02/05/2022
BINTI WA RAIS....01
NA PROFESA HOODU DE CHWAAA (HAMZA H JAFARI)...
FROM TEAM BECAUSE OF LOVE....
OFFICIAL WHAT'S UP NO;;;0746-000 672
Telegram Group👇👇👇👇
https://t.me/HADITHI_MPYADAIMA
OFFICIAL FACEBOOK GROUP.👇👇👇
https://www.facebook.com/groups/296808098705100/?ref=share
BISMILLAH RAHMAN RAHIIM:-
DONDOO MUHIMU...
INASEMEKANA ITAKUWA...KWA WALE AMBAO WATABAHATIKA KUFIKA MWAKA 2030 WATASEMA ILIKUWA...NA HUU NI UTASHI WANGU BINAFSI MWANDISHI Na sio uhalisia...NAMI NAIFANYA KUWA 2025 CHIMBUKO LA KISA HIKI KUWA ILIKUWA...
ANZA NAYO...
Mnamo Tarehe 30/12/2025 nchini Tanzania kulikuwa na Harusi ya kifahari baina ya wapenzi wawili waliopitia misuko suko mingi sana,lakini walipambana sana kutokea kwenye ufukara na sasa vijana hao wamegeuka kuwa matajiri wakubwa nchini Tanzania na nyota maarufu kutokana na umaridadi wao katika kiwanda cha Tasnia ya filamu!Ushiriki wao katika filamu bora na pendwa ya "WA KIBAIGWA," ambayo inasimamiwa na kikosi cha siri cha "NINJA MTETEZI,"ambao ndio waliiongoza misheni ya kuikomboa nchi isiweze kuchukuliwa mikononi mwa Mheshimiwa rais SALMA MAALIMU HAYDARI kwenda kwa walowezi waliokuwa wamefadhiliwa na mfaransa Ruben Teller Nicholus(Ruteni) katika jaribio lao la kuipindua serikali hiyo ya mwanamama shupavu na hodari kutoka ardhi ya taifa la upendo;inasemekana ndio miongoni mwa sababu kubwa ya wawili hao kuwa matajiri.
Sababu nyingine ya utajiri wao,ni ule uwezo binafsi wa bwana harusi katika masuala mazima ya uwezo wa kucheza ngumi za Taekwondo,ambapo mnamo miezi michache kabla ya Harusi yake,kijana huyo alitwaa ubingwa wa Dunia katika mashindano yaliyofanyika nchini Italia.Sababu ya tatu ,wawili hawa walikuwa ni wana IT mashuhuri huku bibi harusi akiwa amehitimu cheti cha Shahada katika fani ya sayansi ya kompyuta na injinia yake,kule bwana Harusi akiwa anacheti maalumu cha Teknolojia ya Habari na mawasiliano kutokea nchini Ufaransa!Bwana harusi alikwenda mbali na kupata cheti cha heshima cha The Special Geneos!Aliidhihirishia Dunia juu ya hilo,baada ya muvi yao kupigwa marufuku na platform kubwa za mauzo mtandaoni kukipinga kile ambacho ninja mtetezi walikusudia kiwafikie waafrika,kwa kisingizio cha kuchochea ubaguzi.Mwana Tehama huyo,alizindua mfumo wake mpya na kuutumia kuiuza filamu hiyo ambayo sasa ilisambaa Dunia nzima na watu kuisifia sana.
Wanaharusi hao alikuwepo HAMZA JAFARI na bibie HUSNA MUSOMAZ!Ndani ya ukumbi huo huo waliokuwepo nyota hao,rafiki yake kipenzi HAROLD CHALIMWA alisherehekea kwa pamoja harusi yake baada ya kumuoa JULIETA DICKSON MTIZWA.Harold pia alishiriki katika filamu pendwa ya WA KIBAIGWA!Huku yeye akiwa muhitimu wa Shahada ya injinia ya Elektronia(Electionicks) katika chuo kikuu cha DAR ES SALAM INSTITUTE OF TECHNOLOGY (DIT)!
