Kiwandanitz

Kiwandanitz Trusted Source of Business in Tanzania and Outside its Borders. You're Most Welcome.

‎Wataalamu na watumiaji wa lishe salama wanahoji :-‎‎Je, Mchele Unaweza Kukaa Muda Mrefu Bila Kuharibika ?‎‎K**a jibu nd...
11/09/2025

‎Wataalamu na watumiaji wa lishe salama wanahoji :-

‎Je, Mchele Unaweza Kukaa Muda Mrefu Bila Kuharibika ?

‎K**a jibu ndiyo.........
‎Fhamu ni kwaniniiiiiiiiiii ?

‎Vivyo hivyo.

‎K**a jibu hapana........
‎Fahamu ni kwaniniiiiiiii ?

‎Na................

‎K**a Mchele Unaweza Kukaa Muda Mrefu Bila Kuharibika...............
‎Fahamu Unaweza Vipi Kutambua Mchele Uliokaa Muda Mrefu, Pia ni Hatari Zipi Zinazoambatana kwa Mlaji ?

‎1️⃣ Je, ni Kweli Mchele Unakaa Muda Mrefu ?

‎Ndiyo. Kwa asili yake, mchele ni nafaka kavu inayoweza kudumu muda mrefu – kati ya miezi 6 hadi miaka 2 kulingana na aina yake na jinsi unavyohifadhiwa.

‎🌾 Mchele mweupe hudumu muda mrefu zaidi kwa sababu huondolewa maganda na mafuta yake asilia.

‎🌾 Mchele wa kahawia hudumu muda mfupi zaidi kwa kuwa una mafuta ya asili yanayoweza kuharibika haraka.

‎2️⃣ Nitajuaje Kuwa Mchele huu Umekaa Muda Mrefu ?

‎Dalili kuu za mchele uliokaa muda mrefu :-
‎🟩 Harufu: Mchele unaonukia k**a unyevu, vumbi, au dawa za kuhifadhia.

‎🟩 Rangi: Hubadilika kutoka nyeupe safi kwenda kijivu, njano au kahawia isiyo ya asili.

‎🟩 Uwepo wa wadudu au ukungu: Madoa meusi, chembe zenye mashimo au unga wa vumbi.

‎🟩 Kubadilika kwa ladha baada ya kupikwa: Hauna ladha nzuri tena, una ladha ya kigeni na wakati mwingine hutoa harufu isiyo yenyewe.

‎3️⃣ Kwa nini Baadhi ya Mchele wa Kuuzwa Unakaa Muda Mrefu Ghalani-Store ?

‎Sababu Kuu :-

‎1. Kusubiri msimu wa bei kupanda – wafanyabiashara wengine huficha akiba ili wauze kwa faida kubwa baadaye.

‎2. Ukosefu wa masoko ya moja kwa moja – mara nyingi wakulima hulazimika kuhifadhi mchele ghalani kwa muda mrefu wakisubiri wanunuzi wakubwa.

‎3. Changamoto za usafiri na miundombinu – mchele hukwama ghalani kutokana na gharama kubwa za usafirishaji au barabara zisizopitika.

‎4. Uhifadhi wa kibiashara – mchele mwengine huwekewa dawa za viwandani za kuzuia wadudu, ili udumu kwa miezi au hata miaka.

‎4️⃣ Madhara Gani kwa Mlaji Anayekula Mchele Uliokaa Muda Mrefu Ghalani-Store ?

‎Kwa mujibu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na tafiti za lishe.

‎🟩 Kupungua kwa thamani ya lishe – protini, vitamini na madini huanza kupotea taratibu.

‎🟩 Kuingia kwa sumu na kemikali – dawa za kuhifadhia mchele zinaweza kuathiri ini, figo na kusababisha matatizo ya kiafya ya muda mrefu.

‎🟩 Madhara ya bakteria na fangasi – baadhi ya mchele huota ukungu unaozalisha sumu hatari inayojulikana k**a aflatoxin, inayoweza kusababisha saratani.

‎🟩 Kuvuruga mfumo wa mmeng’enyo – kula mchele uliokaa sana huleta kuharisha, gesi tumboni au kutapika.

‎🎯 Mwisho :-

‎Mchele unaweza kudumu muda mrefu, lakini ubora wake hupungua kadri unavyohifadhiwa. Mlaji anatakiwa kutumia hisia zake – kuangalia, kunusa na kupima ladha – kabla ya kupika. Ni vyema kununua mchele mpya unaojulikana asili yake badala ya kutegemea akiba ya muda mrefu ghalani-store.





