SONGA AQUA BIRD

SONGA AQUA BIRD Website is not available for now

Hii post ni ya kuzingatia saana
07/04/2023

Hii post ni ya kuzingatia saana

NGOJA NIKUKUMBUSHE KIDOGO

1. K**a ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 40, waliosoma sana na waliosoma kidogo, wote wanakuwa sawa tu, ni wakati huu majigambo ya certificates, diploma, degree, masters, PhD, hupotea kabisa. Ni katika umri huu, inawezekana mwenye elimu ndogo, akatengeneza pesa nyingi sana kuliko mwenye elimu kubwa. Waliosoma sana na waliosoma kidogo, wote wanakuwa sawa tu.

2. K**a ulikuwa haujui, ikifika umri wa miaka 50, mtu aliyesemekana kwamba alikuwa mrembo, na mtu aliyesemekana kwamba alikuwa ana sura mbaya, wote wanaanza kuwa sawa tu. Ni wakati huu, mikunjo usoni, vipara kichwani, mvi n.k, haviwezi kukwepeka tena.

3. K**a ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 60, watu wanakuwa wamestaafu kazi, aliyekuwa na cheo kikubwa na aliyekuwa na cheo kidogo, wote wanakuwa sawa tu. Ni wakati huu, hawa watu wanakuwa washikaji, wanaanza kukaa kijiwe kimoja, wanapiga story zenye idea zinazofanana, mara nyingi utawakuta makanisani au misikitini pamoja.

4. K**a ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 70, mwenye nyumba ndogo na mwenye nyumba kubwa, wote wanakuwa sawa tu, wote wanahitaji nafasi ndogo sana ya kukaa, kwa kuwa ni katika kipindi hiki, kuhamisha-hamisha vitu, inakuwa taabu sana. Mwenye ghorofa atapenda kukaa nyumba ya chini, kwa kuwa miguu yake inaanza kukosa nguvu. Ni wakati huu, watoto huwaachia nyumba na kwenda kuanza maisha yao, hivyo, nyumba huwa kubwa kuliko mahitaji.

5. K**a ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 80, walio na pesa na wasio na pesa, wote wanakuwa sawa tu, hata mwenye pesa anapotaka kutumia pesa zake, anakuwa hajui wapi pa kwenda, wote tajiri na masikini, hubaki nyumbani tu.

6. K**a ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 90, kulala usingizi na kuamka, vyote vinakuwa sawa tu, kwa kuwa hata ukiamka, unakuwa huna cha kufanya,hapa masikini na tajiri, wote wanasubiri kifo tu.

Katika maisha, k**a wewe ulidhani ni mtu muhimu kuliko watu wengine, kwa sababu ya elimu,uzuri,nafasi yako kazini, nyumba,au kipato chako kuwa kikubwa. Basi ulikuwa hujui tu,wewe ni wa kawaida sana, hakuna mtu mwenye nafasi kubwa kuliko mwingine, ni suala la muda tu.

Naomba kuwasilisha

👇🏼

SHEBA link my bio

JINA LA SHAIRI : SHIFAA MTUNZI; SONGA RJ20/03/2023Niko hoi taabani, homa imeni andamasiumwipo maungoni, Bali ni ndani ya...
20/03/2023

JINA LA SHAIRI : SHIFAA
MTUNZI; SONGA RJ
20/03/2023

Niko hoi taabani, homa imeni andama
siumwipo maungoni, Bali ni ndani ya nyama
maumivu ya moyoni, upweke wani sak**a
Habibat ni shifaa, nyongo mkalia ini

sikuwahipo kudhani, kwamba nitakuwa hivi
Kuhisi Niko shidani, sababu malavidavi
Ninakumisi mwandani, k**a mapenzi ya muvi
Habibat ni shifaa, nyongo mkalia ini

kumbe kuwa mbali nawe, ni tabu namna hii
Nina jihisi kiwewe, sijiwezi sisikii
mawazo yangu ni wewe, Huna baya ma thanii
Habibat ni shifaa, nyongo mkalia ini

ni kweli kazi ni ngumu, Ila Bado napambana
malengo yetu muhimu, twawatafutia Wana
weye kwangu maalumu, wakufa na kuzikana
Habibat ni shifaa, nyongo mkalia ini