Ukiachana na Hayo yote,kubwa zaidi, mheshimiwa rais alitakiwa kuhudhuria sherehe hizo za vijana hawa.Lakini ghafla aliipata dharura ambayo ilimfanya amtume makamu wake akamuwakilishe,kisha yeye akatimkia nchini Kenya!
Kuna siri kubwa sana hapa.Siri hii ni ngumu sana kuijua.Siri hiyo ndio chanzo chetu cha kisa hiki cha Binti wa Rais; Mrembo maarufu mitandaoni kwa jina la JASMINE TZ kinaanzia!
Kwa ufupi tuu,mrembo huyu alitokea kumpenda sana Hamza JAFARI toka walipokutana katika masomo ya katika chuo kikuu cha Paris-saclay,mume wa Husna kwa sasa!Ambapo,awali ya wote,Husna na Jasmine walikuwa marafiki wakubwa mnoo.Hapo mwanzo zilinza k**a tetesi ya kuwa,Hamza anatoa kimapenzi na Husna.Baadaye ikaja taarifa kwamba itakapofika mwezi wa 12 tarehe 30,Husna ataolewa.Katika chunguzi zake,akabaini,mtu anayekwenda kumuoa Husna ni Hamza wake.Binti wa Rais alipaniki,akaadhimia lazima afanye kitu kuisambaratisha ndoa hiyo isifanyike.Kwa bahati mbaya sana kwake,mpango wake ulish*tukiwa na Hamza,ambaye kiuhalisia,yeye ndiye kiongozi mkuu wa NINJA MTETEZI!Hivyo mnamo tarehe 29 ya mwezi huo, Jasmine alistaajabu kuk**atwa na Kg 1.15 ya madawa ya kulevya nchini Kenya alipokuwa anajiandaa kusafiri kwenda Nchini Dubai kwenda kukutana na mpenzi wake Hamza!Kitu ambacho hata yeye hakuelewa hilo liliwezekanaje ikiwa hafahamu chochote kuhusu biashara hiyo.
Mheshimiwa rais alimtumia balozi wake amsaidia kuzungumza na serikali ya Kenya wamuachie Binti yake,lakini balozi aligonga mwamba.Hii ndio sababu ya mheshimiwa rais kutimkia nchini Kenya na kuachana na harusi!
****&*****&******&*****&****
Ndege ya Air Tanzania aina ya Air bus A220-300,ilionekana iking'ata ardhi ya uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta kwa kasi ya hatari.Gari za zima moto zilionekana kuifuata kwa nyuma kwa ajili ya tahadhari kusijepatikana madhara yeyote ikiwa kuna bahati mbaya yeyote itajitokeza.
Baada ya ndege hiyo kusimama,vikosi vya wanausalama viliizingira,kisha alionekana mheshimiwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania akiteremka kutoka kwenye ndege hiyo kubwa na nzuri mali halali ya taifa lake.Aliingia kwenye gari maalumu aliloandaliwa,kisha msafara wake ukaondoka pale uwanjani.
Ilikuwa ni safari ya Ghafla,na ya kushangaza,huku hakuna yeyote aliyethubutu kusema wala kujua mheshimiwa rais alifuata nini nchini Kenya.Hata hivyo,habari hii ilivujishwa na mashirika ya habari makubwa ya kimataifa baada ya kuzinasa picha kadhaa kupitia waandishi wao wapelelezi.
****&*****&********
"Namjua vizuri sana binti yangu,nafahamu ni miongoni mwa watu waliochachuka sana kwenye mitandao ya kijamii!Lakini ni muadilifu sana kwenye maisha ya kawaida!Hawezi katu kujihusisha na biashara hiyo haramu.Maana ni mchumi mzuri ambaye anapambana kila siku na jitihada zake naziona...Naomba uchunguzi huu ufanyike haraka sana na kwa haki kupitia vikosi vyetu kushirikiana,ikiwa atakutwa na hatia,nipo radhi anyongwe,ikiwa hatakutwa na hatia,basi aachiwe huru haraka iwezekanavyo!"Ilikuwa ni sauti ya upole, unyenyekevu na utulivu ya mheshimiwa rais wa Tanzania,alipofanikiwa kukutana na Rais wa Kenya kwa ajili ya mazungumzo.