‎Karibu katika uchambuzi wa kina kuhusu maswali ambayo yamekuwa yakizua mijadala katika jamii, hususan kwa walaji wa bid...
29/08/2025

‎Karibu katika uchambuzi wa kina kuhusu maswali ambayo yamekuwa yakizua mijadala katika jamii, hususan kwa walaji wa bidhaa muhimu zaidi katika familia za Kitanzania – Mchele.

‎Swali Kuu :-
‎Je, Kweli Kuwa Mchele Unaouzwa Hupakwa Mafuta ?

‎Kwa mujibu wa tafiti za wataalamu wa afya na kilimo-biashara, ni kweli kwamba katika baadhi ya masoko, mchele hupakwa mafuta, inawezekana pia mafuta yasiyo salama, lengo likiwa ni kuufanya uangaze, usiharibiwe na wadudu, na kuvutia macho ya wanunuzi.

‎Lakini Sasa, Unaweza Je Kujua K**a Mchele Unaonunua Umepakwa Mafuta ?

‎Kuna Ishara Kuu Tatu :-

‎1️⃣. Mchele Unaong’aa Kupita Kawaida.

‎2️⃣. Harufu Isiyo ya Kawaida, mara nyingine harufu ya mafuta.

‎3️⃣. Ukiosha Mchele Mara ya Kwanza, Maji Hugeuka ya Rangi ya Mafuta au Yenye Povu Lisilo la Kawaida.

‎Sababu Gani Zinapelekea Mchele Upakwe Mafuta ?

‎Kuna Sababu Kuu Mbili :-

‎1️⃣. Kibiashara, Wauzaji wengine hufanya hivyo ili mchele uangaze na kuvutia wateja.

‎2️⃣. Kuhifadhi, Hii ni njia ya kienyeji ya kuzuia wadudu na kuudumisha mchele ukae muda mrefu sokoni.

‎Hata hivyo, wataalamu wa afya wanatoa onyo kali, kwa kuwa madhara kwa mlaji si madogo.

‎Miongoni mwa athari zinazoweza kumpata mlaji wa mchele uliopakwa mafuta ni pamoja na :-

‎1️⃣. Shida za mfumo wa chakula, ikiwemo kuharisha au kutapika.

‎2️⃣. Madhara ya ini na figo kutokana na sumu ya mafuta yasiyofaa.

‎3️⃣. Hatari ya muda mrefu ya saratani endapo mafuta yaliyotumika haya hitajiki mwilini.

‎Mwisho :-
‎Kwa mujibu wa taasisi ya Afya Duniani (WHO) na tafiti za Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), matumizi ya kemikali au mafuta yasiyo salama katika vyakula ni kosa la kiafya na kisheria.

‎Hitimisho :-
‎Watanzania wote tunakumbushwa kuwa makini tunaponunua mchele. Chagua mchele unaoujua asili yake, unaonunuliwa moja kwa moja kutoka kwa wakulima au wauzaji wanaoaminika.






‎Je, Mchele Unao Kula ni Bora, Salama na  Safi ?‎Kwa mujibu wa Tanzania Bureau of Standards (TBS), TFDA, na tafiti kutok...
13/08/2025

‎Je, Mchele Unao Kula ni Bora, Salama na Safi ?
‎Kwa mujibu wa Tanzania Bureau of Standards (TBS), TFDA, na tafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), mchele bora hujulikana kwa sifa zifuatazo:-

‎🔍 1️⃣. Muonekano wa Chembe za Mchele

‎Mchele bora kwa mlaji ni lazima chembe zake ziwe sawa kwa umbo, siyo zilizopasuka pasuka.
‎Hauna uchafu k**a changarawe, unga mwingi au mabaki ya maganda.

‎🔬 2️⃣. Harufu ya Asili

‎Mchele bora hauna harufu ya kemikali, ukungu au mafuta mafuta.
‎Mchele wa aina ya aromatic k**a wa Kilombero au Mbeya una harufu ya kupendeza hata kabla ya kupikwa.

‎🌾 3️⃣. Usafi na Usalama wa Afya

‎Umetuzwa kwenye ghala safi, kavu, lenye uingizaji hewa wa kutosha.
‎Unathibitishwa na nembo ya TBS au una cheti cha ubora kutoka bodi husika.

