05/10/2023
Somo la kwanza: Sehemu ya 1
*YAFAHAMU MAJANI TEMBO*
By Charles Philip Dominick
0652807632
[email protected]
Majani maarufu ya Mifugo yaitwayo Majani Tembo
Majani haya yana Majina Mengi k**a vile:
1. Pennisetum purpureum (Jina la Kisayansi)
2. Elephant Grass au Uganda Grass (Jina la kingereza)
3. Mabingobingo (Kiswahili)
4. Napier (Jina Maarufu Zaidi): Jina hili pia limetumiwa Zaidi na walioendeleza mbegu bora za majani haya;
a) Bana: Majani haya yaliitwa “Bana” kutokana na utafiti uliofanywa Africa Kusini, wa kuboresha sifa za majani haya.
Jina “Bana” ni zao la majina ‘Babala’ (Pennisetum Americanum) Pamoja na ‘Napier’ (Pennisetum purpureum). Kwahiyo ‘Ba’ ni Babala, ‘Na’ ni Napier.
Taasisi mbalimbali zimeendelea na kuboresha mbegu za majani haya na kwasasa tuna aina mbalimbali CHOTARA za majani haya zikiwemo;
i) French Cameroon – hii imepatikana baada ya tafiti zilizofanywa Magharibi mwa Africa
ii)Clone 13 – hii imepatikana Kenya kutokana na jitihada zilizofanywa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI).
iii) Kakamega 1 na 2 – Zote aina mbili ni mazao ya utafiti wa kituo cha Utafiti cha Kakamega kilichopo Kenya.
iv) Pakchong 1
V) Juncao
Na nyingine nyingi ambazo siwezi elezea hapa.
*MAMBO YA MUHIMU KUJUA*
1. Majani haya ndio maarufu Zaidi kuliko majani yoyote yale kwenye sekta ya Ufugaji
2. Majani haya ndio yenye wastani mkubwa Zaidi wa uzalishaji wa malisho katika eneo dogo.
3. Majani haya ndio muhimili mkubwa Zaidi wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa
Hujachelewa bado, anza safari nasi, tukufikishe unapopataka.
*Malisho ya Mifugo Tanzania (MAMITA)* , Tupo kwaajili yako
- Kukufundisha
- Kukuuzia mbegu
- Hata ukitaka tutakupandia Malisho
Tutafute kwa *_0652807632_* (Inapatikana Whatsapp)
Somo litaendelea ….