31/05/2018
Hatua tano (5) za mzunguko wa biashara ambazo kila mfanyabiashara au mjasiliamali anapaswa kuzifahamu, ili zimuwezeshe kutatua changamoto atakazokutana nazo katika kila hatua.
1. WAZO LA BIASHARA
2. KUANZA KWA BIASHARA
3. UKUAJI / KUKUA KWA BIASHARA
4. KUPANUKA KWA BIASHARA
5. KUKOMAA KWA BIASHARA
Katika hatua zote hizi hazina wakati maalum kutoka hatua moja kwenda nyengine, inategemea na biashara au mtu/watu – wanaofanya biashara hiyo.
WAZO LA BIASHARA
Wazo la biashara likiambatana na nia ya biashara ni jambo la msingi katika kuanzisha biashara, ambavyo kwa pamoja vitakupa matokeo yanayoweza kuwa aidha hasi au chanya.
Mara nyingi wazo zuri la biashara hutokana na changamoto zinazowakabili watu / jamii Fulani. Changamoto k**a ukosefu wa maji, usafiri, chakula, malazi, vifaa vya ujenzi, madawa, elimu, mawasiliano na kadhalika
Zingatia sana yafuatayo wakati ukijiuliza ni biashara gani ya kufanya
1. Nia ya kufanya biashara
Nia ya kufanya biashara itapatikana kwa kufanya kitu/jambo unalopendelea zaidi, kwani unakuwa unautayari wakati wowote bila ya kusukumwa na mtu yeyote yule. Unapofanya kitu ukipendacho zaidi na kukigeuza kuwa biashara utakuwa una asilimia nyingi zaidi kufanikiwa kwani utafanya kwa ufanisi na umakini wa hali ya juu zaidi.
2. Uhalisia/Kuwezekana
Usiwaze biashara ambayo kiuhalisia haiwezi kufanyika kwani utaishia kupanga kila siku na hutofanikisha lengo lako, pia biashara unayowaza hakikisha itaendana na Maisha yako halisi isije ikawa sababu ya kuharibu Maisha yako binafsi.
3. Ufahamu
Siku zote chagua biashara ambayo utakua na ufahamu nayo au biashara ambayo utakua unaujuzi nayo. Kwa kufanya hivyo itakua rahisi kwako kusimamia kiukamilifu biashara yako kwa urahisi.
4. Wakati sahihi
Biashara inahitaji wakati ulio sahihi ili iweze kuendana na wakati uliopo, usiwaze biashara ambayo ingeweza kufanya vizuri zaidi miaka kumi (10) iliyopita
5. Mazingira sahihi
Unaweza ukawa na wazo zuri la biashara lakini mazingira yakakufanya ukapata matokeo hasi, hivyobasi ni vyema ukachagua mazingira ambayo yatakua rafiki kwa biashara yako ili kuepuka kutumia nguvu kubwa katika kutekeleza biashara yako
6. Mtaji
Si kila biashara zinahitaji fedha ili kuweza kuanzishwa, hivyo basi ni vizuri kuainisha namna ambayo unaweza kupata mtaji wa biashara yako.
Ni vyema ukawa na mawazo tofauti/mengi ambayo yanaweza kufanana au kutofautiana, ila hakikisha mawazo yanayofanana yatatofautiana katika utekelezaji wake.
KUANZA KWA BIASHARA
K**a mfanya biashara au mjasiliamali unapaswa kuiheshimu biashara yako. Unapoanza biashara ni muhimu kuwa umeshakamilisha mambo muhimu ambayo biashara yako inahitaji/itahitaji ili kuweza kuendelea/kuwa na muelekeo mzuri.
Mambo ya msingi unayo hitaji kufahamu wakati wa kuanza biashara yako
1. Nia ya kufanya biashara
Nia ya kufanya biashara itapatikana kwa kufanya kitu/jambo unalopendelea zaidi, kwani unakuwa unautayari wakati wowote bila ya kusukumwa na mtu yeyote yule. Unapofanya kitu ukipendacho zaidi na kukigeuza kuwa biashara utakuwa una asilimia nyingi zaidi kufanikiwa kwani utafanya kwa ufanisi na umakini wa hali ya juu zaidi.
2. Uhalisia/Kuwezekana
Usiwaze biashara ambayo kiuhalisia haiwezi kufanyika kwani utaishia kupanga kila siku na hutofanikisha lengo lako, pia biashara unayowaza hakikisha itaendana na Maisha yako halisi isije ikawa sababu ya kuharibu Maisha yako binafsi.
3. Ufahamu
Siku zote chagua biashara ambayo utakua na ufahamu nayo au biashara ambayo utakua unaujuzi nayo. Kwa kufanya hivyo itakua rahisi kwako kusimamia kiukamilifu biashara yako kwa urahisi.