‎📦 4️⃣. Ufungaji Sahihi

‎Mchele wa kifungashio una taarifa sahihi za:-
‎1. Jina la kampuni au mkulima
‎2. Mahali kilimo kilipofanyika
‎3. Tarehe ya kusindika na mwisho wa matumizi
‎4. Alama ya ubora (TBS/TMQ)

‎📊 TAKWIMU :-

‎Tanzania huzalisha zaidi ya tani milioni 2.6 za mpunga kwa mwaka, lakini bado baadhi ya mikoa huagiza mchele kutoka nje kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi kwa walaji kuhusu mchele bora wa ndani.

‎Zaidi ya asilimia 38 ya walaji wa mijini hununua mchele wa bei ya juu kwa dhana kuwa ndio bora, wakati mikoa ya uzalishaji hutoa mchele mzuri kwa gharama ya chini hadi 30% – 40%.

‎💬 Dkt. Hadija Mwakalukwa – Mtafiti Kutoka SUA Anasema:-
‎“Wateja wanatakiwa kuchagua mchele uliopitia usindikaji rasmi na uliofungwa vizuri. Harufu, rangi na usafi vinaweza kuashiria ubora, lakini muhimu zaidi ni kufuatilia alama za ubora na maeneo ya uzalishaji”

‎Kwa kufanya hivyo, utalinda afya ya familia yako, kuokoa gharama, na kuchangia katika kuinua wakulima wa ndani.




‎K**a kuna jambo ambalo huzungumzwa sana na wakulima, wauzaji wa jumla, wafanyabiashara wa masoko, na walaji wa kila sik...
26/07/2025

‎K**a kuna jambo ambalo huzungumzwa sana na wakulima, wauzaji wa jumla, wafanyabiashara wa masoko, na walaji wa kila siku wa chakula nchini Tanzania, basi ni hili;

‎"Kwa nini Bei ya Mchele Huporomoka Wakati wa Mavuno Lakini Huongezeka Zaidi Punde Baada ya Mavuno ?”

‎📉 Wakati wa Mavuno – Bei Hushuka, Kwanini ?

‎Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), na taarifa za utafiti wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Bodi ya Nafaka (CBT), kuna sababu kuu tatu (3) zinazosababisha kushuka kwa bei ya mchele msimu wa mavuno:-

‎1️⃣ Uwingi wa Mchele Sokoni kwa Wakati Mmoja.

‎Wakulima kutoka mikoa k**a Mbeya, Morogoro, Shinyanga, Rukwa na Tabora huvuna kwa kipindi kimoja, hivyo maghala, masoko na wauzaji hupokea mzigo mkubwa kwa wakati mmoja.
‎➡️ Kwa lugha rahisi “Samaki Wengi Wakielea, Bei Hushuka Sokoni.”

‎2️⃣ Wakulima Kuuza Haraka Kwa Matumizi ya Haraka.

‎Wakulima wengi huchagua kuuza mazao yao mara tu baada ya mavuno kwa sababu:-

‎1. Wana mahitaji ya fedha ya haraka (kulipa madeni, ada za watoto, mahitaji ya nyumbani NK).

‎2. Hawana maghala bora ya kuhifadhi.

‎3. Hawawezi kusubiria bei ipande kwa sababu ya presha ya kiuchumi.

‎➡️ Hivyo huchangia kushuka kwa bei kwa sababu ya wingi wa wauzaji dhidi ya idadi ndogo ya wanunuzi.

‎3️⃣ Ukosefu wa Mfumo Madhubuti wa Stakabadhi ya Ghala (Warehouse Receipt System)
‎Kwa mujibu wa Tanzania Mercantile Exchange (TMX), wakulima wachache tu hutumia mfumo rasmi wa kuhifadhi mpunga/mchele hadi bei iwe juu.

‎➡️ Wengi huuza kwa haraka, kwa bei za walanguzi na sio za mkulima.

‎📈 Nje ya Msimu – Kwa nini Bei Hupanda ?

‎1️⃣ Upungufu wa Mchele Sokoni.

‎Baada ya miezi kadhaa, kiasi kikubwa cha mchele huwa tayari kimeshauzwa au kumalizika kwenye masoko au ghala.

‎➡️ Mahitaji huendelea kuwepo, lakini upatikanaji wa bidhaa hupungua.

