23/04/2026
Ukikwepa haya, umekwepa safari nzima ya kufanikiwa
⸻
1. Kuanza kabla hujawa tayari
Utasubiri sana hadi ujione uko “tayari”… na hiyo siku haitakuja.
Wanaoshinda wanaanza hata k**a mazingira bado hayako Sawa 100%, wanajifunza njiani.
Ukisubiri kikamilike, utaishia kuangalia wengine wakifanikiwa na wewe hutokuja kuanza.
2. Kujipambania mwenyewe
Hakuna mtu anakuja kukuokoa.
Hakuna “destiny helper” atakayekuja na mtaji mkononi, Connection na fursa na kukutafuta ulipo
Ukisubiri msaada, muda unapita. Ukijisukuma mwenyewe, mlango unafunguka.
3. Kupuuzwa
Utafanya vitu vizuri, watu hawatajali.
Wengine wasio na uwezo k**a wako ambao wanafanya vitu k**a vya kupuuzia hivi watapata attention kuliko wewe. Hilo lisifanye uone hauko sahihi
Hata kazini unaweza kuwa bora ndo watu wakaleta unafiki kwako, mtandaoni ndio kabisaaaa
Kosa kubwa ambalo hupaswi kufanya ni wewe kujipuuza na kupuuza uwezo wako
4. Ugumu wa kuanza
Mwanzo utakuwa mgumu, utachanganyikiwa, utajiona hujui unachofanya.
Hii ndio stage wengi wanaacha. Wanaishia kujipanga...
Ugumu wa mwanzo sio ishara ya kushindwa, ni sehemu ya mchakato.
5. Kukatishwa tamaa na watu wako wa karibu
Watu wa karibu watakuambia:
• “hiyo haiwezekani”
• “tafuta kazi tu” Unapoteza muda
Unapaswa kujua kuwa wao Wanaongea kutokana na hofu zao, sio uwezo wako.
6. Matokeo kuchelewa
Utafanya kazi sana… lakini matokeo hayaji haraka.
Hapa ndipo wengi wanakata tamaa na hawataki kusikia.
Mafanikio yanaweza kuchelewa kukujibu, lakini yakija yanabadilisha kila kitu.
Kuchelewa kwa matokeo haimaanishi hufanyi kitu sahihi ...
Ukikwepa haya…
umekwepa safari nzima ya mafanikio.
Kitu gani katika haya unakipitia au umewahi kukipitia ila haijawahi kukukatisha tamaa?