4. Wakati sahihi
Biashara inahitaji wakati ulio sahihi ili iweze kuendana na wakati uliopo, usiwaze biashara ambayo ingeweza kufanya vizuri zaidi miaka kumi (10) iliyopita
5. Mazingira sahihi
Unaweza ukawa na wazo zuri la biashara lakini mazingira yakakufanya ukapata matokeo hasi, hivyobasi ni vyema ukachagua mazingira ambayo yatakua rafiki kwa biashara yako ili kuepuka kutumia nguvu kubwa katika kutekeleza biashara yako
6. Mtaji
Si kila biashara zinahitaji fedha ili kuweza kuanzishwa, hivyo basi ni vizuri kuainisha namna ambayo unaweza kupata mtaji wa biashara yako.
Ni vyema ukawa na mawazo tofauti/mengi ambayo yanaweza kufanana au kutofautiana, ila hakikisha mawazo yanayofanana yatatofautiana katika utekelezaji wake.
UKUAJI / KUKUA KWA BIASHARA
Katika hatua ya ukuaji wa biashara ni wakati ambao mfanyabiashara/mjasiliamali anatakiwa kuwa na umakini wa hali ya juu sana kwani ndio wakati ambao unaweza kujutia maamuzi yako ya kufanya biashara hiyo. Katika ukuaji huo unaweza pitia/kufuata hatua zifuatazo
1. Uwepo kwa biashara
Ili biashara iweze uwepo/kuendelea lazima ujitambue na uwe na moyo wa subira. Katika hatua hii utakutana na changamoto nyingi k**a vile namna ya kupata/kuvutia wateja kupenda bidhaa au huduma zako. Pia hii ni hatua ambayo watu wengi hushikwa na wasiwasi k**a wataweza imudu biashara kwani wakati mwingi itakua ikijiendesha kwa hasara.
2. Uhai/Kuishi kwa biashara
Hii ni hatua ambayo biashara inakua na wateja wa kutosha ambao wataiwezesha biashara kujiendesha kwa faida na sio hasara. Tunasema biashara iko hai kwakuwa inaweza kujihudumia mahitaji yake kwa ujumla.
3. Mafanikio
Katika hatua hii mjasiliamali/mfanyabiashara ataanza kuona matunda/faida ya biashara. Halikadhalika hatua hii inahitaji umakini kwani kutakuwa na vitu vingi vya kufanya/kuamua kwa wakati mmoja; kwa mfano, kutumia faida kwa matumizi yako binafsi, kuongeza mtaji ama kupanua biashara yako. Yote haya yanahitaji umakini mkubwa katika maamuzi.
4. Kukua
Mara nyingi watu wengi hudharau hatua hii kwakua tayari wanapata mafanikio/faida katika biashara wanazofanya, ila wanasahau kuwa kukua kwa biashara kutawezesha kupata mafanikio zaidi na vilevile kuweza kutengeneza ajira na fursa zaidi kwa watu wengine. Maswali makuu mawili ambayo watu wengi huwa nayo katika hatua hii ni namna ambavyo watu wanaweza kukaimu majukumu yake ili kupunguza mzigo wa kazi. Pia k**a anapesa za kutosha/atakuwa na pesa za kutosha ili aweze kukuza biashara yake bila kuathiri biashara iliyopo kwa wakati huo.
5. Ukomavu wa Rasilimali
Hapa mfanyabiashara anakuwa na rasilimali watu ambao wamekomaa kiutendaji kulingana na biashara, pia kukomaa kwa rasilimali fedha ambazo zitawezesha kuwepo kwa biashara kwa miaka mingi ijayo. Ukomavu wa rasilimali utasaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati.
KUPANUKA KWA BIASHARA
Kila biashara iliyokomaa/inayoweza kujiendesha bila hasara na kuingiza faida ya kutosha inahitaji kupanuka ili kujikita zaidi kwenye soko husika na pia kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi. Zingatia yafuatayo pindi unapotaka kutanua wigo/kupanua biashara yako
1. Lifahamu Soko Lako
Tunapozungumzia kufahamu soko lako tunamaanisha kufahamu kwa kufanya tathimini ya kutosha na yenye kuridhisha kuhusu soko unalojihusisha, iwe ni kutoa huduma au kuuza bidhaa. Hakikisha bidhaa/huduma yako inaweza kuuzika kirahisi eneo husika ili isikupe mzigo wa kuanza moja kwani itakugharimu muda na pesa nyingi.
2. Wafahamu washindani wako
Jambo ambalo wafanyabiashara/wajasiliamali wengi hukosea ama kupuuzia ni namna ya kuwatumia washindani wako ili kujiimarisha kibiashara. Unapogundua/kuona umahiri wa mshindani wako katika biashara na kukubali kuwa amekuzidi basi tambua hayo madhaifu yako ambayo unatakiwa kwa namna moja ama nyengine uongeze juhudi ili kuondoa madhaifu hayo. Tunaposema washindani tunamaanisha watu wanaofanya biashara iliyosawia na yako.