‎➡️ Kwa lugha rahisi “Kidogo Chenye Thamani Hulipiwa Zaidi”

‎2️⃣ Usafirishaji Mgumu Kutoka Mikoa ya Uzalishaji.

‎Wakati wa mvua, barabara nyingi vijijini huwa hazipitiki vizuri, na baadhi ya mashamba huathiriwa na mafuriko.

‎➡️ Hii husababisha gharama za usafirishaji kupanda, hivyo husababisha bei ya mwisho kwa mlaji kuwa juu zaidi.

‎3️⃣ Mfumuko wa Bei na Gharama za Uendeshaji.

‎Kupanda kwa gharama za mafuta, ushuru wa usafirishaji, kodi na gharama za kuhifadhi huongeza bei.

‎➡️ Wasambazaji hulazimika kuongeza bei kufidia gharama hizo.

‎📊 Namba Hazidanganyi

‎🟩 Ripoti ya mwaka 2023 kutoka NBS inaonyesha kuwa bei ya kilo moja ya mchele ni;

‎Tsh 1,200 – 1,400 wakati wa mavuno.

‎Tsh 2,000 – 2,500 nje ya msimu, katika maeneo ya mijini k**a Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.

‎🟩 Asilimia 67 ya wakulima wa mpunga nchini huuza mazao yao ndani ya siku 30 baada ya mavuno, bila kusubiri bei kuwa nzuri (SUA Research Report 2022).

‎🗣️ Wadau Wanasema Je..........?

‎Mzee Mathias Lyimo, mkulima wa Mbarali, Mbeya anasema...............

‎“Tunashindwa Kuvumilia, Tuna Madeni, Watoto Wanahitaji Ada, Hivyo Tunauza tu Hata k**a Bei ni Ndogo.”

‎Bi. Shukuru Nassoro, muuza mchele Kariakoo, Dar es Salaam asema..........

‎“Wakati Hakuna Mavuno, Bei Hupanda. Hata Sisi Wauzaji Tunahangaika Kupata Mchele wa Uhakika.”

‎✍️ Karibu Katika Maoni...............

‎Sababu Gani Zinachangia Bei ya Mchele Huporomoka Wakati wa Mavuno Lakini Huongezeka Zaidi Punde Baada ya Mavuno ?



‎Wapi Utapata Mchele wa Bei Nafuu Ambao ni Bora, Salama na Safi ?‎‎Katika dunia ya leo inayozingatia afya, swali moja ku...
23/07/2025

‎Wapi Utapata Mchele wa Bei Nafuu Ambao ni Bora, Salama na Safi ?

‎Katika dunia ya leo inayozingatia afya, swali moja kubwa linaendelea kuulizwa na Watanzania wengi kila siku;

‎“Ni wapi nitapata mchele wa bei nafuu lakini wenye ubora, usalama na safi kwa matumizi ya familia yangu ?”

‎Taarifa hii inaleta majibu ya kitaalamu, kwa uchambuzi wa kina, ili kujibu swali la maelfu ya walaji, wafanyabiashara na wadau wote wa sekta ya chakula nchini Tanzania.

‎🛒 Wapi Utapata Mchele wa Bei Nafuu Ambao ni Bora, Salama na Safi ?

‎Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CBT), mikoa ifuatayo inatambulika kitaifa kwa kuzalisha mchele bora zaidi, hivyo huuzwa kwa bei nafuu sokoni kutokana na ushindani wa uzalishaji:-

‎✅ 1. Mbeya – Haswa Bonde la Usangu (Mbarali) na Kyela

‎Mchele maarufu: “Super Mbeya” na ule unaotoka Kamsamba Sumbawanga maarufu "Mchele wa Kamsamba”

‎Bei ni nafuu kutokana na uzalishaji mkubwa na uwepo wa viwanda vya kukoboa ndani ya mkoa.

‎✅ 2. Morogoro – Kilombero na Ifakara

‎Inazalisha mchele wa “Kilombero Aromatic Rice” unaovutia wateja kwa harufu ya asili na ladha.

‎✅ 3. Shinyanga – Kahama na Ushetu

‎Wingi wa mashamba na njia rahisi za usafiri hufanya bei kuwa ya wastani na mchele kufika kwa urahisi kwa walaji.

‎✅ 4. Tabora – Igunga na Nzega

‎Wanazalisha kwa wingi na kuuza kwa bei ya chini kuelekea Kanda ya Kati na Magharibi.