Nionapo simu Yako, homa yangu Inashuka
na hiyo sauti Yako, ndio tiba iso shaka
nikisikia kicheko, amani yaimarika
Habibat ni shifaa, nyongo mkalia ini

kinacho nipa faraja, nikuona upo nami
siku bado zinakuja, pia utakuwa nami
upendo hauto chuja, mahabatani sihami
Habibat ni shifaa, nyongo mkalia ini

Weye kwangu matibabu, honey wanipa shifaa
Nakupenda mahbubu, penzi tele limejaa
Mie ni wako habibu, baba yake na thaniaa
Habibat ni shifaa, nyongo mkalia ini

Jina la shairi: DEGREE YANITESAMtunzi : SONGA RASHIDY17/02/2023Nahama nyumbani kesho, yamenifika rohoniSasa hii ni micho...
17/02/2023

Jina la shairi: DEGREE YANITESA
Mtunzi : SONGA RASHIDY
17/02/2023

Nahama nyumbani kesho, yamenifika rohoni
Sasa hii ni michosho, yakunyimana amani
sihitaji amrisho, nahamia ubakini
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

Hii nyumba yetu sisi, tunaye baba na mama
nyumba Haina nafasi, tumezaliwa mapema
mkubwa Nina jihisi, niharakishe kuhama
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

Najuta kukaa hapa, baada ya kumaliza
Sasa Nina tapa tapa, maneno yanaumiza
Kwa mola wangu na apa, nauomba muujiza
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

kila ninacho kifanya, nambiwa Sina bidii
Nikiacha kukifanya, nambiwa sisaidii
Magumu nambiwa fanya, kutumia digirii
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

Baba anavyo amka, unikuta Niko macho
hunifanyia dhiaka, ajua kitu sinacho
kwa sauti anawaka, kwamba digirii chocho
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

Ninapewa kazi nyingi, nifanye kwa digirii
zinataka nguvu nyingi, Wala sio digirii
najikaza Mara nyingi, kijana wa digirii
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

vijana wa maskani, madili wana ninyima
Wana uchungu moyoni, ishu kubwa ni kusoma
Wasema waofisini, hawawezi kujituma
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

Warembo wa mtongani, kariakoo na buza
Bwejuu, paje, chukwani, pesa ndio huchunguza
Kibuki wa kikwajuni, kwa pesa wajipoteza
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

Nafunguka ya moyoni, kwa majirani na baba
mwatuweka utumwani, hakuna mateso haba
kwahiriwa twatakani, Ila ajaira ni haba
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

k**a ni kujiajiri, mazingira si rafiki
vyanzo vya mitaji ghari, bidhaa Bei ni dhiki
elimu imetughuri, maisha hayosoviki
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

vijana tupambaneni, mtaani ni kugumu
usomi tuuachini, turudini kwenye gemu
pia tujiajirini, kazi zilo kwenye damu
Digirii yanitesa, kukaa nyumbani Basi.

it was miwaleni spring
04/02/2023

it was miwaleni spring

the logo that bright
20/01/2023

the logo that bright

our workers are full responsible
26/03/2022

our workers are full responsible

I has born
22/02/2022

I has born

Welcome all clients and friends
20/01/2022

Welcome all clients and friends

we aim to entertain you 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
14/01/2022

we aim to entertain you
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

14/01/2022
K**a hutaki sikulazimishi jamaniiiiiii
14/01/2022

K**a hutaki sikulazimishi jamaniiiiiii

Address

Kikwajuni Juu
Zanzibar
22.02.2022

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SONGA AQUA BIRD posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to SONGA AQUA BIRD:

Share