MBUKE TIMES

MBUKE TIMES Mbuke Times ni blog inayokupa mtazamo wa kipekee wa maisha, ujasiriamali, na elimu ya lugha ya kiing

Endelea kujifunza nasi kupitia www.mbuke.blogspot.com Tuna darasa binafsi la mtu mmoja mmoja. Tuinbox upate msaada katik...
05/01/2023

Endelea kujifunza nasi kupitia www.mbuke.blogspot.com
Tuna darasa binafsi la mtu mmoja mmoja. Tuinbox upate msaada katika English.

 Unaweza tumia Awesome k**a kiitikio cha kukubali jambo fulani kuonyesha kufurahishwa na kukubaliana na kilichosemwa.Mfa...
03/01/2023



Unaweza tumia Awesome k**a kiitikio cha kukubali jambo fulani kuonyesha kufurahishwa na kukubaliana na kilichosemwa.
Mfano, mtu anakuambia: I will call you before I leave home – nitakupigia kabla sijaondoka nyumbani.
Wewe unaweza mjibu: Awesome! Yaani umeona hilo wazo lake ni poa sana.

It won't be easy. You will need some waiting time. But if you wait long enough, and do what is required while you wait, ...
26/06/2021

It won't be easy. You will need some waiting time. But if you wait long enough, and do what is required while you wait, you will get the reward. And that's Entrepreneurship.

JINSI YA KUWAFANYA WATEJA WAKUTAFUTE BADALA YA WEWE KUWATAFUTAKuna njia ya kisasa na bora ya kutafuta wateja ambayo k**a...
11/05/2021

JINSI YA KUWAFANYA WATEJA WAKUTAFUTE BADALA YA WEWE KUWATAFUTA
Kuna njia ya kisasa na bora ya kutafuta wateja ambayo k**a ukiifahamu, ukaifanyia kazi kwa kuzingatia miongozo yake utafaidika sana kupata wateja haswa kupata wateja mtandaoni.
Njia hiyo tunaiita Inbound Marketing.
Wazo kuu katika njia hii ni kuwapa walengwa wako machapisho yenye thamani kwao - yaani yenye kuwatoa sehemu fulani kuwaweka sehemu nyingine bora zaidi.
Machapisho yatakua na thamani kwa walengwa wako pale yatakapojibu kero zao, shauku zao, kuwapa miongozo na kuboresha ufahamu wao.
Unapowapa watu machapisho ya thamani unachofanya ni kuwachuja akina nani haswa unapaswa kuwasiliana nao, maana k**a sio walengwa wako, hawatoona yathamani. Pia wewe mwenyewe utajituma kufikiria yale muhimu tuu kwa aina ya watu unaowalenga.
Mfano wewe unauza samaki. mapisho la thamani kwa walengwa wako yaweza kuwa faida za samaki, jinsi ya kuwaandaa samaki, mapishi tofauti ya samaki, jinsi ya kujua k**a samaki wameharibika au la, n.k
Hivyo basi jikite kuchapisha mambo ambayo yanawagusa walengwa wako. Shida ya wajasiriamali wengi wamekua watu wa kufuata mkumbo, kupost kila kitu au kupost wanayoyapenda wao na sio yanayowalenga wateja wao watarajiwa.
Usipopost yanayowalenga wateja wako unaweza jikuta unawavuta kwako watu wengi ambao, kweli wanaweza kulike na kucomment kwenye posts zako, lakini wasije nunua bidhaa zako siku ukitangaza kwakua hao sio watu wenye 'interest' au uwezo wa kununua bidhaa zako.
Lingine la kusisitiza katika njia hii ya kupata wateja ni kuwa na subira. Unahitaji kuweka machapisho mengi, kwa muda mrefu ili ujenge kukubalika, kupendwa na kutegeemewa, kabla watu wenyewe hawajaanza kukutafuta kuuliza unauza nini au wakuulize watapataje bidhaa zako.
Hii ni njia bora sana ya kupata wateja hasa huku mtandaoni ambapo watu wamejaa wasiwasi wa kutapeliwa na kukosa imani na ubora wa bidhaa zinazouzwa.
Machapisho yako bora yatakusaidia pia kujenga brand bora ambayo itakusaidia kuwafanya watu wakuamini, na hata wewe pia uweze kuwa na bei zenye maslahi.
BOFYA LINK uendelee kujifunza mambo ya ujasiriamali kupitia WhatsApp https://chat.whatsapp.com/K3x6eo7Ri9g4TXrEPr6ed7

Jiunge leo kwa group la Ujasiriamali Academy , ambapo kila Alhamis huwa tuna mada muhimu kwako mjasiriamali na wewe unay...
04/02/2021

Jiunge leo kwa group la Ujasiriamali Academy , ambapo kila Alhamis huwa tuna mada muhimu kwako mjasiriamali na wewe unayetaka kuwa mjasiriamali.