‎✅ 5. Rukwa – Bonde la Ziwa Rukwa

‎Mchele ni wa bei nafuu na hushindana kwa ubora na ule wa Mbeya.

‎🟩 Tanzania huzalisha zaidi ya tani milioni 2.6 za mpunga kwa mwaka, lakini bado baadhi ya mikoa huagiza mchele kutoka nje kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi kwa walaji kuhusu mchele bora wa ndani.

‎Zaidi ya asilimia 38 ya walaji wa mijini hununua mchele wa bei ya juu kwa dhana kuwa ndio bora, wakati mikoa ya uzalishaji hutoa mchele mzuri kwa gharama ya chini hadi 30–40%.






‎Kwanini Mbeya – Mkoa Pekee Unaongoza Katika Uzalishaji wa Mchele Bora na Salama Tanzania.‎‎Karibu pamoja tuangazie mcha...
20/07/2025

‎Kwanini Mbeya – Mkoa Pekee Unaongoza Katika Uzalishaji wa Mchele Bora na Salama Tanzania.

‎Karibu pamoja tuangazie mchango wa Mkoa wa Mbeya katika kilimo, uzalishaji na biashara ya mchele bora, salama na wa uhakika nchini Tanzania.

‎Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), na taasisi ya SRI-Africa (System of Rice Intensification Africa).......................
‎"Mbeya Imekuwa Miongoni mwa Mkoa Kinara Katika Mnyororo Mzima wa Thamani ya Mpunga na Mchele Kuanzia Kilimo, Uchakataji hadi Masoko"

‎✅ Sababu Tano Kuu Zinazoifanya Mbeya Kuwa Mkoa Pekee na Maarufu Katika Kilimo na Biashara ya Mchele Tanzania.

‎1️⃣ Uwepo wa Bonde la Usangu – Chanzo Kikuu cha Maji ya Umwagiliaji

‎Mbeya imebarikiwa kuwa na Bonde kubwa la Usangu lililo katika Wilaya ya Mbarali, eneo lenye mfumo wa asili wa mito, mabonde na miundombinu ya umwagiliaji.
‎➡️ Hali hii huwezesha kilimo cha mpunga kwa misimu yote miwili ya mwaka, huku ikihakikisha upatikanaji wa maji ya kutosha, jambo linaloongeza mavuno na ubora wa mazao.

‎2️⃣ Udongo Wenye Rutuba na Hali ya Hewa Inayofaa

‎Mbeya ina ardhi yenye rutuba ya hali ya juu, haswa katika maeneo ya Mbarali, Kyela na Rujewa.
‎➡️ Udongo huu una virutubisho muhimu kwa ukuaji wa mpunga bora na unaongeza kiwango cha uzalishaji.
‎➡️ Aidha, mkoa huu una mvua za kutosha na halijoto ya wastani inayoruhusu ustawi wa zao la mpunga bila changamoto kubwa za ukame au magonjwa.

‎3️⃣ Miundombinu Imara ya Usindikaji na Masoko

‎Mbeya ina idadi kubwa ya viwanda vya kukoboa mchele, maghala ya kuhifadhi, na masoko ya kisasa k**a vile Soko la Mchele la Igawa na mtandao wa wauzaji kutoka ndani na nje ya nchi.
‎➡️ Hii huwezesha uzalishaji wa mchele ulio safi, salama na unaokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa, kwa matumizi ya nyumbani na kuuza nje.

‎4️⃣ Uwekezaji wa Serikali na Sekta Binafsi

‎Kwa miaka ya hivi karibuni, serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) na Tanzania Mercantile Exchange (TMX) imewekeza katika sekta ya mpunga Mbeya.
‎➡️ Wakulima hupata mikopo, pembejeo, elimu ya kilimo bora na masoko ya uhakika kwa kutumia mifumo ya kisasa.
‎➡️ Pia, mashirika binafsi na miradi ya kimataifa k**a AGRA, BRiTEN na Kilimo Trust yameongeza tija kwa kuwajengea wakulima uwezo.

‎5️⃣ Utamaduni wa Kilimo cha Mpunga na Ushirikiano wa Jamii

‎Mbeya ina historia ya muda mrefu ya kilimo cha mpunga k**a zao kuu la kiuchumi.
‎➡️ Wakazi wake wameurithisha utamaduni huu kizazi kwa kizazi, wakijenga utaalamu wa asili na wa kisasa.
‎➡️ Ushirikiano baina ya wakulima, vikundi vya ushirika na taasisi za kifedha umeimarisha mnyororo wa thamani kutoka shambani hadi sokoni.

