Forest Industries Training Institute - FITI

Forest Industries Training Institute - FITI We offer Technician certificate in Forest Industries Technology and various short courses including

01/06/2026

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), Dkt. Tuli Salum Msuya, akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Hosteli ya Wasichana unaoendelea katika Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) Moshi leo, tarehe 01 Juni 2026.

Mradi huo unaofadhiliwa na TaFF umefikia asilimia 35 ya utekelezaji wake na unalenga kuboresha huduma za malazi kwa wanafunzi wa k**e, kuongeza mazingira bora ya kujifunzia Chuoni hapo.

TaFF inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya elimu ili kujenga kizazi chenye ujuzi na uwezo wa kuendeleza sekta ya misitu kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), Dkt. Tuli Salum Msuya,leo tarehe 01 Juni 2026 ameambatana na Mkurugenz...
01/06/2026

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF), Dkt. Tuli Salum Msuya,leo tarehe 01 Juni 2026 ameambatana na Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Edward Kohi, kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Hosteli unaoendelea katika Chuo Cha Viwanda vya Misitu Moshi Kilimanjaro.

Mradi huo unaofadhiliwa na Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) umefikia asilimia 35 ya utekelezaji wake na unatarajiwa kuboresha mazingira ya malazi kwa wanafunzi pamoja na kuongeza uwezo wa chuo kuhudumia idadi kubwa zaidi ya wanafunzi wa k**e.

TaFF inaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za mafunzo katika kuimarisha miundombinu ya elimu na maendeleo ya sekta ya misitu nchini.

Watumishi wa Chuo cha Viwanda vya Misitu leo tarehe 01 Juni 2026 wamepata mafunzo kuhusu Utumishi wa Umma pamoja na Kuzu...
01/06/2026

Watumishi wa Chuo cha Viwanda vya Misitu leo tarehe 01 Juni 2026 wamepata mafunzo kuhusu Utumishi wa Umma pamoja na Kuzuia na Kupambana na Rushwa yaliyotolewa na Bi, Beatrice Chingonikaya mwezeshaji kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Mafunzo haya yamelenga kuimarisha maadili ya utumishi wa umma, uwajibikaji, uwazi na kuongeza uelewa wa watumishi katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa mahali pa kazi.

Mafunzo hayo yameratibiwa na Idara ya Utawala wa Umma na Usimamizi wa Rasilimali Watu ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Chuo Cha Viwanda vya Misitu kimeandaaa Mafunzo ya Muda mfupi kuhusu“Licensed Timber Grading and Inspection Refresher Cou...
29/05/2026

Chuo Cha Viwanda vya Misitu kimeandaaa Mafunzo ya Muda mfupi kuhusu

“Licensed Timber Grading and Inspection Refresher Course”

📅 Tarehe: 15 – 26 Juni 2026
💰 Ada ya Mafunzo: Tsh 1,000,000/=

Mafunzo haya yamelenga kuwajengea washiriki uwezo wa:

Ukaguzi wa mbao kwa viwango vinavyokubalika

Upimaji na upangaji wa ubora wa mbao

Kuongeza ufanisi katika biashara na usimamizi wa mazao ya misitu

Kuhuisha maarifa kwa wataalamu wa sekta ya mbao

📍 Mafunzo yatafanyika katika Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI).

📞 Kwa mawasiliano zaidi:
0658293577 / 0745407388

📧 Barua pepe:
[email protected]
[email protected]

FITI — “Home for Forestry Skills Development

Dirisha la Udahili lipo wazi kuanzia Tarehe 28 Mei mpaka Julai 10 2026.
29/05/2026

Dirisha la Udahili lipo wazi kuanzia Tarehe 28 Mei mpaka Julai 10 2026.

Eid Al Adha Mubarak.
27/05/2026

Eid Al Adha Mubarak.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, ametembelea Banda la Chuo cha Viwanda vya Misitu katika Ma...
22/05/2026

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, ametembelea Banda la Chuo cha Viwanda vya Misitu katika Maonesho ya Nyuki yanayoendelea kwenye viwanja vya Vita mkoani Tabora leo tarehe 22 Mei 2026, ikiwa ni kilele cha maonesho hayo kitaifa.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na chuo katika kuendeleza sekta ya misitu, matumizi endelevu ya rasilimali za misitu pamoja na mchango wa mafunzo ya kitaalamu katika kukuza uchumi wa taifa kupitia sekta ya misitu na ufugaji nyuki.

22/05/2026

Chuo chetu kinatoa Mafunzo katika mnyororo mzima wa mazao ya misitu karibu Chuoni kwetu Upate Mafunzo Bora na yanayokuandaa kutenda zaidi katika Sekta ya Uhifadhi wa Misitu, Matumizi endelevu ya mazao ya misitu na Kuhusu Teknolojia ya Viwanda vya Misitu.

21/05/2026

Tunapokea na Kufanyia Kazi changamoto na maoni yanayotolewa na Wateja wetu pamoja na wadau tunaoshirikiana nao Ili kuboresha zaidi bidhaa zetu na Huduma zetu kwa maendeleo endelevu katika Sekta ya matumizi endelevu ya mazao ya misitu pamoja na Ufugaji wa Nyuki wenye tija.

Address

Forest Industries Training Institute, Box 1925
Moshi

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Telephone

+255787676981

Website

https://www.instagram.com/fiti_moshi?igsh=MW90N2NlM3FlOHlidQ%3D%3D

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Forest Industries Training Institute - FITI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Forest Industries Training Institute - FITI:

Share