"Tanzania na Kenya ni marafiki wa muda mrefu,tumekwishachonganishwa sana!Lakini katu hatuwezi hifadhi chuki zetu.Hili ni dogo sana dada yangu.Ninachotaka ni haki itendeke,ili hata k**a ni kweli kajiingiza kwenye biashara hizo,basi tumsaidie.K**a kachezewa mchezo,tumjue huyo aliyeshiriki upuuzi huu.Sio kwamba nakataa kumuachia binti yako!Ila ni lazima tuujue ukweli wote!"Rais wa Kenya alisikika akiongea kwa busara.
Amir jeshi mkuu wa Tanzania,aliinama na kuyakumbatia mashavu yake.Huzuni ilimfika pabaya.Aliwaza sana,ni wapi alipokosea kumpa malezi binti yake mpaka ajihusishe na usafirishaji wa madawa ya kulevya!Amekosa nini binti yake hadi hali iwe hivyo!Hakika Jasmine Tz ndiye kipenzi chake.Huyo ndiye mziwanda wake.Loooh!Tumbo la uzazi alilisikia likimkata.Kuna muda aliona presha inataka kumpanda,mara alihisi inashuka.
"Tayari,"Ni sauti ya afisa mmoja wa usalama ndiye iliyemsh*tua mheshimiwa rais kutoka kwenye rundo la mawazo.Akasimama yeye na mwenyeji wake kwenda kwenye chumba maalumu walichokuwa wameandaliwa kwa ajili ya mkutano wa kuijadili taarifa za uchunguzi wa awali uliofanywa kwa kushirikiana kwa wapelelezi wa Tanzania na Kenya.
Taratibu za ufunguzi wa mkutano huo zilifuatwa,kisha mkuu wa upelelezi wa kitengo hicho kilichokabidhiwa misheni alianza kuisoma taarifa hiyo, "..... Inaonekana tarehe 28, Jasmine alituwa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta majira ya jioni akitokea nchini Afrika Kusini,kisha akakata tiketi ya ndege kwa ajili ya kujiandaa na safari ya Kesho yake kwenda Dubai!Tulipomfanyia mahojiano ya toka awali na mpaka sasa, mtuhumiwa hakusita kuweka bayana ukweli huu.Hii imeturidhisha kwamba,hakuwa na mpango wala nia yeyote ya kutuongopea,"alinyamaza kidogo kisha akafunua ukurasa mwingine.
Macho yake yalitua kwenye karatasi hiyo huku ukumbi wote ukiwa kimya na sikivu kwa kila alilotamka.Alikohoa kidogo ndipo akaendelea, "Tulimuuliza mtuhumiwa namba moja,baada ya kutoka uwanja wa ndege alielekea wapi?Alisema hakuenda sehemu yeyote zaidi ya Amadwala Lodge,ambapo gharama yake ni sawa na shilingi 123,900/= za kitanzania.Alidai alifika hapo kwa ajili ya kupumzika na kupata mlo wa jioni! Tumefuatilia kwa umakini,tukaona ni sahihi kabisa wala hakudanganya.Kesho yake Asubuhi alinyooka moja kwa moja uwanjani kwa ajili ya safari yake,akakutwa na kidhibiti hicho.Hapo ndipo tulipoanza kujenga wasiwasi,inawezekana vipi mizigo aliyopita nayo siku ya jana ilikuwa salama halafu leo ikutwe na kasoro?"