‎📈 Takwimu Zinazothibitisha Umaarufu wa Mkoa wa Mbeya Kuwa Kinara Katika Uzalishaji wa Mchele Bora na Salama Tanzania.

‎Mbeya huzalisha zaidi ya asilimia 23 ya mpunga wote nchini (Sensa ya Kilimo 2020/21 – NBS).

‎Inasafirisha mchele kwenda mikoa ya Kanda ya Kati, Kaskazini, Mashariki na hata nje ya nchi (Zambia, Malawi, DRC).

‎🎤 Kauli ya Mdau wa Kilimo – Bi. Amina Mwamwaja, mkulima wa Kyela;

‎“K**a mkulima wa mpunga Mbeya, najivunia kuona mazao yangu yanafika Dar es Salaam, Arusha hadi Zambia. Serikali imetuwezesha kupata mikopo na mafunzo, mchele wetu ni bora na wa uhakika.”

‎MWISHO:
‎Mkoa wa Mbeya umejijengea heshima kitaifa k**a kitovu cha mchele bora Tanzania. Kupitia mazingira rafiki ya kilimo, rasilimali watu, uwekezaji wa serikali na sekta binafsi pamoja na miundombinu ya usindikaji na usafirishaji Mbeya inaendelea kuwa dira ya maendeleo katika sekta ya mpunga kwa taifa na Afrika Mashariki.



‎FAHAMU MIKOA MITANO INAYOONGOZA KWA KILIMO CHA MPUNGA NA BIASHARA YA MCHELE NCHINI TANZANIA‎‎Katika miaka ya hivi karib...
17/07/2025

‎FAHAMU MIKOA MITANO INAYOONGOZA KWA KILIMO CHA MPUNGA NA BIASHARA YA MCHELE NCHINI TANZANIA

‎Katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya kilimo cha mpunga nchini Tanzania imeendelea kuwa miongoni mwa sekta muhimu zinazochangia kwa kiasi kikubwa chakula, ajira, na pato la taifa.
‎Mchele ni chakula kikuu kwa jamaniii kubwa ya Watanzania wengi pia bidhaa ya kibiashara ndani ya nchi na nje ya mipaka ya nchi.

‎Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Wizara ya Kilimo, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na taasisi k**a Tanzania Agricultural Research Institute (TARI), zinaeleza katika kipindi cha mwaka 2020/2021, Tanzania ilishika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa mpunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), nyuma ya Madagascar.

‎Imebainika kuwa kuna mikoa mitano ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa mpunga na biashara ya mchele nchini Tanzania.

‎📊 Ifuatayo ni Mikoa Mitano Inayoongoza kwa Kilimo cha Mpunga na Biashara ya Mchele Tanzania

‎1️⃣ Mkoa wa Mbeya

‎Wilaya kuu: Mbarali, Kyela, na Busokelo.

‎Maeneo ya Bonde la Usangu ndiyo kitovu kikuu cha kilimo cha mpunga nchini.

‎Uzalishaji: Zaidi ya tani 800,000 kwa mwaka.

‎Kibiashara: Mkoa huu unasafirisha mchele kwenda mikoa ya jirani k**a Dar es salaam, Morogoro, Dodoma, Iringa NK pia nje ya nchi kupitia mipaka ya kusini (Malawi na Zambia).

‎2️⃣ Mkoa wa Shinyanga

‎Wilaya kuu: Shinyanga Vijijini na Kahama.

‎Umejipambanua kwa kilimo cha mpunga unaotegemea mvua na unalimwa kwa wingi katika mabonde ya mto Simiyu.

‎Kibiashara: Mchele wa Shinyanga husafirishwa kwa wingi kwenda Mwanza, Tabora, na Dar es Salaam.

‎3️⃣ Mkoa wa Morogoro

‎Wilaya kuu: Kilombero, Ulanga na Ifakara.

‎Bonde la Kilombero lina rutuba kubwa na mvua za kutosha, hivyo hutoa mchele wa hali ya juu.

‎Kibiashara: Mkoa huu una viwanda vya kuchakata mchele na usafirishaji wa bidhaa kwenda Dar es Salaam, Pwani na hata Zanzibar.

