28/01/2026
Napata msukumo wa kumuombea Mtu mmoja leo, inawezekana ni Wewe...I don't know, God knows!!
Inawezekana kuna Vita vikali unapigana navyo sirini na unaona kabisa hakuna namna utatoboa!..Sikiliza, keep fighting, keep moving, usiishie njiani, this is for you;
K**a Daniel; utatoka katikati ya hilo tundu la Simba salama, hao simba hawatakudhuru wewe.
K**a Daudi mbele ya Goliath; Mungu atakupa Jiwe dogo, utaliangusha hilo Jitu lenye dharau na kejeli mbele yako, watu watashangaa umewezaje kushinda kirahisi hivyo!
K**a M***a; Mungu atakupa Fimbo, utaigawanya hiyo bahari mbele yako, utavuka ng'ambo na kila kilicho chako, hautaacha chochote nyuma, utawaona Adui zako wakizama mbele ya macho yako.
K**a Ayubu; Utayashinda hayo Majaribu yote. Katikati ya fedheha na maudhi, Imani yako haitotikiswa kabisa.
K**a Esther; utaipindua Mipango yote ya hila dhidi yako, inayopangwa na watu wako wa karibu wenye lengo la kukumaliza wewe na familia yako.
K**a Yusuph; Ndugu zako wanaokuchukia leo, saa inakuja watakupigia magoti. Utasalimika kwenye huo mtego wa mke wa Potifa. Kupitia hilo gereza walilokufunga, wakuu watakujua na kukuita uketi pamoja nao.
K**a Joshua; Jua halitazama mpaka uupate ushindi wako.
Yes, Utashinda tu no matter what!
Wewe ni zaidi ya Mshindi.
Focus don't be distracted!
Christ over Everything!