22/02/2024
KATI YA SERIKALI NA TANESCO NANI NDIYE CHANZO CHA MGAWO WA UMEME??
Siku chache zilizopita kulitoka tamko kwamba mgawo wa umeme ambao sasa unamaliza mwaka tangu ulipoanza unaweza kuisha tarehe 16. Haikusemwa ni tarehe 16 ya mwezi ama mwaka gani na ndiyo maana siku chache baadaye mtu yule yule aliyetangaza mwisho wa mgawo kuwa ni tarehe 16 akaibuka na kujitetea kwamba HAKUTAJA TAREHE YA MWEZI GANI NA MWAKA GANI.
Kwa kuzingatia tamko tu hili la SERIKALI kuhusiana na tarehe ya kumalizika kwa mgawo mkali wa umeme tunalazimika kujikumbusha baadhi ya mambo ili tumfahamu MTAALAMU WA MGAWO WA UMEME ni nani kati ya Serikali na TANESCO yake.
Ukisoma Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwenye kipengele cha ahadi ambazo watahakikisha serikali yao inatekeleza endapo CCM itapata ridhaa ya kuunda hiyo serikali utaona kwamba WALIAHIDI KUONGEZA MEGAWATII 3607 ili kufikia kiwango cha uzalishaji wa umeme kinachofikia Megawati 4915 KUFIKIA MWAKA 2020. Katika Ilani ile ya uchaguzi waliainisha jinsi watakavyopata hizo Megawati 3607 za nyongeza.
Halafu WAKAPATA RIDHAA iwe kiharamu ama kihalali na ghafla WAKABADILI GEA ANGANI. Wakaamua KUVITUPILIA MBALI UTEKELEZAJI WA VYANZO WALIVYOAHIDI KWENYE ILANI YAO YA UCHAGUZI ambavyo vingi vilikuwa vikilenga kutumia GESI ASILIA kutoka Mtwara na Songosongo na badala yake WAKAINGIA KWENYE UHARIBIFU WA MAZINGIRA PALE RUFIJI.
Wakati wakianza uharibifu wa mazingira pale Rufiji wakaahidi kwamba kufikia mwezi September mwaka 2021 TAYARI WATAANZA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA MAJI unaofikia Megawati 2100. SEPTEMBER IKAWA SEPTEMBER 2023 na sasa tupo mwezi February mwaka 2024,MTAMBO WALIOAMUA KUUPA JINA LA JULIUS NYERERE kutoka Stigler's Gorge HALIJATOA HATA ROBO MEGAWATI na tunachosikia mpaka wakati huu ni MARA BWAWA LIMESHAJAA MAJI,WANAMALIZIA MAJARIBIO YA HAPA NA PALE n.k
Ndipo TANESCO kwa kauli moja WAKAIBUKA NA TANGAZO LA MGAWO. Wale wa Tanga,Arusha na kwingineko hawakukutana nao sana isipokuwa sisi wa Kilimanjaro,Dar es salaam n.k NDIO TUMEKUTANA NAO SANA MPAKA SASA. Mwezi October 2023 Raisi wa JMT akaibuka na AMRI kwamba ANAWAPA TANESCO MIEZI SITA wahakikishe MGAWO WA UMEME UMEKWISHA. Kimsingi mwezi wa sita wa AGIZO LA RAISI umebakiza siku takriban TATU tu na kinachoonekana sasa ni MGAWO KUUMA ZAIDI.
Hapo nyuma sababu za MGAWO ZILISEMWA ni kutokana na vyanzo vinavyozalisha kwa maji kutokuwa na maji kutokana na UKAME. Baadaye baada ya mvua kunyesha mpaka kusoma kijiji kule HANANG TANESCO wakaibuka na hoja kwamba sasa MGAWO UNASABABISHWA NA MIUNDO MBINU YAO KUSOMBWA NA MAJI YA MAFURIKO.
Kwa hiyo,KIMSINGI sababu za MGAWO WA UMEME HAZIJULIKANI HASA NI NINI. Baadhi ya wadau WANAOZALISHA UMEME niliobahatika kuzungumza nao wanasema kwamba TANESCO ILIKATAA KUNUNUA UMEME KUTOKA KWAO MPAKA IKULU ILIPOINGILIA KATI ndipo wamekubali ingawa itachukua muda kwa wadau hawa kuweza kuanza kuuza umeme huo kwa TANESCO.
Kwa namna yoyote ile MGAWO WA UMEME hapa nchini si suala la BAHATI MBAYA bali ni MIPANGO MADHUBUTI YA WANAOTAKA KUMTAFUTIA MAMA SAMIA SIFA YA KUMALIZA MGAWO. Pengine ni mbinu ya kutafuta HURUMA kwa mwendazake JPM.
BADO TUNAISOMA NAMBARI.