‎4️⃣ Mkoa wa Tabora

‎Wilaya kuu: Urambo na Sikonge.

‎Umeanza kuonekana kwa kasi kubwa katika uzalishaji wa mpunga kutokana na uwekezaji wa mashamba makubwa.

‎Kibiashara: Mchele kutoka Tabora husafirishwa kwenda Singida, Dodoma na Kigoma.

‎5️⃣ Mkoa wa Mwanza

‎Wilaya kuu: Misungwi, Kwimba na Magu.

‎Mikoa ya kanda ya ziwa ina hali ya hewa inayowezesha uzalishaji mkubwa wa mpunga hususani kwenye mabonde ya mito.

‎Kibiashara: Mwanza ni soko la kimkakati kwa biashara ya mchele kutokana na uwepo wa bandari ya ziwa na mtandao wa reli na barabara unaorahisisha usafirishaji wa mazao kwenda Kagera, Mara, na Kenya.

‎🔍 Mwisho
‎Mikoa hii mitano ina mchango mkubwa katika kuhakikisha usalama wa chakula, kuongeza kipato cha wakulima, na kukuza biashara ya ndani na ya kimataifa ya mchele. Serikali, kupitia Wizara ya Kilimo na taasisi k**a Tanzania Mercantile Exchange (TMX) na TADB, inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya masoko, usindikaji, na miundombinu ya kilimo.




Fahamu Kwanini Kila February 14 Huadhimishwa ni Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) ?Tumaini langu upo poa................
14/02/2025

Fahamu Kwanini Kila February 14 Huadhimishwa ni Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) ?

Tumaini langu upo poa.............

Karibu tufahamu kwanini kila ifikapo February 14 Dunia huadhimisha ni siku ya wapendanao (Valentine’s Day) ?

Twendeeeee tufahamu 👇

Siku ya wapendanao, au Valentine’s Day, huadhimishwa kila mwaka tarehe 14 Februari duniani kote k**a siku ya kuonesha upendo, hasa kati ya wapenzi.
Kumbukizi ya siku hii imechochewa na historia ya kidini na tamaduni za Kirumi.

Asili ya Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day)

Asili ya Valentine’s Day inamhusu Mtakatifu Valentine, ambaye alikuwa Padri wa Kirumi katika karne ya 3.

Mfalme Claudius II wa Roma aliamua kuwa askari wa kijeshi hawapaswi kuoa, akiamini kuwa ndoa huwafanya kuwa dhaifu vitani. Lakini Padre Valentine alikaidi agizo hilo na akaendelea kuwaoza/kufungisha ndoa askari hao kwa siri.

Alipogunduliwa, alik**atwa na kuhukumiwa kifo.
Alipokuwa gerezani, aliandika barua ya kuaga kwa binti wa mlinzi wa gereza, ak**alizia na maneno "From your Valentine", ambayo bado hutumika mpaka leo.

Valentine aliuawa tarehe 14 Februari, mwaka 269 BK, na hivyo jina lake likahusishwa na upendo wa kimapenzi.

Mila za Kirumi (Lupercalia)
Kabla ya Ukristo, Warumi walikuwa na sherehe ya Lupercalia, iliyofanyika Februari 13-15, kusherehekea uzazi na ndoa. Wakati Ukristo ulipoenea, Kanisa Katoliki lilitaka kuondoa mila za kipagani na badala yake likaifanya Siku ya Mtakatifu Valentine rasmi mnamo karne ya 5 chini ya Papa Gelasius I.

Hamasa ya Valentine’s Day Duniani

Katika enzi za kati (Middle Ages), watu walianza kuihusisha siku hii na upendo wa kimapenzi.
Mshairi Geoffrey Chaucer wa Uingereza aliandika mashairi yanayohusisha Valentine’s Day na upendo wa wapenzi.
Hii ilichochea kuenea kwa kumbukizi ya siku ya Valentine’s Day.

Pia mnamo Mwaka 1840, mwanamke aitwaye Esther Howland kutoka Marekani alianzisha biashara ya kadi za Valentine's Day 💌 na kuzifanya kuwa maarufu sana.

Katika Karne ya Leo................
Valentine’s Day ni siku kubwa kwa kumbukizi ya upendo (Siku ya Wapendanao) ambapo watu hununua maua, chokoleti, kadi za upendo kwa ajili ya wapendwa wao.