"Kwa ushirikiano mkubwa sana,tukaamua kuipekuwa Amadwala lodge maana ndipo mahali kulipoonekana kuna tatizo.Yafuatayo ndiyo tuliyoyabaini,"akanyamaza kidogo kisha akautizama uongozi wake.Mheshimiwa rais alionekana akitikisa kichwa kwa shauku ya kutaka kusikia, "mnamo majira ya saa mbili na nusu usiku, "aliendelea kuisoma taarifa ile, "Jasmine Tz na walinzi wake walitoka na kwenda kwenye ukumbi wa chakula.Walipokula,walizungukia upande wa baa kwa ajili ya kutizama burudani zilizokuwa zikiendelea eneo hilo.Saa tano kasoro robo,walirejea nyumbani kwao kulala.Lakini kuna kosa ambalo walitenda bila wao kujua.Kwani,kwa muujibu wa Cctv Camera zilizofungwa pale,zilifanikiwa kumuonesha mzee mmoja aliutumia mwanya ule wa akina Jasmine kutoka,akaingia chumba cha Jasmine kwa kufungua kitasa kwa mbinu za kijasusi."
"Pamoja na kwamba mtu yule alikuwa na sura ya kizee,lakini tembea yake ilionesha kabisa alikuwa anaigiza!Hii inatupa wasiwasi kwamba mtu yule alivaa kinyago maalumu cha sura bandia!Mzee huyo alionekana akitoka na kuurudishia mlango ule kwa umakini,kiasi kwamba hata Jasmine na walinzi wake waliporudi hawakungundua chochote kwamba walivamiwa.Hivyo basi,tunathibitisha kwamba,mzee huyu ndiye aliyepandikiza madawa ya kulevya kwenye mizigo ya Jasmine.Uhakika huu unakuja,baada ya kufanya mahojiano ya kina na vijana wetu waliowak**ata watuhumiwa hawa,ambapo walisema,walilazimika kuweka umakini baada ya kupatiwa taarifa kwamba kuna watu wanampango wa kusafirisha mihadarati kupitia uwanja huo kwenda Dubai.Mtoa taarifa alikwenda mbali,na kuelezea namna watu hao walivyo walivyo.Na kweli,ndani ya nusu saa Jasmine Tz alifika akiwa kaongozana na walinzi wake.Walipopekuliwa walikutwa na madawa hayo ya Kulevya!"
Msoma taarifa alisimama kusoma na kuhema kwa nguvu,akarejesha macho kwenye ukurasa mwingine na kuendelea, "Taarifa za uchunguzi zinaonesha,Mzee yule alifika dakika tano baada akina Jasmine kufika pale.Akamtaka muhudumu ampe kwanza daftari la kujaza taarifa za wateja,kisha akaanza kujaza.Akamuuliza muhudumu,ni chumba gani kipo wazi kati ya 107 mpaka 111? Muhudumu akamuambia,ni 111 pekee!Mzee yule akajaza chumba hicho.Akalipa pesa yake,huku akijaza yeye ni mfanya biashara kutokea Naivasha.Ajabu inakuja pale ambapo mzee huyo aliaga majira ya saa tatu na robo kuwa kuna mahala anakwenda,atachelewa kurudi,lakini hakurudi jumla.Hii nayo inatudhihirishia kwamba mzee yule alifika pale kwa lengo maalumu,hivyo alivyotekeleza,hakuona sababu ya kuendelea kubaki.Moja ya vitu vinavyotuchanganya ni kwamba mzee yule alifika pale kwa miguu!Mpaka sasa hatujajua mzee huyo yupo wapi?Anaishi wapi?Na ni kwa nini alifanya hivyo!"
"Kwa haraka haraka tuu,tukio hili tunalihusisha na mipango ya Wazungu,katika moja ya hatua za Muendelezo wa kumshinikiza rais wa Tanzania kuwaachia huru akina Ruben Teller Nicholus(Ruteni) na wenzake,kufuatia kesi yao ya uhaini inayowakabili mahak**ani.Sisi k**a wapelelezi wa tukio hili,tunatoa ushauri wa kumuachia huru binti wa Rais,kwa sababu,kuwa kwake huru hakutatupoteza kwenye chunguzi zetu,bali kutatuletea ukaribu wa kuwanasa maadui wanaojaribu kumzunguka mrembo huyu k**a kichaka cha kujitetea,kisha tutawak**ata na kuchukua hatua stahiki kuweza kufahamu haswa ni nini chanzo! Tunaahidi kuwa,katika kila hatua atakayoipiga binti yako nje ya ngome yako,kutakuwa na walinzi wa siri wanamfuatilia!Ahsanteni kwa kunisikiliza!"