3. Andaa mpangokazi wa biashara yako
Ili kutanua wigo wa biashara yako ni bora kuandaa mpango kazi ambao utakuwezesha kujitathimini utendaji wako kazi k**a umefikia malengo au laa. Hakikisha mpango kazi wako utainisha mambo muhimu k**a vile matumizi ya fedha kwani ndicho hasa kinachobeba muelekeo wa biashara, kuwepo ama kutokuwepo kwa biashara kunategemea matumizi mazuri elekezi ya fedha za biashara. Hivyo basi kuwa makini katika kuandaa au kutafuta watu wataokusaidia kuandaa mpango kazi utakao kuwezesha kuingia katika soko kwa kishindo kitakachokua endelevu.
4. Kujitangaza
Unaweza kutangaza biashara katika hatua ya kukua lakini katika hatua hii ndio wakati muafaka kutangaza bidhaa/huduma yako kwa wateja na umma kwa ujumla, kwa kufanya hivyo utatengeneza mtandao ambao utakuwezesha kukutana na wateja wako kwa wingi. Kwa kutumia mitandao ya kijamii utaweza kutoa maelezo ya huduma zako/bidhaa zako kwa urahisi na kujenga imani kwa wateja wako. Pia kutangaza biashara yako itakurahisishia kufahamu mahali gani hasa usogeze huduma/bidhaa zako kulingana na muutikio wa watu na kukurahisishia wewe kutanua biashara yako kiurahisi.
5. Ushauri
Biashara inahitaji mawazo hivyo basi tafuta watu ambao wataweza kukushauri kuhusiana na masuhala yote yanayohusiana na biashara yako hususani katika masuala ya kifedha.
KUKOMAA KWA BIASHARA
Hatua hii ni hatua ambayo mambo makuu mawili yanaweza kutokea
1. Kuendelea kwa biashara
Katika hatua hii biashara inaweza kuendelea k**a itaweza kuangaliwa kwa umakini saaana hususani katika namna ya uendeshaji kwa ujumla. Hapa ndipo biashara itakua inaingiza kiwango kikubwa cha pesa na kukunufaisha na kuona matunda ya uliyo yapanda hapo awali. Uendeshaji bora wa biashara katika hatua hii.
Kwa mfano
Matumizi bora ya pesa unayoyapata katika kipindi hichi yatakufanya uweze kumudu misukosuko ya kupanda na kushuka kwa thamani ya bidhaa zako katika soko na hata upatikanaji wa malighafi pia. Ujue wakati gani wa kutumia pesa, wakati gani wa kufanya manunuzi, kuajiri watu wenye taaluma na uzoefu n.k
Uwekezaji uliokuwa na tija kwa biashara yako. Moja katika suala ambalo watu wengi huliweka kando ni uwekezaji, kwani huhitaji mamilioni kufanya uwekezaji. Pesa unazozipata katika kipindi hiki usikubali kuziweka benki zote tafuta miradi ambayo inaendeshwa na watu wengine ambayo unaweza kufanya uwekezaji na kupata faida bila ya wewe kutumia jasho jingi saaana
Rasilimali watu. Kuajiri ni taaluma, sio kila mtu unaweza kumuweka kila mahali. Ni muhimu kuhakikisha unatumia gharama ndogo kabisa kuwa na rasili mali watu watakao leta matokeo yanayotimiza malengo ya biashara
Ubunifu wa bidhaa kuongeza hamu na shauku kwa watumiaji. Moja ya sababu ya watumiaji wa bidhaa kuwa na tabia ya kujaribu bidhaa tofauti ni Ubunifu wa bidhaa. Kwa mfano kwa bidhaa k**a vinywaji unaweza ukawa unabadilisha muonekano wa chupa kila mara, ambapo itasaidia kuonekana ni kinywaji kipya na kuendana na wakati.
2. Kufa / Kupotea kwa biashara
Kuna mifano mingi sana wa kampuni mbalimbali na biashara mbalimbali zimekufa na kupotea kabisa baada ya kufika hatua ya ukomavu. Hii imetokana na kutokuwa na maamuzi sahihi kwa wakati sahihi katika kutafuta rasilimali watu, kutokuwa na Ubunifu, uwekezaji usiokuwa na tija, matumizi mabaya ya pesa za biashara kwa mfano; kuingiza matumizi binafsi katika mzunguko wa pesa za biashara n.k
Hivyo basi ni muhimu saana k**a mfanya biashara au mjasiliamali kuzingatia mambo ya msingi yatakayowezesha biashara yako kuendelea, kukua na kuwa na Maisha bora kabisa.
Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi ujue namana ambayo unaweza kuendesha biashara yako kiufanisi zaidi.
MWANDISHI: AMRI R MGAZA
Simu: +255 673 260 990
Email: [email protected]
[email protected]