Happy Valentine's Day 💞


Kiwandani ni Watoa Huduma ya Matangazo ya Biashara (Mtandaoni - Digital Marketing na Nje ya Mtandaoni - Printing)Kuhusu ...
06/02/2025

Kiwandani ni Watoa Huduma ya Matangazo ya Biashara (Mtandaoni - Digital Marketing na Nje ya Mtandaoni - Printing)

Kuhusu Ubunifu wa Sanaa ya Picha.

Awali Kiwandani Tulitoa Huduma ya Sanaa ya Utengenezaji Picha K**a OFFER kwa Kila Huduma ya Tangazo.

Baadaa ya Mapokezi kuwa Makubwa, Uhitaji Kuongezeka Ndipo Tukaanza Kuuza kwa Kila Anayehitaji.

Kwa Kuwa Mwezi February (Valentine's Day) ni Mwezi wa Kushare Upendo kwa Familia, Mwenza, Ndugu, Jamaa na Marafiki, Kiwandani Tumeanda OFFER Maalumu Kwako👇

🎑 🏞 🗾 🌄 🎑 🏞 🗾 🌅 🎑 🏞 🗾 🌅

✍️ Bei za Kawaida za Picha Mbao Kuanzia :-
A5 ni Tsh 15,000/=
A4 ni Tsh 25,000/=
A3 ni Tsh 45,000/=
A2 ni Tsh 80,000/= na
A1 ni Tsh 100,000/= .......kwa Picha Mbao Moja, Katika Kipindi Hiki cha Valentine's Day Utapata Picha Mbao Kuanzia Tatu kwa NUSU BEI

Sambamba na Hilo!
Kwa Wewe Unayehitaji Kutengeneza PICHA MBAO Moja tu, Unapata na BONUS ya GB 10 za Internet Bure za Mtandao wa HALOTEL

Mawasiliano 0714 543 336
Victorian Sosten - Huduma kwa Wateja

Mahali: Morogoro - Soko la Chifu Kingalu, Chumba Namba 137.

Mikoani Tunatuma Bila Shinda Yoyote.

Karibu Tukuhudumie.





Najua umesikiaaaaaa 🧏‍♂️Yawezekana pengine umeambiwa mengi kuhusu "Role Models" Twendeeeee tufahamu kwanini Role Model k...
24/01/2025

Najua umesikiaaaaaa 🧏‍♂️
Yawezekana pengine umeambiwa mengi kuhusu "Role Models"

Twendeeeee tufahamu kwanini Role Model katika maisha

Role Model ni neno lenye maneno mawili ya kiingereza (Role na Model)

Role likiwa na maana Kazi au Shughuli
na
Model likiwa na maana Mfano

Kwa kutumia muktadha wa kimazingira tunaweza kusema *Role Model* maana yake *Mfano wa Kuigwa*

Twendeeeee taratibu...........

Role Model ni mtu ambaye ana sifa, tabia, au mafanikio yanayovutia na kumsukuma mtu mwingine kutaka kuwa k**a yeye au kufuata nyayo zake.

Role Model huwa ni mtu ambaye anaheshimika, ana maadili mazuri, na ameonyesha mafanikio katika maisha au eneo fulani la kazi, elimu, au jamii.

Maana ya Kuwa na Role Model

1. Kichocheo cha Mafanikio.
Role Model hukupa motisha ya kufanikisha malengo yako kwa kukuonyesha kuwa inawezekana kufanikisha ndoto zako.

2. Mwongozo wa Maadili.
Role Model anakusaidia kujifunza na kufuata tabia bora, maadili, na njia sahihi za kufanikisha maisha.

3. Mwelekeo wa Kimaisha.
Role Model anakusaidia kuweka malengo na kuelewa jinsi ya kuyafikia kwa kuiga njia alizotumia kufanikiwa (Yaani kutatua changamoto katika safari ya kutaka kuwa unayetaka)

4. Ushawishi Chanya.
Role Model anakupa ushawishi mzuri unaokufanya kuwa mtu bora, hasa unapochukua mafunzo kutoka kwake.

Mfano wa Role Model anaweza kuwa mzazi, mwalimu, mtu maarufu, kiongozi wa kijamii, au hata rafiki mwenye sifa za kipekee zinazokutia moyo.

Sema nasi Role Model wako ni nani ?

Na

Ni vigezo gani ulitumia katika kumtafuta Role Model wako ?


Address

SUA
Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kiwandanitz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share