21/04/2017
HISTORIA FUPI YA MKOA WA
MBEYA.
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa
minne (4) iliyopo katika Nyanda za
Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa
mingine ni Rukwa, Iringa na Ruvuma.
Mkoa wa Mbeya ulianzishwa mwaka
1961 na ulikuwa ukijulikana kwa jina
la ‘Southern Highland Province’ kwa
kujumuisha baadhi ya maeneo ya
mikoa ya Iringa na Rukwa. Mkoa una
eneo la km. za mraba 63,617 Kati ya
hizo km. za mraba 61,783 ni za nchi
kavu na km. za mraba 1,834 ni eneo la maji.
Kulingana na Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 1967 mkoa ulikuwa na watu 969,053, Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 Mkoa wa Mbeya ulikuwa na jumla ya watu 2,063,328.
Kufikia mwaka 2010 mkoa ulikadiriwa kuwa na watu 2,662,156. Mkoa wa Mbeya upo kusini magharibi mwa eneo la Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mkoa upo katika Latitudi kati ya 7º na 9º 31’ kusini ya Ikweta na Longitudo kati ya 32º na 35º mashariki ya Greenwich. Mkoa unapakana na nchi za Zambia na Malawi upande wa kusini, Mkoa wa Rukwa upande wa magharibi, Mikoa ya Tabora na Singida kwa upande wa kaskazini ambapo kwa upande wa mashariki unapakana na Mkoa wa Iringa. Mji wa Tunduma katika
Wilaya ya Mbozi na Kasumulu katika
Wilaya ya Kyela, hufanya milango ya
kuingilia na kutokea nchi za Zambia
na Malawi.
Katika enzi za ukoloni wa Waingereza,
Mkoa wa Mbeya ulikuwa ukijulikana
kwa jina la ‘Southern Highland Province’. Mkoa ulikuwa ukiunganisha
baadhi ya maeneo ya mikoa mitatu ya
sasa ambayo ni Iringa na Rukwa. Jina
la Mbeya limetokana na neno la kisafwa."Ibheya" ambalo maana yake ni chumvi, kutokana na wafanyabiashara kufika.na kubadilishana mazao yao kwa chumvi.
Mji wa Mbeya uliendelea kupanuka pande zote isipokuwa eneo la Kaskazini lilitawaliwa na milima. Ujio wa Wanyakyusa kutoka Rungwe ndiyo ulioleta Uluteri mjini Mbeya.
Kabila la Wasafwa ndiyo wenyeji halisi wa mji wa Mbeya, na hata ukiangalia asilimia kubwa ya majina ya maeneo ya jiji hili ni ya kisafwa mfano uyole, igawilo, loleza, ituha N.k
Mji wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo mwaka 1927. Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana katika milima iliyopo karibu na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa, hali iliyosababisha mji wa Mbeya kupewa jina la utani k**a "The Scotland of Africa" baada ya kutambua k**a uoto, hali yake ya hewa na muonekano wa milima (hills) inayouzunguka mji wa Mbeya kufanana na Scotland mfano uoto unaopatikana katika mlima Loleza. Mkoa huu ni
moja kati ya mikoa mikongwe tisa (9)
iliyokuwepo mpaka wakati wa uhuru
mwaka 1961.
Katika kipindi hicho, makabila makuu
katika Mkoa wa Mbeya yalikuwa ni Wasafwa, Wanyakyusa, Wandali,
Wasangu, Wamalila, Wanyiha, wakimbu na Wanyamwanga. Ambapo jamii hizo ni maarufu kwa kujishughulisha na kilimo na ufugaji mdogomdogo.
