05/12/2016
"Hydroponics" ni utaratibu wa kuotesha mimea kwa kutuma Maji kidogo bila kuhusisha mchanga /udongo kabisa. Mimea inaoteshwa katika chombo maalumu "Tray" ambacho ni kisafi na kina matundu chini ili kusaidiana Maji yasituame chini wakati wa umwagiliaji mimea.
Dairy Link Tanzania inatoa mafunzo na kufunga "hydroponics fodder" kwa wafugaji wa ng'ombe, mbuzi, kuku na sungura. hii itamsaidia mfugaji kupunguza gharama ya malisho ya mifugo yake kwa asilimia hamsini (50%) na kuongeza uzalishaji kwa asilia sabini (70%) kwani Hydroponics fodder humfanya mnyama kushiba vizuri pia kupata kiwango bora cha virutubisho vinavyohitajika ili kuongeza uzalishaji na ukuaji kwa matokeo mazuri kiafya. Pia eneo dogo la kufunga mfumo huu linakuwezesha kupata chakula cha kutosha mifugo yako.
Ukitaka kufungiwa mfumo huu tafadhali wasiliana nasi tukuhudumie kwa gharama nafuu.
Karibuni wote!
[email protected]