03/07/2026
DONDOO KUMI MUHIMU ZA KUZINGATIA KATIKA UANDISHI WA BUSINESS PLAN.
Ili uweze kuwa na business plan nzuri, yenye mpangilio thabiti na kueleweka lazima iwe na vitu 10 muhimu sana. Ambavyo usipo viweka basi plan yako itakuwa na mapungufu.
Kutokana na mtiririko wa elimu tunayotoa kila siku, basi huu ni muendelezo wa elimu hiyo ambayo hii tunadadavua vitu hivyo muhimu vinavyo jenga taswira ya plan yako.
1. MUHTASARI.
Hii ni sehemu moja muhimu ya business plan ambayo inaelezea kwa ufupi na kwa undani kitu ambacho kipo kwenye plan, na ubeba ujumbe kamili juu ya lengo la mradi.
2. MCHANGANUO WA BIASHARA.
• Kuelezea bidhaa na huduma zitakazo tolewa.
• Historia fupi ya kiwanda au kampuni au mradi
• Lengo la mradi husika.
• Upekee wa bidhaa au huduma zitakazotolewa.
3. MASOKO.
• Utafiti na uchambuzi
• Onesha wateja ulio walenga katika mradi huo.
- Onesha ukubwa wa soko na mwenendo wake.
- Onesha ushindani wa soko husika.
- Onesha makadirio ya Hisa.
• Mpangilio wa masoko
- Onesha mpango mkakati katika uuzaji.
- Onesha mpango mkakati katika uuzaji.
- Onesha bei ya kila bidhaa au Huduma zitakazotolewa.
- Onesha mpango mkakati wa matangazo na promosheni.
4. UTAFITI, MBINU, NA MAENDELEO.
• Onesha mbinu na maendeleo.
• Onesha matokeo ya tafiti za kiufundi.
• Onesha mahitaji ya kitafiti.
• Onesha gharama zitakazotumika katika kufanya tafiti.
5. UZALISHAJI.
• Onesha eneo mradi utakapo endeshwa.
• Onesha mahitaji ya uzalishaji k**a vifaa na vitendea kazi.
• Onesha mfumo wa usafirishaji na usambazaji.
• Onesha nguvu kazi itakayotumika kwenye mradi (wafanyakazi).
• Onesha gharama ya uzalishaji.
6. UTAWALA.
• Onesha muundo wa utawala.
• Onesha timu nzima ya uongozi kwa kuonyesha mtendaji mkuu.
• Onesha muundo wa kisheria kwa kuonyesha makubaliano ya kihisa na mikataba ya waajiriwa.
• Onesha bodi ya wakurugenzi na washauri.
7. HATARI MUHIMU KATIKA MRADI.
• Ainisha matatizo yasiyozuilika.
• Onesha vikwazo hatarishi.
• Onesha njia mbadala za utatuzi wa matatizo.
8. FEDHA.
• Utabiri wa kifedha
- Onesha taarifa ya faida na hasara. (Profit and Loss report)
- Onesha taarifa mizania (balance sheet).
- Onesha mzunguko wa fedha (cash flow).
- Onesha udhibiti gharama (cost controls)
• Onesha vyanzo na matumizi ya fedha.
• Onesha mpango wa bajeti.
• Onesha hatua za uwezeshaji.
9. ONESHA HATIMA YA MRADI.
• Onesha malengo ya mradi.
• Onesha ukomo wa mradi.
• Onesha uhusiano wa matukio.
10. VIAMBATANISHO (Appendix and/or Bibliography Segments)
Kipengele hiki utoa nafasi ya kutoa maelezo ya ziada ambayo hayakuchambuliwa kiundani katika sehemu husika za ripoti hapo mwanzo, k**a vile michoro, miongozo, taarifa za kifedha ( financial data) n.k.
KUMBUKA: "Kufanya biashara bila mpango kazi (business Plan) ni sawa na kuendesha gari isiyo na taa gizani"
KUPATA BUSINESS PLAN YENYE UBORA WASILIANA NASI KWA NAMBA:
+255 785 494 456
+255 753 494 456
Barua pepe: [email protected]
Nyumbani Business Plan LTD