Karibu kila wilaya ipatikanayo mkoa wa Mbeya inakabira moja la wenyeji k**a ilivyo ainishwa; wilaya za mbeya mjini na vijijini wenyeji ni Wasafwa, Wenyeji wa wilaya za Rungwe na Kyela ni
Wanyakyusa. Wenyeji wa wilaya ya Ileje ni Wandali. Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu ingawa watu waishio huko zaidi ni Wanyiha. Wenyeji wa wilaya ya Mbozi ni Wanyiha na Wanyamwanga,
Kijiografia, Mkoa ulianzishwa katika
maeneo yanayojulikana hivi sasa
k**a Uhindini, Uzunguni na Majengo. Mji ulipangwa kufuatana na.kawaida ya miji ya kikoloni ya Afrika Mashariki kuwa na sehemu tatu.zifuatazo;
(i) Uzunguni k**a sehemu ya
nyumba za Wazungu na kando yake ofisi za serikali.(Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Polisi na Mahak**a)
(ii) Uhindini k**a mtaa wa biashara uliokuwa mikononi mwa.wafanyabiashara wenye asili ya Kihindi na Kiingereza
(iii) Majengo k**a sehemu kwa
ajili ya wafanyakazi Waafrika na familia zao.
Kwa upande wa masuala ya kiimani,
Mkoa ulikuwa umegawanywa k**a
ifuatavyo;
(i) Kanisa Anglikana lililokuwa dhehebu rasmi la Uingereza ambalo lipo chini ya eneo la Uzunguni karibu na ofisi za
kiserikali k**a Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mahak**a.
(ii) Kanisa la Moravian la mjini.lilijengwa eneo la Majengo iliyokuwa sehemu kwa ajili ya makazi ya Waafrika.
(iii) Kanisa Kuu Katoliki lililokuwa
maeneo kati ya Uzunguni na Uhindini karibu na Majengo ambalo lilihudumia Wazungu wachache hasa Waeire na Wahindi kutoka Goa na Waafrika wachache.
Kwa upande wa masuala ya uchumi
Mkoa wa Mbeya ulitegemea kilimo cha
mazao ya chakula yakiwemo mahindi,
viazi vitamu, mtama, mpunga na ndizi. Shughuli nyingine zilikuwa ni biashara na viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza zana za kilimo.
Kielimu, shule zilizokuwepo zililenga
hasa kutoa elimu kwa watoto wa
machifu, wazungu na wahindi. Shule hizi zilikuwa zinamilikiwa na serikali na mashirika ya dini. Shule za serikali zilijulikana k**a ‘Native Authority’ na za mashirika ya dini ziliitwa shule za wamisionari. Waalimu wazalendo walikuwa wachache, wengi wao walikuwa ni wazungu. Misheni ya Rungwe ndiyo pekee iliyokuwa na Chuo cha Elimu katika Mkoa wa Mbeya baada ya uhuru.
Kuhusu huduma za afya, jamii kwa
kiasi kikubwa ilikuwa inatumia tiba za kienyeji. Hospitali zilikuwa chache zikitoa huduma bure isipokuwa hospitali za wamisionari.
Kisiasa, mkoa umekua ukitawaliwa na wakuu wa mikoa kadhaa tokea kuanzishwa kwake mpaka sasa ambao ni; Mh Seleman Kitundu, mh Waziri Juma (1964-1964), John B Mwakangale (1964-1965), Aaron Mwakang'ata (1965-1967), Osward Marwa (1967-1971), Peter Siyovelwa (1971-1973), John Shija(1973-1975), Richard Wambura (1975-1977), Kingunge Ngombale Mwilu(1977-1982), Chrisant M Mzindakaya(1982-1982), Michael Baruti (1982-1983) Meja jenerali (mst) Makame Rashidi (1983-1989), Nalaila Kiula (1989-1990), Zakhia Meghji (1990-1990), Azan Aljabri (1990-1990), Paulo P Kimiti (1991-1995), Basil P Mramba (1995-2000), Mateo T Qares (2000-2006), John l Mwakipesile (2006-2011), Abbas H Kandoro (2011-2016) Amos Makala (2016 mpaka wakati huu