Leo tunaenda kujifunza kwa mapana zaidi kuhusu FURSA, maana hamna ujasiriamali bila fursa. Hata hivyo wengi hawajui fursa ni nini, hawajui jinsi ya kutambua fursa, na hata ukishaitambua fursa, ufanye nini ili ikuletee kipato.

Bofya link hii kujiunga: https://chat.whatsapp.com/K3x6eo7Ri9g4TXrEPr6ed7

Kheri ya mwaka mpya 2021. Mungu akujalie furaha, na baraka tele.
31/12/2020

Kheri ya mwaka mpya 2021. Mungu akujalie furaha, na baraka tele.

WAZO LA BIASHARA LA MWAKA!Picha hii kutoka Manizales, huko nchini Colombia inaonyesha Mjasiriamali mwenye  mbuzi wawili ...
31/12/2020

WAZO LA BIASHARA LA MWAKA!
Picha hii kutoka Manizales, huko nchini Colombia inaonyesha Mjasiriamali mwenye mbuzi wawili ambapo hutembea nao mtaani akiuza Maziwa fresh kabisa ya mbuzi.

Ukitaka Maziwa anasimama na kukamua mbuzi wake hapo hapo ukiwa unaona!

Ujasiriamali ni ubunifu na kuthubutu! Je , Mwaka 2020 umekuacha ukithubutu kufanya jambo gani la kipekee k**a Mjasiriamali?

🇹🇿

Wengi wanatumia mitandao kutangaza bidhaa au huduma zao, lakini hawaoni matokeo mazuri wanayotarajia.Siri ya mafanikio i...
29/12/2020

Wengi wanatumia mitandao kutangaza bidhaa au huduma zao, lakini hawaoni matokeo mazuri wanayotarajia.

Siri ya mafanikio ipo kwenye matumizi sahihi ya mitandao katika kujenga imani na brand ya biashara yako na wewe kwanza kabla ya kuwaza kuuza.

Soma points hizi na karibu kwa masomo zaidi na ushauri kupitia WhatsApp 0623 029 683.

MITANDAO YA KIJAMII INAKUINGIZIA KIPATO?Unachohitaji sio tuu kupost bidhaa au huduma zako. Ili mitandao ya kijamii ikule...
27/11/2020

MITANDAO YA KIJAMII INAKUINGIZIA KIPATO?
Unachohitaji sio tuu kupost bidhaa au huduma zako.
Ili mitandao ya kijamii ikuletee faida, unapaswa ujikite kwenye kuwanufaisha walengwa wako kupitia machapisho yako.
Na kingine unahitaji kujikita kwenye kujenga brand bora ili uaminike, na uwafikie watu sahihi, na washawishike kufanya biashara nawe.
Kuna mengi ya kufanya ili ujiweke kwenye nafasi nzuri ya kuaminika, na kushawishi watu. Maandishi ya kile unachotaka kuwaambia watu, ubora wa picha unazotumia ni baadhi tuu ya mambo unayopaswa kuzingatia.
Kwa msaada zaidi tuwasiliane.

MJASIRIAMALI VS MFANYABIASHARA Sio kila anayefanya biashara ni Mjasiriamali. Kumekuwepo na idadi kubwa ya watu wanaojiit...
17/11/2020

MJASIRIAMALI VS MFANYABIASHARA
Sio kila anayefanya biashara ni Mjasiriamali. Kumekuwepo na idadi kubwa ya watu wanaojiita au kuitwa wajasiriamali lakini kiukweli ni wafanyabiashara tuu.

Ili tukue zaidi kiuchumi k**a taifa tunahitaji sana kuwa na wajasiriamali, watu ambao wana kiu na uthubutu kweli kweli wa kutatua changamoto za jamii, watu wenye kuzalisha "thamani" na sio ili mradi tuu kuganga njaa au kujineemesha kifedha.

