu sana, nimeshangaa kuona mnafahamiana tena mna ukaribu.”

“Kawaida tu, yupo lakini?”

“Kwani yeye amekuelekeza lini hapa?”

“Muda kidogo, ni k**a miezi minne hivi imepita.”

“Ni kweli alikuwa anaishi hapa…”

“Na sasa?”



“Amehama.”

“Amehamia wapi?”

“Soweto.”

“Dah….sijui itakuwaje sasa?” akasema kwa sauti Suma.

“Vipi ni muhimu sana kuonana naye?”

“Sana tena sana yaani.”

“Pole sana, unajua anapofanyia kazi?”

“Hapana.”

“Nitakusaidia, labda hapo unaweza kumpata.”

“Nitashukuru sana ndugu yangu.”

“Anafanya kazi Benki ya CRDB.”



“Wapi?”

“Ile iliyopo kwenye round about. Jengo la Kahawa.”

“Ahsante sana kaka, utakuwa umenisaidia sana. Ngoja nitajaribu kwenda kumwulizia pale.”

“Poa bwana.”

Suma akaondoka zake.

Address

Uhindini
Mbeya

Telephone

+255745327319

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Joo_Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Joo_Tz:

Shortcuts

Share