05/05/2022
viwavi jeshi vamizi(fallarmyworm)
Viwavi jeshi vamizi ni wadudu waharibifu ambao walianza kuonekana Afrika Mashariki kuanzia mwaka 2016.Wanaweza kuwa na rangi nyeusi, kahawia au kijani
Wanakula mimea zaidi ya aina 80.Wanaharibu zaidi mimea jamii ya nafaka ingawa mazao hayo yakiwa hayapo wanaharibu sana pamba.
Asili na Usambaaji wa Kiwavi jeshi vamizi (Fall Armyworm)
Asili yake ni Amerika ya kati na kusini a -Machi, 2017Mwaka 2016 alionekana nchini NIGERIAZaidi ya nchi 20 za Afrika zimevamiwa na mdudu huyuTanzania alionekana katika mikoa ya Ruvuma,Rukwa na mbeya mwaka 2017Zaidi ya mikoa 20 TZ imeshavamiwa na FAW-Machi, 2018
MZUNGUKO WA MAISHA YA KIWAVI JESHI VAMIZI (FALLARMYWORM

TABIA ZA NONDO WA KIWAVI JESHI VAMIZI
Huonekana kwa urahisi nyakati za usikuAna uwezo wa kuruka umbali kilometa 100 kwa usiku mmojaAnataga mayai 50-200 kwa mafungu Mayai hufunikwa na utando mweupe Mayai huanguliwa kati ya siku 2 hadi 5 kuwa funza Funza hutapakaa kwenye majani na huanza kula majani upande wa chini ya mmea Funza ni waharibifu zaidi muda wa asubuhi sana na jioni Funza hutoa kinyesi kinachomkinga asiliwe na wadudu wengine au sumu isiweze kumfikia
NJIA ZA KUDHIBITI NONDO NA FUNZA WA KIWAVI JESHI VAMIZI
Kagua shamba lako mara kwa mara ili uweze kutambua k**a nondo, mayai, funza au viashiria au dalili za uharibifu katika zao la mahindi na mimea ya nafaka au mipamba na uchukue hatua zinazostahili Kinga mazao kwa kutumia njia za kiutamaduni mfano, weka shamba katika hali ya usafi,tumia mbegu inayokinzana na nondo wa k**a zipo, kilimo cha kubadili mazao au kupanda mimea inayozuia wadudu wasiingie shambani Ondoa masalia ya mimea ya mimea baada ya kuvuna na choma moto Tumia mitego yenye mtego wa maji yenye harufu ya kipepeo jike, hivyo kuwa na uwezo wa kuvutia madume na mara yanapoingia yanakufa.

VIUADUDU VINAVYOWEZA KUDHIBITI KIWAVIJESHI VAMIZI
Alpha-cypermethrin 10EC (systemic)lambda-cyhalothrin 5 SC au 100CS (Contact)Indoxacarb 14.5 EC au 150 EC/SL