🇹🇿

NJIA ZA KUPATA JINA LA BIASHARA AU BRAND YAKO ( Sehemu ya 1)Kwenye kupata jina la biashara kuna mambo mawili ya kufahamu...
03/08/2020

NJIA ZA KUPATA JINA LA BIASHARA AU BRAND YAKO ( Sehemu ya 1)
Kwenye kupata jina la biashara kuna mambo mawili ya kufahamu. Kwanza kuna mitindo inayotumika kupata jina, halafu kuna vigezo vya kuzingatia jina unalolibuni linakua navyo ili liwe na mashiko na kukuletea manufaa.

Post hii inaangalia TUU MITINDO ya kupata jina, siku nyingine tutaangalie VIGEZO vya kuzingatia. Post hii ni muhtasari wa mojawapo ya sura za kitabu chetu cha MUONGOZO WA BRANDING KWA MJASIRIAMALI.

Ni muhimu upate nakala yako ya hicho kitabu kina mambo mengi sana yatakayokufanya ujenge brand bora kwa ajili ya biashara yako.

1. Tumia lugha ya kilatini kutafsiri maana fulani
Njia hii inakutaka kwanza uwe na wazo fulani kuhusu jina la biashara. Mfano unawaza kuwa ufungue kampuni ya utalii ambayo itajikita pia na kuhakikisha unatunza mazingira.

Hivyo basi kwakua wazo kuu ni kutunza mazingira, unaingia mtandaoni na kusearch maana ya neno mazingira kwa kilatin, unakuta kuwa na AMET, hivyo unaamua kuiita kampuni yako AMET ADVENTURES. Huu ni mtazamo tuliotumia kumtengenezea mteja wetu wa Kenya hilo jina la biashara yake, ikaitwa Amet Adventures.

Mifano mingine, bila shaka umeona magari yanayotumia jina la AUDI. Hili jina ni la kilatin, ambalo ni tasfiri ya jina ukoo la mwanzilishi wa hiyo kampuni ya AUDI. Yeye mwanzilishi anaitwa August Horch, hivyo alitamani aite kampuni yake Horch ila kwa kilatin, ndio maana akaiita AUDI.

--Somo litaendelea. Na waweza jipatia kitabu chetu cha BRANDING ujisomee mengi kuhusu branding.

HIKI NDICHO CHA KUUZA K**A WEWE NI MJASIRIAMALIUkitambua mbinu hii basi unaweza uza chochote kile na ukapata faida. Acha...
30/07/2020

HIKI NDICHO CHA KUUZA K**A WEWE NI MJASIRIAMALI
Ukitambua mbinu hii basi unaweza uza chochote kile na ukapata faida. Acha kujiuliza ufanye biashara gani, badala yake anza kujiuliza watu wanahitaji nini, watu wana changamoto gani , utoaji mzima wa huduma na uuzaji wa bidhaa zilizopo una changamoto gani.

Siri ya kuuza chochote, ni kutambua changamoto na mahitaji ya watu, ukajua namna bora ya kuwaeleza na kuwaonyesha, na wakaamini unacho cha kutimiza mahitaji yao au kutatua changamoto zao. Unachohitaji sio tuu kumuuzia mteja leo, unahitaji uweze kumuuzia na kesho , na siku zijazo.Unahitaji wateja ambao wataambiana .

Mfano wewe ni fundi seremala, mtu anakuja kukuambia umtengenezee meza ya bei kubwa tuu, tena meza yenyewe sio ya kulia chakula wa kusomea, ni meza tuu itakayokua k**a pambo sebuleni (sitting room) kwake. Ila wewe unaitengeneza bila umakini mkubwa , na kweli unaitoa meza ila haina ubora mzuri wa mtu kuiangalia akaona fahari.

Hapo wewe ulichoangalia ni kuwa mteja anataka tuu meza, haukuwaza hivi kwanini haswa anataka meza. Ila ungejua kuwa anachotafuta mteja ni ufahari na sio tuu meza, usingempatia meza ili mradi, ungejikita kuifanya meza hiyo iwe ya kifahari pia.

Address

Soweto
Moshi
00255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MBUKE TIMES posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to MBUKE TIMES:

Share