Makofi yalisikika yakiupongeza uchunguzi huo.Baada ya hapo marais hawa walizungumza kwa pamoja.Kisha wakafikia muafaka kwamba, Jasmine Tz atarudishwa nchini Tanzania tarehe 01/01/2026!
****&***&***&***********
Jasmine Tz alikuwa na furaha kubwa kuachiwa huru.Wasi wasi wake mkubwa ulikuwepo juu ya mpenzi wake Hamza ambaye alihusika kumpa mipango kazi ya safari yake kutoka Afrika Kusini kwenda kukutana Dubai tarehe 29 kwa ajili ya kutekeleza ahadi yao ya kwenda kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza toka wajuane!Ililazimika kuwe na mizunguko mirefu ili kupoteza maboya,kwani,ilihitajika usiri mkubwa sana kwa ajili ya kuutetea uhasama wa kijana huyo na mheshimiwa rais.Hamza alimsisitiza,ikiwa atakosea hatua hata moja tuu,basi,kesho yake tarehe 30 atampa adhabu kali ambayo hatokuja kuamini maishani mwake.Lau k**a angelish*tuka mapema,basi ni heri angeutumia ule mpango wake A kuivuruga harusi ile,kuliko mpango huu B alioupanga baada ya Hamza kujaa kwenye 18 zake.Ama hakika siku zote,ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu!
Sasa amekwishakosea,hawakufanikiwa kuonana Hamza wake!Je,Hamza wake atamuelewa?Hilo lilimpa wasi wasi.Hivyo alikuwa na shauku ya kutamani kuongea na mpenzi wake kisha amsimulie madhira yaliyomkuta na kumuomba msamaha!
"Simu zako hizi hapa,huo ujinga jinga wako usirudi Mxciuuuu!"Mheshimiwa rais alisikika akimsonya mwanaye wakati anampatia simu zake.
"Kaaah mama...Si yamekwisha!"Alideka mrembo yule huku akifurahi kupatiwa simu zake.
"Wewe kenua tuu mimeno yako,umenitia hasara litoto wewe...!"Alimkazia uso huku akimuoneshea kidole cha shahada.
Jasmine Tz aliwasha simu yake,kisha aliwashwa kupekuwa kwenye mtandao wa Instagram.Alipoingia tuu alikutana na picha ya Husna akiwa katika mkao wa Kimahaba na Hamza wake.Kwa mara ya kwanza aliuona moyo wake unamvuta na kutaka kuchomoka.Alijikaza na kujaribu kusoma ujumbe ulioandikwa,ingawa mandhari yale aliyatambua kwamba ni Dubai kwenye hoteli ya Jumeirah,lakini alitaka kujua zaidi!"TUNAMSHUKURU Mungu, Fungate letu linazidi kunoga siku hadi siku!"Baada ya kuusoma ujumbe huu,alianza kutetemeka.
"Mama,hivi Hamza JAFARI alifunga ndoa?"
"Ndio,haujapata tuu habari.Nasikia harusi yao ilifana kweli!"Mheshimiwa rais alimjibu binti yake pasina kuelewa anamuumiza kwa kiwango gani.Ghafla alimshuhudia mwanaye akisimama,lakini alipojaribu kuunyanyua mguu wake apige hatua,alishindwa na kuanguka chini k**a mzigo na kusikika kwa mshindo wa "Tiii!"....Pale pale alipoteza fahamu!
Ha-haaaaa....haiyaaa sasa...Ngoma ndio kwanza inaanza...Picha linaanza Rasmi...Karibuni sana ndugu zangu nyote because of love...Nawasihi msitokee...!!!Tuwe pamoja mwanzo mwisho...
ITAENDELEA...